Uzinduzi wa kadi za Chama cha Mapinduzi za kieletroniki mkoa wa Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,891
939
Uzindizi wa kadi za Chama cha Mapinduzi za kieletroniki mkoa wa Dodoma​

15 Oct 2021

Katibu Wa NEC Organaizesheni na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt. Maudline Cyrus Castico amezindua Rasmi Kadi za Kieletroniki za Chama Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma white House

Dkt. Maudline Castico amekuwa Mgeni Rasmi wa Uzinduzi wa Kadi za Kieletroniki zaidi ya** Elfu arobaini na sita mia saba thelathini na mbili (46,732) za CCM Mkoa wa Dodoma na wilaya zake 7

Katibu wa Nec Organaizesheni Dkt. Castico amesema Lengo la zoezi hili ni Kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kupata Takwimu sahihi za Wanachama wake Kwa ngazi zote

“ Hadi sasa wanachama waliojisajili kwa Mfumo wa Kieletroniki ni zaidi ya M .1,854,681 ambapo Mkoa wa dodoma waliojisajili ni zaidi ya 127,068 ikiwa una wanachama zaidi ya 616891 ” Dkt. Maudline Castico

Mwisho Dkt. Castico amewashukuru sana wanachama wote wakiongozwa na Makatibu wa Mikoa kwa kuendelea kuonyesha juhudi za kusajili wanachama katika mfumo mpya wa kieletroniki kwa kufanya hivi ni kukiunga Mkono Chama Cha Mapinduzi na kuhamasisha zoezi hili kwa Mikoa mingine kukamilisha kwa wakati

Aidha amemaliza kwa kupongeza Mkoa wa Dodoma kwa kuwa Mfamo mzuri wa mikoa mingine katika zoezi la Kusajili kieletroniki na mikoa mingine iige hatua hii nzuri na kufanya vizuri zaidi ya Mkoa wa Dodoma

#kaziiendelee

Imetolewa na:

IDARA YA ORGANAIZESHENI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

IMG-20211015-WA0071.jpg

IMG-20211015-WA0070.jpg

IMG-20211015-WA0072.jpg

IMG-20211015-WA0074.jpg
 
Back
Top Bottom