Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mungi, Oct 6, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Kwanza kabisa niwapongeze mods kwa busara zao za kipekee, maana kama siyo wao leo hii ningekuwa naendelea kuugulia ban.

  Muda huu nipo kwenye eneo la mkutano wa uzinduzi wa kampeni katika uwanja wa Ndarvoi uliopo katika kata ya Daraja mbili.

  Watu wanaendelea kuingia kwenye eneo la mkutano, tutaendelea kuwajuza kwa kila kitakachokuwa kinaendelea.

  Jf daima!

  Yupo pia Pepe mwimbaji machachari wa nyimbo peoples power, amekuja na cd za matukio ya M4C, zinaonyesha mpaka tukio la mauaji ya Daudi Mwangosi aleliyeuawa na polisi pamoja Ally Zona aliyeuawa morogoro

  UPDATE:
  Tayari makamanda Lema, Milya, na Nanyaro wameshaingia uwanjani.
  Uwanja umefurika. Picha mtazipata.
  Mkutano unafunguliwa kwa dua.

  JAMES MILYA:
  Ndugu zangu ni mara yangu ya kwanza kumnadi mgombea wa chama changu kipya kumnadi mgombea wa chama chetu tokea nilipovua gamba.
  Tumedhamiria kubadilisha hali ya kisiasa nchini kwa vitendo, tuhakikishe tunamchagua diwani wa cdm.
  Inasikitisha Mnally aliyewachapa viboko waalimu akafukuzwa, leo ccm wanamchagua kuwa kiongozi.
  Ndugu zangu tunamleta kamanda msofe (mgombea), mchagueni akawashughulikie panya kwenye halmashauri yetu.
  Mtupatie jembe hili litusaidie kwenye harakati za kuleta maendeleo.
  Nimekuwa ccm, wana agenda tatu tu.
  Agenda ya kwanza, kufungua kikao, ya pili muhtasari wa kikao kilichopita, ya tatu, kujadili hali ya kisiasa nchini. Hawajadili kero za wananchi.
  Taarifa za ccm:
  ndugu zangu watu hawa ilikuwaonyesha kuwa wamepata nguvu ndani ya arusha, wamedhamiria kutembea kila kaya, wako tayari hata kugawa laki kwa kila mtu. Hivyo pokeeni hizo hela ni za kwetu, kura tumchague kamanda msofe.

  NANYARO:
  ndugu zangu, leo hii tupo mbele yenu, na daraja mbili ni zaidi ya jimbo, na nimfikishie salamu mgombea wa ccm bw. Mushi, kuwa chadema tuna diwani wa daraja mbili, ccm wana mgombea wa daraja mbili.
  Chadema tunasema kuna manunuzi ambayo tunaweza kufanya nje ya vikao kwa maendeleo ya wananchi.
  Tuna mambo ya msingi ya kutaka kuokoa maisha ya wananchi.
  Kuwaondoa wamachinga mjini ni bomu ambalo litalipuka si muda mrefu.
  Kamanda Nassari amekamua vya kutosha.

  LEMA:
  wali wakushiba unauona kwenye sahani, hapa biashara imekwisha.
  Milya anaendelea kutupa taarifa kuwa vijana wake aliowaacha ccm wanampa taarifa kuwa ccm wameaanda zaidi ya mil 500, wapo tayari kutoa laki kwa kila mtu ili washinde hii kata.
  Tumeanzisha M4C, tumegawana kwa kanda, mimi nimepangiwa kanda ya kaskazini. Umaskini siyo uadilifu, tunapiga vita umaskini usiku na mchana. Leo umaskini unaendelea kuwakandamiza watanzania, tutapiga umaskini vita hata kwa figo zetu.
  Ndugu zangu hatuwezi kuichagua ccm, maisha ni ngumu hali ni mbaya.
  Kazi ya chadema ni kupiga vita ujinga, na kuwaelimisha watanzania.
  Msofe tunakutuma kwenye halmashauri, kazi yako ni moja, pigania wanyonge, wewe ni baunsa, katumie ubaunsa wako kuwashughulikia panya wa halmashauri.
  Lengo la chadema siyo kushinda, lengo la chadema ni kushinda na kulinda haki na uadilifu, tuwapate watu watiifu wakuwaongoza watu. Ukileta zakuleta tunakumwaga chini.
  Kitu ambacho kikwete atasababisha katika nchi hii ni kumwaga damu za watanzania kwa misingi ya udini.

  Picha:

  DSC03720.JPG
  Kamanda Lema akimtambulisha mgombea udiwani wa kata ya Daraja II Bw. Msofe


  DSC03706.JPG Kamanda Lema akitoa usia
  DSC03705.JPG Mbunge aliyeko Honeymoon akikamua jukwaani
  DSC03702.JPG Umati wa wananchi waliohudhuria Mkutano wa uzinduzi wa kampeni Daraja Mbili
  DSC03704.JPG
  Dongo Janja na Lema hawakufahamiana barabarani.

  [​IMG]
  Kada maarufu wa CCM Mzee Zacharia akikabidhiwa kadi ya chadema, tukio likishuhudiwa na Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Arusha Kamanda Nanyaro (kushoto), Mbunge Lema na Msofe wa pili kulia
  DSC03695.JPG Kamanda Ephata Nanyaro akikamua jukwaani
  DSC03684.JPG
  Umati ukishuhudia uzinduzi wa kampeni
  Umati 3.JPG Wali wa kushiba unauona kwenye sahani
  Pepe na shabiki machachari wa chadema.JPG
   

  Attached Files:

 2. D

  Darick JF-Expert Member

  #21
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante kaka kwa kutumia muda wako kutujuza kinachoendelea hapo Ndarvoi, tunaendelea kukufuatilia.
  BIG UP!!
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #22
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,423
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  aaah aya bwana mi ngoja nikaoshwe miguu nitarudi baadae...best wishes
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #23
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 33,252
  Likes Received: 40,277
  Trophy Points: 280
  Niko hapa tanzanite wazee club napata nyama choma nakuja sasa hivi hapo relini kujoin na mzee mungi.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 5. D

  Darick JF-Expert Member

  #24
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante kaka kwa kutumia muda wako kutujuza kinachoendelea hapo Ndarvoi, tunaendelea kukufuatilia.
  BIG UP!!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #25
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,310
  Likes Received: 2,205
  Trophy Points: 280
  Mungi usinichekeshe hiyo ilishanipeleka ban zaidi ya Mara tano. Ila Jana wakati natoka mtwara ambako CDM ipo juu sana kuliko Arusha nikashangaa kuona status yako inasomeka banned
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #26
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Mkuu kazi yangu ni mmoja tu, kuripotia matukio, kila atakayeingia hapa nitawaripotia
   
 8. S

  Soki JF-Expert Member

  #27
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,307
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Namwona Ritz yuko hapa anauchungulia huu uzi kwa makini kwelikweli!!
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #28
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Tunakushukuru sana Kamanda,tupo pamoja sana.Jitahidi na picha mbili tatu hivi itapendeza zaidi.
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #29
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,250
  Likes Received: 4,690
  Trophy Points: 280
  Mungi, katika watu ambao nawaheshimu JF na wewe humo angalia usijivunjie heshima yako JF, kauli zako za kejeli dhidi ya imani nyingine ni kuleta chuki Jamvini, wewe unaweza kuona kawaida kutoa kejeli kuwaita wavaa pekos, lakini hujue watu wanakusoma na unajijengea chuki za bure.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #30
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Tunakushukuru sana mkuu!
   
 12. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #31
  Oct 6, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mungi,
  Sijakusoma vizuri. Emu funguka.


  TUMBIRI (PhD, University of HULL - United Kingdom),
  tumbiri@jamiiforums.com
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #32
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Mkuu wangu mi na wewe ndo tunaongoza kupigwa ban kwa ajili ya wale jamaa zetu.
   
 14. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #33
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mkuu usisahau kutuunganisha wote katika uwanja huo kwa njia ya picha za tukio zima.
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #34
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Mkuu nipo kwenye mkutano, usije ukasababisha nikarudishwa mahabusu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #35
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,177
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  hizo ndizo mada unazo weza kujadili zaidi yaani maada ikiwa na kaudini fulani hukosekani..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #36
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  picha utazipata
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #37
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  picha mtazipata
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #38
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kwani kamtaja nani kwa imani yake?
  Kuna watu wenye imani ya kuvaa Pekos? Acha kuweweseka bana!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #39
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,177
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  mke wangu nilishampiga marufuku huo ujinga..
   
 21. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #40
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,310
  Likes Received: 2,205
  Trophy Points: 280
  Mkuu TUMBIRI hiyo signature inamaanisha nini? Kabla hujapewa majibu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...