Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kata ya Daraja Mbili - Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mungi, Oct 6, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Kwanza kabisa niwapongeze mods kwa busara zao za kipekee, maana kama siyo wao leo hii ningekuwa naendelea kuugulia ban.

  Muda huu nipo kwenye eneo la mkutano wa uzinduzi wa kampeni katika uwanja wa Ndarvoi uliopo katika kata ya Daraja mbili.

  Watu wanaendelea kuingia kwenye eneo la mkutano, tutaendelea kuwajuza kwa kila kitakachokuwa kinaendelea.

  Jf daima!

  Yupo pia Pepe mwimbaji machachari wa nyimbo peoples power, amekuja na cd za matukio ya M4C, zinaonyesha mpaka tukio la mauaji ya Daudi Mwangosi aleliyeuawa na polisi pamoja Ally Zona aliyeuawa morogoro

  UPDATE:
  Tayari makamanda Lema, Milya, na Nanyaro wameshaingia uwanjani.
  Uwanja umefurika. Picha mtazipata.
  Mkutano unafunguliwa kwa dua.

  JAMES MILYA:
  Ndugu zangu ni mara yangu ya kwanza kumnadi mgombea wa chama changu kipya kumnadi mgombea wa chama chetu tokea nilipovua gamba.
  Tumedhamiria kubadilisha hali ya kisiasa nchini kwa vitendo, tuhakikishe tunamchagua diwani wa cdm.
  Inasikitisha Mnally aliyewachapa viboko waalimu akafukuzwa, leo ccm wanamchagua kuwa kiongozi.
  Ndugu zangu tunamleta kamanda msofe (mgombea), mchagueni akawashughulikie panya kwenye halmashauri yetu.
  Mtupatie jembe hili litusaidie kwenye harakati za kuleta maendeleo.
  Nimekuwa ccm, wana agenda tatu tu.
  Agenda ya kwanza, kufungua kikao, ya pili muhtasari wa kikao kilichopita, ya tatu, kujadili hali ya kisiasa nchini. Hawajadili kero za wananchi.
  Taarifa za ccm:
  ndugu zangu watu hawa ilikuwaonyesha kuwa wamepata nguvu ndani ya arusha, wamedhamiria kutembea kila kaya, wako tayari hata kugawa laki kwa kila mtu. Hivyo pokeeni hizo hela ni za kwetu, kura tumchague kamanda msofe.

  NANYARO:
  ndugu zangu, leo hii tupo mbele yenu, na daraja mbili ni zaidi ya jimbo, na nimfikishie salamu mgombea wa ccm bw. Mushi, kuwa chadema tuna diwani wa daraja mbili, ccm wana mgombea wa daraja mbili.
  Chadema tunasema kuna manunuzi ambayo tunaweza kufanya nje ya vikao kwa maendeleo ya wananchi.
  Tuna mambo ya msingi ya kutaka kuokoa maisha ya wananchi.
  Kuwaondoa wamachinga mjini ni bomu ambalo litalipuka si muda mrefu.
  Kamanda Nassari amekamua vya kutosha.

  LEMA:
  wali wakushiba unauona kwenye sahani, hapa biashara imekwisha.
  Milya anaendelea kutupa taarifa kuwa vijana wake aliowaacha ccm wanampa taarifa kuwa ccm wameaanda zaidi ya mil 500, wapo tayari kutoa laki kwa kila mtu ili washinde hii kata.
  Tumeanzisha M4C, tumegawana kwa kanda, mimi nimepangiwa kanda ya kaskazini. Umaskini siyo uadilifu, tunapiga vita umaskini usiku na mchana. Leo umaskini unaendelea kuwakandamiza watanzania, tutapiga umaskini vita hata kwa figo zetu.
  Ndugu zangu hatuwezi kuichagua ccm, maisha ni ngumu hali ni mbaya.
  Kazi ya chadema ni kupiga vita ujinga, na kuwaelimisha watanzania.
  Msofe tunakutuma kwenye halmashauri, kazi yako ni moja, pigania wanyonge, wewe ni baunsa, katumie ubaunsa wako kuwashughulikia panya wa halmashauri.
  Lengo la chadema siyo kushinda, lengo la chadema ni kushinda na kulinda haki na uadilifu, tuwapate watu watiifu wakuwaongoza watu. Ukileta zakuleta tunakumwaga chini.
  Kitu ambacho kikwete atasababisha katika nchi hii ni kumwaga damu za watanzania kwa misingi ya udini.

  Picha:

  DSC03720.JPG
  Kamanda Lema akimtambulisha mgombea udiwani wa kata ya Daraja II Bw. Msofe


  DSC03706.JPG Kamanda Lema akitoa usia
  DSC03705.JPG Mbunge aliyeko Honeymoon akikamua jukwaani
  DSC03702.JPG Umati wa wananchi waliohudhuria Mkutano wa uzinduzi wa kampeni Daraja Mbili
  DSC03704.JPG
  Dongo Janja na Lema hawakufahamiana barabarani.

  [​IMG]
  Kada maarufu wa CCM Mzee Zacharia akikabidhiwa kadi ya chadema, tukio likishuhudiwa na Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Arusha Kamanda Nanyaro (kushoto), Mbunge Lema na Msofe wa pili kulia
  DSC03695.JPG Kamanda Ephata Nanyaro akikamua jukwaani
  DSC03684.JPG
  Umati ukishuhudia uzinduzi wa kampeni
  Umati 3.JPG Wali wa kushiba unauona kwenye sahani
  Pepe na shabiki machachari wa chadema.JPG
   

  Attached Files:

 2. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 14,714
  Likes Received: 18,349
  Trophy Points: 280
  pamoja sana kamamnda...big up sana kwa mods japo nikisikia neno BAN hata mitaani tu damu huwa inasisimka...
   
 3. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,666
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mungi welcome to the world... Kulikoni ulifanya nini?

  Endelea kutujuza what is going on hapo maana wewe ni mzee wa live za kiukweli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Kweli kamanda, kuna baadhi ya members wanakera sana wanatusababishia ban.
  Eneo la mkutano ni padogo, na hili liwe jambo la kulipigania kuhakikisha kunakuwa na maeneo ya wazi.

  Tujitahidi kuwa tunachagua viongozi wenye nia na dhamira njema na wananchi wa nchi hii.
  Ni aibu mtu mmoja tu anamiliki zaidi ya ekari 15 halafu watu hawana maeneo, serikali haina eneo la wazi kufanyia mkusanyiko
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,423
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  sijui mimi niwarushie live kuhusu nanilii
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu nakuambia usithubutu kuwagusa wale ndg zetu wanaovaa pekos, utakiona cha moto
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Hahaaaa Smile hebu rusha live hiyo nanilii
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,104
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 0
  Kwani kuna tukio gani linaendelea huko kwako; au ndio unajitahidi kuongeza matundu ili uwe kama nyavu nini?
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,423
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  ndo wapi huko mkuu unaturushia?
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,423
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  aaah tujadili mada bana..uhuhuuuuuu
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Daraja mbili mkuu
   
 12. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,666
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Hahahahaaa...Yaani na hao ndio watakuja kuniletea matatizo humu jamvini maana issue zao zinavyoniboaga huwa siwezi kuvumilia kabisa niapoona viroja vyao...Pole sana Mkuu. Tuendelee na ya daraja II
   
 13. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,386
  Likes Received: 1,469
  Trophy Points: 280
  Mbona kama hamko tayari kutujuza
   
 14. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,526
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tumegee kila kinachojiri bila kusahau picha
   
 15. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,423
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  mkoa gani mkuu?
   
 16. m

  mnyinda JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee wa mahakamani endelea kutujuza tunakuaminia mungi,vipi atakuwepo nani na nani?auni slaa pekeyake,
   
 17. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 32,057
  Likes Received: 11,514
  Trophy Points: 280
  Picha ni muhimu sana Mungi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 32,057
  Likes Received: 11,514
  Trophy Points: 280
  Picha ni muhimu sana Mungi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Hahaaaa Smile. Ni Arusha
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,998
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  wakuu kwa picha msitie shaka. Mzee Mwanakijiji alinifundisha kuwa picture always speakes louder than words
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...