Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA waendelea, Kawe kumewaka moto leo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,363
217,395
Rais Mtarajiwa wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea Urais wa Chadema Mh Tundu Lissu, ambaye wachambuzi wa kisiasa wanamkadiria kujinyakulia zaidi ya 70% ya kura zote, leo tena anaingia kwenye viwanja vya Tanganyika Packers kuongea na wananchi.

=====
LIVE FEED:



MBOWE: HATUOGOPI TBC WALA SERIKALI. TBC WAKIJITAFAKARI TUPO TAYARI KUWASAMEHE

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwa katika Kampeni za CHADEMA, Kawe Jijini Dar amesema jana katika Mkutano wao wa Mbagala waliwataka TBC kuondoka, jambo lililopokelewa vema na Watanzania wengi husasan wale wanaopenda Uandishi wa Habari wa haki

Amesema, "Napenda niwaambie Wanahabari wote, Chama chetu kinaamini katika Uhuru wa Habari, kinamini katika Uandishi wa Habari unaofanywa kwa Weledi, usio na upendeleo"

Amesisita, "Chombo chochote kinachotaka kutoa taarifa zetu, tunakiruhusu, tunakikaribisha, tutashirikiana nacho lakini kitoe taarifa za ukweli bila upendeleo bila ushabiki"

Ameongeza, "TBC wametoa tamko. Wanasema taarifa wametoa Polisi, sisi taarifa tumetoa kwa Mungu. Tunapenda kuwambia TBC, Polisi imekuwa sehemu ya maisha yetu wala hatutishwi na mtu kwenda Polisi kutushtaki"

Amesema TBC wajitafakari na wakiona wapo tayari kufanya kazi kwa uadilifu, CHADEMA ipo tayari kuwasamehe ila sio kutishana kwa sababu wao hawaiogopi TBC wals Serikali ila wanawaheshimu wote na taaluma ya habari

Kawe ( 451 X 640 ).jpg
 
Kumtoa mtu ndani kwake hadi aje kusikiliza sera zako ni jambo ambalo linahitaji technique nyingi. Kwanza hamasa

CHADEMA hamkua na hamasa yoyote ya kuhamasisha watu juu ya uzinduzi wa kampeni yenu, amsha amsha hazikuepo kama zile enzi za Dkt. Slaa.

Hamkua na vitu vya kushawishi watu waje zaidi ya Lissu, hamuoni CCM wanakodi mpaka wasanii ili wajaze uwanja?

CHADEMA mnafeli, Katibu Mkuu umefeli.

Kiujumla mmefeli nyote na mkiendelea hivyo hivyo mtapoteza mvuto kabisa.
 
Kwa Nini walishindwa media coverage?

Chadema mngewalipa ITV Cash. Ili warushe matangazo

Promotion ilikuwa hafifu, pa system isiwe moja.

Mlishindwa kuita wasanii na kuwalipa?
 
Back
Top Bottom