Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mungi, Oct 6, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Kwanza kabisa niwapongeze mods kwa busara zao za kipekee, maana kama siyo wao leo hii ningekuwa naendelea kuugulia ban.

  Muda huu nipo kwenye eneo la mkutano wa uzinduzi wa kampeni katika uwanja wa Ndarvoi uliopo katika kata ya Daraja mbili.

  Watu wanaendelea kuingia kwenye eneo la mkutano, tutaendelea kuwajuza kwa kila kitakachokuwa kinaendelea.

  Jf daima!

  Yupo pia Pepe mwimbaji machachari wa nyimbo peoples power, amekuja na cd za matukio ya M4C, zinaonyesha mpaka tukio la mauaji ya Daudi Mwangosi aleliyeuawa na polisi pamoja Ally Zona aliyeuawa morogoro

  UPDATE:
  Tayari makamanda Lema, Milya, na Nanyaro wameshaingia uwanjani.
  Uwanja umefurika. Picha mtazipata.
  Mkutano unafunguliwa kwa dua.

  JAMES MILYA:
  Ndugu zangu ni mara yangu ya kwanza kumnadi mgombea wa chama changu kipya kumnadi mgombea wa chama chetu tokea nilipovua gamba.
  Tumedhamiria kubadilisha hali ya kisiasa nchini kwa vitendo, tuhakikishe tunamchagua diwani wa cdm.
  Inasikitisha Mnally aliyewachapa viboko waalimu akafukuzwa, leo ccm wanamchagua kuwa kiongozi.
  Ndugu zangu tunamleta kamanda msofe (mgombea), mchagueni akawashughulikie panya kwenye halmashauri yetu.
  Mtupatie jembe hili litusaidie kwenye harakati za kuleta maendeleo.
  Nimekuwa ccm, wana agenda tatu tu.
  Agenda ya kwanza, kufungua kikao, ya pili muhtasari wa kikao kilichopita, ya tatu, kujadili hali ya kisiasa nchini. Hawajadili kero za wananchi.
  Taarifa za ccm:
  ndugu zangu watu hawa ilikuwaonyesha kuwa wamepata nguvu ndani ya arusha, wamedhamiria kutembea kila kaya, wako tayari hata kugawa laki kwa kila mtu. Hivyo pokeeni hizo hela ni za kwetu, kura tumchague kamanda msofe.

  NANYARO:
  ndugu zangu, leo hii tupo mbele yenu, na daraja mbili ni zaidi ya jimbo, na nimfikishie salamu mgombea wa ccm bw. Mushi, kuwa chadema tuna diwani wa daraja mbili, ccm wana mgombea wa daraja mbili.
  Chadema tunasema kuna manunuzi ambayo tunaweza kufanya nje ya vikao kwa maendeleo ya wananchi.
  Tuna mambo ya msingi ya kutaka kuokoa maisha ya wananchi.
  Kuwaondoa wamachinga mjini ni bomu ambalo litalipuka si muda mrefu.
  Kamanda Nassari amekamua vya kutosha.

  LEMA:
  wali wakushiba unauona kwenye sahani, hapa biashara imekwisha.
  Milya anaendelea kutupa taarifa kuwa vijana wake aliowaacha ccm wanampa taarifa kuwa ccm wameaanda zaidi ya mil 500, wapo tayari kutoa laki kwa kila mtu ili washinde hii kata.
  Tumeanzisha M4C, tumegawana kwa kanda, mimi nimepangiwa kanda ya kaskazini. Umaskini siyo uadilifu, tunapiga vita umaskini usiku na mchana. Leo umaskini unaendelea kuwakandamiza watanzania, tutapiga umaskini vita hata kwa figo zetu.
  Ndugu zangu hatuwezi kuichagua ccm, maisha ni ngumu hali ni mbaya.
  Kazi ya chadema ni kupiga vita ujinga, na kuwaelimisha watanzania.
  Msofe tunakutuma kwenye halmashauri, kazi yako ni moja, pigania wanyonge, wewe ni baunsa, katumie ubaunsa wako kuwashughulikia panya wa halmashauri.
  Lengo la chadema siyo kushinda, lengo la chadema ni kushinda na kulinda haki na uadilifu, tuwapate watu watiifu wakuwaongoza watu. Ukileta zakuleta tunakumwaga chini.
  Kitu ambacho kikwete atasababisha katika nchi hii ni kumwaga damu za watanzania kwa misingi ya udini.

  Picha:

  DSC03720.JPG
  Kamanda Lema akimtambulisha mgombea udiwani wa kata ya Daraja II Bw. Msofe


  DSC03706.JPG Kamanda Lema akitoa usia
  DSC03705.JPG Mbunge aliyeko Honeymoon akikamua jukwaani
  DSC03702.JPG Umati wa wananchi waliohudhuria Mkutano wa uzinduzi wa kampeni Daraja Mbili
  DSC03704.JPG
  Dongo Janja na Lema hawakufahamiana barabarani.

  [​IMG]
  Kada maarufu wa CCM Mzee Zacharia akikabidhiwa kadi ya chadema, tukio likishuhudiwa na Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Arusha Kamanda Nanyaro (kushoto), Mbunge Lema na Msofe wa pili kulia
  DSC03695.JPG Kamanda Ephata Nanyaro akikamua jukwaani
  DSC03684.JPG
  Umati ukishuhudia uzinduzi wa kampeni
  Umati 3.JPG Wali wa kushiba unauona kwenye sahani
  Pepe na shabiki machachari wa chadema.JPG
   

  Attached Files:

 2. S

  Soki JF-Expert Member

  #41
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,307
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sasa ni saa kumi kasoro, Mungi nini kinaendelea wakati huu...je makamanda wameanza kuingia uwanjani?
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #42
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,423
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  si mkeo? mimi sio mimi smile
   
 4. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #43
  Oct 6, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  "Hadha Min Fadhil Rhabi - Hizi ni Rehema za Mwenyezi Mungu"
   
 5. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #44
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu angalia biashara za watu hizo!
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #45
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,483
  Likes Received: 14,132
  Trophy Points: 280
  Tupe updates mkuu Mungi nakuaminia!
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #46
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,250
  Likes Received: 4,689
  Trophy Points: 280
  Mkuu chama,
  Makamanda kama kawaida yao wapo kazini wanatumika kisiasa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #47
  Oct 6, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Basi ni "PM" kamanda!


  TUMBIRI (PhD In Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), B.com(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Best Student in Form Six National Exams)
  tumbiri@jamiiforums.com
   
 9. r

  raymg JF-Expert Member

  #48
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Weka picha mkuu...afu daraja mbili ndio wapi huko kaka!...
   
 10. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #49
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,476
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dah! hata mimi sitaki nisikie ananiambia anaenda huko, wale mapapaa wanajua kutomasa, mtoto anaegea hovyo baada ya siku mbili majamaa wanamgonga, wanajidai kwa kuboresha huduma zao sasahivi wanamfanyia massage.
   
 11. S

  Soki JF-Expert Member

  #50
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,307
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Dah Mungi naona kimya sana Mkuu!!
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #51
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,009
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nami nipo njia moja nakuja Makamanda!!

  Pamoja na jua kuwaka kama limeshushwa vile lakini haijalishi kwani lazima tuweke kambi mahala lengwa!


   
 13. hasason

  hasason JF-Expert Member

  #52
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 1,558
  Likes Received: 794
  Trophy Points: 280
  Hii ni chitchat au news reporting couse sioni cha maana kinachoendelea zaid ya porojo za ban hebu makamanda wenye akili hapo daraja 2 tupen adds!
   
 14. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #53
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 23,517
  Likes Received: 19,740
  Trophy Points: 280
  Kamanda Mungi kama vipi tupe na matokeo ya uchaguzi leo leo
   
 15. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #54
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Naona mnataka kuchafua hali ya hewa kwa maneno ya kashfa.
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #55
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,483
  Likes Received: 14,132
  Trophy Points: 280
  Mungi niaje mkuu tupe updates
   
 17. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #56
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,666
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Mkuu Molemo, wameguswa...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #57
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 23,517
  Likes Received: 19,740
  Trophy Points: 280

  Mnaitana.......acha uoga, ina maana bila kolabo huwezi ku-hit
   
 19. m

  mnyinda JF-Expert Member

  #58
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado sijakupata haondio akinanani?mbona sijaelewa?mungi lete picha na maelezo
   
 20. M

  Molemo JF-Expert Member

  #59
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Angalia picha za mwanzo ameshaziweka juu.
   
 21. c

  chama JF-Expert Member

  #60
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,005
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ritz
  Makamanda kila siku wanadai Ritz, Chama na Zomba wanapokea posho Lumumba; cha ajabu kaulizetu zimekuwa huru kwenye kutetea maslahi ya CCM; ila wao makamanda wanaonyesha wazi kabisa wengi humu JF ni waganga njaa wanatumika kisiasa na wengine wanatumia sana JF kujitangaza ili wapewe nafasi za kugombea kupitia Chadema; wamekazania Zitto hafai ukiwauliza majibu hawana wamebaki kusema Zitto ni mbinafsi lakini hawabainishi ubinafsi wake upo wapi; kwenye mjadala huu sidhani kama utamuona Aweda,Mwanakijiji, Mwita Maranya na Matola wanawatumia makamanda uchwara waganga njaa kwasababu wanaujua ukweli umesimama wapi.

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
Loading...