Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mungi, Oct 6, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,996
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Kwanza kabisa niwapongeze mods kwa busara zao za kipekee, maana kama siyo wao leo hii ningekuwa naendelea kuugulia ban.

  Muda huu nipo kwenye eneo la mkutano wa uzinduzi wa kampeni katika uwanja wa Ndarvoi uliopo katika kata ya Daraja mbili.

  Watu wanaendelea kuingia kwenye eneo la mkutano, tutaendelea kuwajuza kwa kila kitakachokuwa kinaendelea.

  Jf daima!

  Yupo pia Pepe mwimbaji machachari wa nyimbo peoples power, amekuja na cd za matukio ya M4C, zinaonyesha mpaka tukio la mauaji ya Daudi Mwangosi aleliyeuawa na polisi pamoja Ally Zona aliyeuawa morogoro

  UPDATE:
  Tayari makamanda Lema, Milya, na Nanyaro wameshaingia uwanjani.
  Uwanja umefurika. Picha mtazipata.
  Mkutano unafunguliwa kwa dua.

  JAMES MILYA:
  Ndugu zangu ni mara yangu ya kwanza kumnadi mgombea wa chama changu kipya kumnadi mgombea wa chama chetu tokea nilipovua gamba.
  Tumedhamiria kubadilisha hali ya kisiasa nchini kwa vitendo, tuhakikishe tunamchagua diwani wa cdm.
  Inasikitisha Mnally aliyewachapa viboko waalimu akafukuzwa, leo ccm wanamchagua kuwa kiongozi.
  Ndugu zangu tunamleta kamanda msofe (mgombea), mchagueni akawashughulikie panya kwenye halmashauri yetu.
  Mtupatie jembe hili litusaidie kwenye harakati za kuleta maendeleo.
  Nimekuwa ccm, wana agenda tatu tu.
  Agenda ya kwanza, kufungua kikao, ya pili muhtasari wa kikao kilichopita, ya tatu, kujadili hali ya kisiasa nchini. Hawajadili kero za wananchi.
  Taarifa za ccm:
  ndugu zangu watu hawa ilikuwaonyesha kuwa wamepata nguvu ndani ya arusha, wamedhamiria kutembea kila kaya, wako tayari hata kugawa laki kwa kila mtu. Hivyo pokeeni hizo hela ni za kwetu, kura tumchague kamanda msofe.

  NANYARO:
  ndugu zangu, leo hii tupo mbele yenu, na daraja mbili ni zaidi ya jimbo, na nimfikishie salamu mgombea wa ccm bw. Mushi, kuwa chadema tuna diwani wa daraja mbili, ccm wana mgombea wa daraja mbili.
  Chadema tunasema kuna manunuzi ambayo tunaweza kufanya nje ya vikao kwa maendeleo ya wananchi.
  Tuna mambo ya msingi ya kutaka kuokoa maisha ya wananchi.
  Kuwaondoa wamachinga mjini ni bomu ambalo litalipuka si muda mrefu.
  Kamanda Nassari amekamua vya kutosha.

  LEMA:
  wali wakushiba unauona kwenye sahani, hapa biashara imekwisha.
  Milya anaendelea kutupa taarifa kuwa vijana wake aliowaacha ccm wanampa taarifa kuwa ccm wameaanda zaidi ya mil 500, wapo tayari kutoa laki kwa kila mtu ili washinde hii kata.
  Tumeanzisha M4C, tumegawana kwa kanda, mimi nimepangiwa kanda ya kaskazini. Umaskini siyo uadilifu, tunapiga vita umaskini usiku na mchana. Leo umaskini unaendelea kuwakandamiza watanzania, tutapiga umaskini vita hata kwa figo zetu.
  Ndugu zangu hatuwezi kuichagua ccm, maisha ni ngumu hali ni mbaya.
  Kazi ya chadema ni kupiga vita ujinga, na kuwaelimisha watanzania.
  Msofe tunakutuma kwenye halmashauri, kazi yako ni moja, pigania wanyonge, wewe ni baunsa, katumie ubaunsa wako kuwashughulikia panya wa halmashauri.
  Lengo la chadema siyo kushinda, lengo la chadema ni kushinda na kulinda haki na uadilifu, tuwapate watu watiifu wakuwaongoza watu. Ukileta zakuleta tunakumwaga chini.
  Kitu ambacho kikwete atasababisha katika nchi hii ni kumwaga damu za watanzania kwa misingi ya udini.

  Picha:

  DSC03720.JPG
  Kamanda Lema akimtambulisha mgombea udiwani wa kata ya Daraja II Bw. Msofe


  DSC03706.JPG Kamanda Lema akitoa usia
  DSC03705.JPG Mbunge aliyeko Honeymoon akikamua jukwaani
  DSC03702.JPG Umati wa wananchi waliohudhuria Mkutano wa uzinduzi wa kampeni Daraja Mbili
  DSC03704.JPG
  Dongo Janja na Lema hawakufahamiana barabarani.

  [​IMG]
  Kada maarufu wa CCM Mzee Zacharia akikabidhiwa kadi ya chadema, tukio likishuhudiwa na Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Arusha Kamanda Nanyaro (kushoto), Mbunge Lema na Msofe wa pili kulia
  DSC03695.JPG Kamanda Ephata Nanyaro akikamua jukwaani
  DSC03684.JPG
  Umati ukishuhudia uzinduzi wa kampeni
  Umati 3.JPG Wali wa kushiba unauona kwenye sahani
  Pepe na shabiki machachari wa chadema.JPG
   

  Attached Files:

 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #81
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 34,055
  Likes Received: 41,756
  Trophy Points: 280
  Nassari: anazungumzia watuhumiwa wa mauaji ya mwenyekiti wa cdm arusha.
  Anasema polisi wanavujisha siri za wasamaria waliofichua siri za wauaji.
  Anasema kutoroka kwa watuhumiwa hao ni maigizo.
  Anatoa taarifa kwa wanausalama kuwa wasipowapata wauaji hao hapa arusha hapatakalika.
  Kikwete anaambiwa kuwa hajamuumba mtu hata mmoja ana mamlaka ya kuua hata mmoja.
  Anasema ccm wakileta t.shirt wananchi wawaulize mbona hawajawapima size???
  Nassari anasema daraja II kutuma salamu kuwa arusha ni kisima cha mabadiliko.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 3. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #82
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi daraja mbili ni maeneo gani hapo arusha? Ni nje ya mji?
   
 4. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #83
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,246
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Ndungu yangu nakushauri tafuteni shughuli za kufanya mnatumiwa bila kufahamu jaribuni kujitathimini upya na uamuzi wenu.
   
 5. Nyiluka

  Nyiluka Member

  #84
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hivi CUF hawajaweka mgombea?
   
 6. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #85
  Oct 6, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Mkuu Mungi,
  Rekebisha hapo kwenye red. Najua ni typing error
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. a

  adolay JF-Expert Member

  #86
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,774
  Likes Received: 3,404
  Trophy Points: 280
  Badala ya kujadili mkutano na jinsi ya kukipamba chadema, wachovu wawili wanadraw attention na kuwatowa kwenye

  maada wapotezeeni hao. mkiendeleza majadala nao mtapoteza muelekeo wa hoja ya mkutano na ukombozi wa M4C kwa

  watanzania.
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #87
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 34,055
  Likes Received: 41,756
  Trophy Points: 280
  Lema kapanda jukwaani sasa:
  Anasema tuinamishe kichwa tumshukuru mungu kwani tumeshashinda.
  Anaanza kwa kusema wali wa kushiba unauona kwenye saani(ana mnukuu vicent nyerere)
  Anasema ccm wametenga milioni 500 kila nyumba itagawiwa laki 1. Anasema chakula kikiletwa wananchi wale.
  Anasema chama chetu hatuamini kwenye umaskini ndo maana tunapiga vita umaskini usiku na mchana.
  Lema anazidi kulonga kuwa hatuwezi kuwa na chama kinachotumia nembo ya jembe na nyundo wakati kuna watu wanalima kwa matrekta ya kukodi kwa bei ghali.


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #88
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,246
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu chama,
  Kwa wastani Chadema wanafanya mikutano Arusha kwa mwezi mara 20 kwa miezi sita wanafanya mikutano 120 wastani wa mkutano mmoja wanatumia milioni 30...kwa miezi 6 wanatumia zaidi ya milioni 300 ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #89
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wanamuunga mkono mgombea wa CCM
   
 11. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #90
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 34,055
  Likes Received: 41,756
  Trophy Points: 280
  Lema: anasema tutapiga chini bila kujali kuwa tutakosa madaraka kwani madaraka bila uadilifu ni kazi bure.
  Anasema JK atakwenda kusababisha umwagaji damu kwa kutumia udini.
  Anasema kabla ya cuf kufunga ndoa na ccm makada wa ccm walikua wanatangaza cuf ni chama cha dini flani.


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #91
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,996
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Lema:
  hakuna chama kinachopigania maslahi ya watanzania kama chadema. Wabunge na viongozi wake hawapunziki, wanapigania haki na usawa wa mtanzania
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #92
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,996
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Mkuu Daudi mchambuzi uko kwa wapi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #93
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,382
  Likes Received: 763
  Trophy Points: 280


  Ni Arusha mjini, chini kidogo ya Mount Meru Curio Market. Kama unapafahamu Fire basi utakuwa umefika.
   
 15. m

  mnyinda JF-Expert Member

  #94
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunamshukuru mungu kwa kila jambo inamaana kamatukishindwa tumwache mungu?mbona unaniboa?
   
 16. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #95
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkutano unatia matumaini! wana Daraja II msituangushe! tuko pamoja nanyi.
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #96
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,996
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  mkuu wali wa kushiba unauona kwenye sahani. Subiri mapicha mkuu
   
 18. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #97
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 34,055
  Likes Received: 41,756
  Trophy Points: 280
  Lema Anasema hakuna chama kinapigania maslahi kama chadema.
  Anasema chadema kinapigania haki ya watu wote na sio kanisa wa
  Lema anazidi kulonga kuwa ubunge sio pepo bali ni kazi ya uadilifu kwa iyo akija mtu amenizidi uadilifu nipigeni chini na mumchague.
  Anasema tumepewa mkuu wa wilaya mwenye kiherehere.

  Lema anazidi kusema kuwa wamachinga wa arusha wanazidi kuteseka, anasema tusifikiri wamachinga ni takataka.
  Anasema siku wamachinga wakiondoka barabarani na wasionekane kabisa basi usiku tutaokota wananchi waliochomwa visu na watu wanaojitafutia rizki kwa njia mbadala.
  Anawapongeza kwa kufanya kazi ya mungu kwa kujigawia kiwanja cha kilombero.
  Anasema sheria inayo kandamiza maskini na kutukuza matajiri ni sheria ya kupinga.
  Nisipofa leo nitakufa nitakufa kesho ila siko tayari kufa kwa malaria ila niko tayariu kufa kupambania haki ya nmsingi.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #98
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,008
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ritz!

  Pole sana! Tangu awali nimeshakuambia ya kwmb utumwa wako hakika utakujajutia na hata best zako wakiongozwa na zomba nakuomba ukae nao na waelimishe taratibu na bila shaka mwaweza elewesha watumwa wenzie!

  Laaalabuk!

   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #99
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,246
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  "Tantararira"
   
 21. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #100
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 34,055
  Likes Received: 41,756
  Trophy Points: 280
  Mkuu nipo kwenye hili shamba upande wa kulia kwenye hizi nguzo mbili upande wa kulia wa jukwaa la wahewshimiwa.


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...