Uzinduzi wa Leseni Kwa wahandisi waliosajiriwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzinduzi wa Leseni Kwa wahandisi waliosajiriwa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tangawizi, May 17, 2011.

 1. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Leo, Dr. Magufuli ambaye ni waziri wa ujenzi amezindua rasmi matumizi ya leseni kwa ajiri ya practising engineers and engineering consultants kama sheria inavyoelekeza.
  Moja ya mambo muhimu aliyoyagusia ni bodi ya wahandisi sasa kuwa mstari wa mbele kutoa ushauri mbadala kwa serikali katika mambo muhimu yanayohusu uhandisi, bila kusubiri kutumwa au kusukumwa kama ilivyo sasa.
  Kwa mtazamo wangu, Magufuli amesema kitu muhimu sana maana imekuwa kama ni tabia sasa wahandisi kuacha fani na kuwa wanasiasa hata kwa kazi zilizo za kitaalamu.
  Bila ushiriki wa dhati wa wahandisi katika kuhakikisha ubora wa kazi zinazofanywa na kupiga vita rushwa, nchi hii haitakaa kuja kujengeka. Ni aibu kuona wahandisi wanachangia kwa kiasi kikubwa kuchakachua ubora wa kazi zinazofanywa....naamini Dr. Magufuli ametoa changamoto....kazi kwa wahandisi sasa kuona nasi tunacheza sehemu yetu....tukumbuke, heshima yetu itajengwa na matendo yetu na siyo vinginevyo!! Tuache kupiga domo na kuwa waadilifu tukifanya kazi.
   
 2. m

  mushi.richard Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Jul 31, 2007
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lazima wawe na impact kwenye jamii na sio kuwa majina tu Eng. so and so!
   
 3. Bon

  Bon Senior Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama itapunguza kasi ya professionals kwenda kwenye siasa, tatizo kuu malipo, ineonekana siasa inalipa kuliko professions.
   
Loading...