Uzinduzi wa mtandao wa 5G Afrika ni ishara ya uongozi wa China duniani kwenye enzi mpya

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
VCG41N1211073843.jpg
Mwaka 2015, China ilitangaza kuwa itaongeza maendeleo ya dijitali kuwa sehemu ya miradi ya Ukanda Mmoja na njia moja.

Hii ni njia moja ya kutosheleza mahitaji yanayoongezeka ya mtandao wa kasi ambao unategemewa na mamilioni ya biashara kila siku hasa kwenye nchi zinazoendelea.

Tayari China ilikuwa imeanzisha miradi ya Ukanda mmoja na njia moja mwaka 2013, inayohusisha ujenzi wa barabara, viawanja vya ndege, bandari na miundo mbinu mingine ya kuwezesha biashara.

Lakini kwa kuzingatia hali halisi na ulazima wa teknolojia ya kasi, barabara au reli bila intaneti haijakamilika.

Na ili kufanikisha lengo hilo la kuwepo kwa huduma ya 5G kampuni ya teknolojia ya Huawei ya China mwaka 2019 ilizindua simu ya mkononi inayotumia teknolojia ya 5G nchini Uingereza.


Athari chanya za ujio wa 5G Afrika
Kanda ya Afrika mashariki Kenya imekuwa nchi ya kwanza kuanza kutumia kwa majaribio huduma ya 5G.

Kwenye uzinduzi wa huduma hiyo waziri wa Habari na Teknolojia Joe Mucheru alisema ni hatua muhimu ya “kuweka msingi imara kwa kizazi kipya cha wavumbuzi na wajasiriamali.

Kwa mujibu wa kampuni ya Huawei ya China ambayo ni mshirika wa kuendeleza huduma hiyo, 5G inaweza kuunganisha zaidi ya vifaa milioni 1 katika eneo la kilomita moja mraba ikilinganishwa na 4G ambayo inaweza tu kuunganisha vifaa 100,000 katika eneo sawa na hilo.

Waziri Mucheru anasema hiyo inafanya kasi ya huduma ya 5G kuunganisha kwa haraka biashara za utengenezaji bidhaa na mnyororo wa usambazaji kwenye biashara.

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom inashirikiana na Huawei na Nokia kuleta huduma hiyo nchini kenya.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Safaricom Peter Ndegwa, majaribio yataanza na wateja wa kampuni hiyo mjini katika mji mkuu Nairobi na miji mingine na baadaye kuongeza hadi zaidi ya maeneo 150 ndani ya kipindi cha miezi 11 ijayo.

Ndegwa anasema lengo la msingi la kipindi cha majaribio litakuwa kutathmini kama wateja watafurahia kasi ya hadi Mbps700 huku ikiwa na mpango wa kutoa kasi zaidi ya Mbps 1,000 katika miezi ijayo.

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo Duniani, UNCTAD biashara ya mtandaoni Barani Afrika inakua kwa wastani wa asilimia 14 kwa mwaka.

Na ripoti ya kituo cha biashara cha kimataifa ITC ya 2021 inaonesha kuwa Afrika ilikuwa na masoko 631 ya mtandaoni hadi mwishoni mwa 2019.

Lakini changamoto kwa masoko hayo ni pamoja na ufikiaji mdogo a ukosefu wa intaneti. Mwaka wa 2017, kwa mfano, ni asilimia 30% tu ya Waafrika wangeweza kupata huduma ya intaneti.

Ripoti ya ITC inasisitiza kuwa wanawake lazima wawe na huduma za uhakika za intaneti ili kuwawezesha kushiriki ununuzi na uuzaji wa mtandaoni.

Kuelewa huduma ya 5G

5G hutumia mawimbi ya redio kusambaza na kupokea data kati ya antena au mlingoti na simu yako.

Inategemea masafa ya redio ya juu kuliko teknolojia ya awali ya rununu.

5G inafaa zaidi kwa maeneo ya yenye miji yenye watu wengi wanaotumia intaneti kwa wakati mmoja.

Hii ndiyo ya kasi zaidi kwa sasa.

Kwa kutumia 5G, tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.

G5 inajibu mahitaji ya watumiaji

Mwishoni mwa mwaka 2020 Mamlaka ya mawasiliano ya mji wa Beijing ilitangaza kuwa idadi ya watumiaji wa huduma ya intaneti wa 5G mjini Beijing imeongezeka na kuwa zaidi ya milioni 5, kufuatia uzinduzi rasmi wa huduma hiyo kibiashara mwaka 2019.

Kuanzia mwezi Agosti 2020 jumla ya vituo 44,000 vya 5G vimekuwa vikitoa huduma mjini Beijing.

Hata hivyo serikali na mamlaka husika nchini China inafahamu kuwa ufanisi mkubwa wa huduma ya 5G utawezekana kwa kushirika nchi nyngi duniani ili kuwa na hatma ya pamoja.
 
Sipendi Mmarekani ambavyo ameshindea kushindana na kasi ya Mchina anaamua kumfanyia fitina badala ya kushindana naye kwa usawa.
Ila pia mchina mimi simuamini hata robo hasa anapodeal na sisi waafrika
 
Ila mchina ana roho ngumu hakati tamaa pamoja na vikwazo lkn bado anasonga,hii spirit ndio inaufanya uchumi wao uendelee kustawi kwa kasi.Hawa jamaa kuwatoa kwenye reli ni kazi sana.
 
Back
Top Bottom