Uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru butiama aibu tupu

COMPLICATOR2011

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
253
35
Nafuatilia kipindi cha uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru tbc1, kwa kweli ni aibu tupu watu ni wachache sana achilia mbali hao waliova sare ambao naamini wamelipwa perdiem na taasisi zao ndio maana wako hapa. Kiufupi uzinduzi haujafana. Hlf kuna maswali 2 nataka niulize;
1. Kwa nini sherehe hizi mbili ziunganishwe maana naona sasa maana harisi ya kumbukumbu ya mwl. Nyerere haipo au ndio kutaka kumsahau kiaina?
2. Hivi mwenge huu wa uhuru unakimbizwa tanganyika tu au na zanzibar pia, kama ni tanganyika tu ni kwa nini uwemo kwenye vielelezo vya nguzo au alama za Taifa la tz.
 
Mkuu mbona sherehe ziko shega tu!! Kwa kijijini watu wale ni wengi. Naona wakurya wanacheza ngoma mbalimbali kama vile Ilitungu, Lilandi na kadhalika. Mwenge wa uhuru unakimbizwa na huko Tanzania Zanzibar.
 
Mwenge utakimbizwa Unguja pamoja na Pemba kwa mujibu wa Shabani Kissu(mtangazaji).
-lkn watu ni wachache kwasababu hawajui wanaenda kwenye hivyo viwanja kwa lipi: kuenzi miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa au wanaenda kwa shuguli za kuasha Mwenge!!!!. Kwa mtazamo wa haraka Watanzania Mwenge wameisha uchoka kwani hauna Dili tena na hao watu wachache wanaonekana viwanjani ni kwa ajili kumuenzi Baba wa Taifa tu.
 
mwaka jana ulilala huku kwetu asubuhi kulikuwa na bahari ya kondom zilizotumika......
 
Jamaa anasema ukiwa unakimbiza mwenge hata ukifiwa, ukiumwa utakiwa kuacha.
 
vita vya kagera watu wote walishiriki hata ambao hawakuenda walichangia vyakula kama ng'ombe. Mbona wakati huu wananchi hawaoni umoja na serikali yao wala wao tu?. Ikitokea vita mi siendi ujinga huu. Wataenda nape, riz, baba riz wanaofaidi nchi na mafisadi wenzao.
 
Lakini nasikia hali ya hewa sio nzuri so inawezekana hicho ndo kizingiti cha watu kujitokeza.lakin pia ikumbukwe kua Butiama ni kijiji so kwa hali nnavoiona hali sio mbaya,
 
Mwenge utakimbizwa kwa muda gani? Mbona wamechelewa kuuwasha?
 
Natamani kwenda kwenye kumbukumbu za mwalimu lakini sitaki kuonekana kwenye mbio za mwenge.
Mbio za mwenge kwa sasa ni mradi tu wa wachache kujineemesha.
 
Acheni kuangalia hayo mambo ya kipuuzi, tune ITV ufuatilie mambo ya maana kwenye Kigoda cha mwalimu
 
Wakuu, hakuna kitu kinachonipa kichefuchefu kama mbio za mwenge wa uhuru. Hazina faida na hazitakuwa na faida yoyote kwa mwananchi wa kawaida anayeshinda na kulala njaa kila siku.
 
zile ndo nguo huyo baba wa taifa alikua anavaa?naona hazina sehemu ya kuvalia tai.
 
Mwenge utakimbizwa kwa muda gani? Mbona wamechelewa kuuwasha?

Mwaka huu mwenge utakimbizwa kwa kipindi kisichozidi siku 57; tofauti na miaka yote, mwaka huu mwenge utapita kila makao makuu ya mikoa tu, na sherehe za kuzima mwenge zitaenda sambamba na kilele cha miaka 50 ya UHURU. Hivyo sherehe za kuzima mwenge zifanyika jijini DSM, Disemba 9, 2011. Utazimwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Tz, Dr. Jakaya Halfani Mwinyikambi Mrisho Kikwete katika uwanja wa UHURU. Nyote mwakaribishwa, burudani mbalimbali kutoka mikoa yote ya Tz zitakuwemo!!!!!
 
Mwenge hauna mvuto kwani ulishapoteza maana yake.......................sasa hivi mwenge umekuwa sehemu ya mafisadi kujipumzisha na kukusanya michango
 
Nimekumbuka mbali sana, HALAIKI inapendeza sana na sherehe ni bomba! Ukilinganisha idadi ya watu wa kijijini na mahudhurio, kwa kweli watu ni wengi
 
Back
Top Bottom