Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mungi, Oct 6, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Kwanza kabisa niwapongeze mods kwa busara zao za kipekee, maana kama siyo wao leo hii ningekuwa naendelea kuugulia ban.

  Muda huu nipo kwenye eneo la mkutano wa uzinduzi wa kampeni katika uwanja wa Ndarvoi uliopo katika kata ya Daraja mbili.

  Watu wanaendelea kuingia kwenye eneo la mkutano, tutaendelea kuwajuza kwa kila kitakachokuwa kinaendelea.

  Jf daima!

  Yupo pia Pepe mwimbaji machachari wa nyimbo peoples power, amekuja na cd za matukio ya M4C, zinaonyesha mpaka tukio la mauaji ya Daudi Mwangosi aleliyeuawa na polisi pamoja Ally Zona aliyeuawa morogoro

  UPDATE:
  Tayari makamanda Lema, Milya, na Nanyaro wameshaingia uwanjani.
  Uwanja umefurika. Picha mtazipata.
  Mkutano unafunguliwa kwa dua.

  JAMES MILYA:
  Ndugu zangu ni mara yangu ya kwanza kumnadi mgombea wa chama changu kipya kumnadi mgombea wa chama chetu tokea nilipovua gamba.
  Tumedhamiria kubadilisha hali ya kisiasa nchini kwa vitendo, tuhakikishe tunamchagua diwani wa cdm.
  Inasikitisha Mnally aliyewachapa viboko waalimu akafukuzwa, leo ccm wanamchagua kuwa kiongozi.
  Ndugu zangu tunamleta kamanda msofe (mgombea), mchagueni akawashughulikie panya kwenye halmashauri yetu.
  Mtupatie jembe hili litusaidie kwenye harakati za kuleta maendeleo.
  Nimekuwa ccm, wana agenda tatu tu.
  Agenda ya kwanza, kufungua kikao, ya pili muhtasari wa kikao kilichopita, ya tatu, kujadili hali ya kisiasa nchini. Hawajadili kero za wananchi.
  Taarifa za ccm:
  ndugu zangu watu hawa ilikuwaonyesha kuwa wamepata nguvu ndani ya arusha, wamedhamiria kutembea kila kaya, wako tayari hata kugawa laki kwa kila mtu. Hivyo pokeeni hizo hela ni za kwetu, kura tumchague kamanda msofe.

  NANYARO:
  ndugu zangu, leo hii tupo mbele yenu, na daraja mbili ni zaidi ya jimbo, na nimfikishie salamu mgombea wa ccm bw. Mushi, kuwa chadema tuna diwani wa daraja mbili, ccm wana mgombea wa daraja mbili.
  Chadema tunasema kuna manunuzi ambayo tunaweza kufanya nje ya vikao kwa maendeleo ya wananchi.
  Tuna mambo ya msingi ya kutaka kuokoa maisha ya wananchi.
  Kuwaondoa wamachinga mjini ni bomu ambalo litalipuka si muda mrefu.
  Kamanda Nassari amekamua vya kutosha.

  LEMA:
  wali wakushiba unauona kwenye sahani, hapa biashara imekwisha.
  Milya anaendelea kutupa taarifa kuwa vijana wake aliowaacha ccm wanampa taarifa kuwa ccm wameaanda zaidi ya mil 500, wapo tayari kutoa laki kwa kila mtu ili washinde hii kata.
  Tumeanzisha M4C, tumegawana kwa kanda, mimi nimepangiwa kanda ya kaskazini. Umaskini siyo uadilifu, tunapiga vita umaskini usiku na mchana. Leo umaskini unaendelea kuwakandamiza watanzania, tutapiga umaskini vita hata kwa figo zetu.
  Ndugu zangu hatuwezi kuichagua ccm, maisha ni ngumu hali ni mbaya.
  Kazi ya chadema ni kupiga vita ujinga, na kuwaelimisha watanzania.
  Msofe tunakutuma kwenye halmashauri, kazi yako ni moja, pigania wanyonge, wewe ni baunsa, katumie ubaunsa wako kuwashughulikia panya wa halmashauri.
  Lengo la chadema siyo kushinda, lengo la chadema ni kushinda na kulinda haki na uadilifu, tuwapate watu watiifu wakuwaongoza watu. Ukileta zakuleta tunakumwaga chini.
  Kitu ambacho kikwete atasababisha katika nchi hii ni kumwaga damu za watanzania kwa misingi ya udini.

  Picha:

  DSC03720.JPG
  Kamanda Lema akimtambulisha mgombea udiwani wa kata ya Daraja II Bw. Msofe


  DSC03706.JPG Kamanda Lema akitoa usia
  DSC03705.JPG Mbunge aliyeko Honeymoon akikamua jukwaani
  DSC03702.JPG Umati wa wananchi waliohudhuria Mkutano wa uzinduzi wa kampeni Daraja Mbili
  DSC03704.JPG
  Dongo Janja na Lema hawakufahamiana barabarani.

  [​IMG]
  Kada maarufu wa CCM Mzee Zacharia akikabidhiwa kadi ya chadema, tukio likishuhudiwa na Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Arusha Kamanda Nanyaro (kushoto), Mbunge Lema na Msofe wa pili kulia
  DSC03695.JPG Kamanda Ephata Nanyaro akikamua jukwaani
  DSC03684.JPG
  Umati ukishuhudia uzinduzi wa kampeni
  Umati 3.JPG Wali wa kushiba unauona kwenye sahani
  Pepe na shabiki machachari wa chadema.JPG
   

  Attached Files:

 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #61
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,483
  Likes Received: 14,132
  Trophy Points: 280
  Ooooffffff:..........point...........

   
 3. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #62
  Oct 6, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Nakala: Mikael P Aweda, Mzee Mwanakijiji, Mwita Maranya, Matola, nk
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #63
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 565
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  sasa ww chama suala la ZITO hapa limeingiaje? Hebu tujadili uzinduzi wa kampeni, unaweweseka na nn? B a gentle man o woman
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #64
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,009
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ritz at work!

  Pole sana na utumwa unakunyanyapaa!Ungana na lile genge lako na mkachukue chenu kwa mafisadi na acha kutapika kama hujui dhamani ya utu wako kibinadamu!

  Pole mtumwa asiyejijua!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #65
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 33,287
  Likes Received: 40,356
  Trophy Points: 280
  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 7. c

  chama JF-Expert Member

  #66
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,005
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ritz
  umewaona makamanda?

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 8. c

  chama JF-Expert Member

  #67
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,005
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  ahaaa haaa kuishabikia Chadema uniahitaji kuwa na busara za mfu

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 9. MARUMARU

  MARUMARU JF-Expert Member

  #68
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  wewe umezidi sasa mambo ya Zitto na mkutano wa daraja 2 kuna uhusiano ngani? Au ndio mmetumwa kumpa promo kwa kila khali
   
 10. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #69
  Oct 6, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Sasa kama kuishabikia CDM unahitaji kuwa na busara za mfu, Je yule anaeipinga si anatakiwa kuwa na busara za mfu pia!!


  TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
  tumbiri@jamiiforums.com
   
 11. c

  chama JF-Expert Member

  #70
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,005
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Lakini si umesoma na kuelemika kidogo tatizo lipo wapi? Hata kwenye mahubiri ya jumapili wachungaji hutia habari za mitaani kuongeza chachandu kwenye mafundisho

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 12. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #71
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 755
  Trophy Points: 280
  Mangwea enzi hizo alisifia sana CCM na kudai baba ndie aliejenga makao makuu. Akajidai kuwa yeye ni damu ya kijani, Katika nyimbo yake ya "Si ndio CCM".
  Alivaa sana Kijani Na Njano.

  Lakini Leo hii miaka michache tu imepita kauona ukweli, sio CCM wala Makao Makuu, na damu yake ni nyekundu wala si kijani, kaamua kutoa kibao cha "Masikini Wenzangu". Ndani kahoji Maisha bora yako wapi??? (Mwanzoni alidai anayo yeye).


  Now to The Point: Leo Unafanyika ufunguzi wa kampeni za udiwani kata ya Daraja II, home to Joh Makini, Nikki, Bonta etc yaani "River Camp".

  Ni wasanii wazuri wanao-hit kila mara, na wasomi sana tu kama Nikki na Bonta. Lakini sijawahi waona wakija kuhamasisha wananchi japo tu wajitokeze kupiga kura (haijalishi watachagua chama gani), sijawahi wasikia hata mara moja wakiweka misimamo yao ya kiitikadi hadharani.

  River Camp na wengine wa Ara mko wapi?? Wateja wa miziki yenu ni hawa hawa wananchi wa Ara. Jitokezeni muwaambie ukweli, muwashauri.
  Duniani Kote wasanii ndio kioo cha jamii.

  Bob Marley aliikomboa mioyo mingi kwa mashairi yake.
  USA Wasanii wengi na Wachezaji ndio wanaohimiza watu kupiga kura (bila kuangalia itikadi) lakini ingefaa zaidi kuchagua Obama.
  Kenya kina Eric Wainana mpaka walihamishwa nchi.

  Acheni ushamba njooni muikomboe Arusha, njooni tujibebe na sisi, tufungue na Studios, tuwekeze watu waje wanunue na kazi zenu.
  Palipo na ukombozi pana opportunities, njooni achaneni na Ruge, ona alichowafanya kina Ngwea.


  Much Respect to Shah Bang na Tarakimu.
   
 13. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #72
  Oct 6, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Inasikitisha sana. Mashabiki wa Zitto humu JF ni Pro-CCM (Anti - CDM). Wenyewe wanadhani wanamsaidia kumbe wanazidi kumwaribia. Wanamsapoti Zitto wakati huo huo wanaponda Chama chake. Na hata siku moja hawajawai kumwalika ajiuenda na Chama chao kama kweli wanamtakia mema na ni Potential kwa Chama chao!
   
 14. S

  Soki JF-Expert Member

  #73
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,307
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Una uhakika na unachosema? Tafadhali thibitisha
   
 15. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #74
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hivi nimepotea njia au?

  Nisaidieni wakuu, hapa tunafuatilia na kujadili mkutano wa daraja mbili au Zitto Kabwe?
   
 16. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #75
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,225
  Likes Received: 2,632
  Trophy Points: 280
  Dogo janja ndani ya nyumba! Anahamasisha vijana wa daraja mbili wahakikishe ccm hawanunui shahada.
   
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #76
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ndiyo Agenda kuu ya wafuasi wa Magamba wakidhani kazi yao inafanywa vyema na mtu wao
   
 18. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #77
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 33,287
  Likes Received: 40,356
  Trophy Points: 280
  Dogo janja jukwaani: anasema kuna viongozi wa ccm wanashauri chadema mgombea wa kumsimamisha, nassari ana hoji tangu lini adui akakuelekeza mbinu za vita.
  Anasema jk anacheza na farasi canada wakati kina mama wajawazito wanajifungulia sakafuni.


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #78
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Read btn the lines....
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #79
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,250
  Likes Received: 4,689
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 21. m

  mnyinda JF-Expert Member

  #80
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii forum.. Kama unataka news reporting tafuta gazeti.. Ijumaa litakufaa zaidi..
   
Loading...