Uzinduzi wa Jengo la Maalim Seif: Alberto na Jabir - Kalamu Zinazosema na Kuandika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
Hata kama hawakuweka majina yao sentensi zao zitakujulisha waandishi hawa. Kulia ni Jabir Ali na kushoto ni Ali "Alberto" Saleh. Hakuna asiyewajua watu hawa. Makala zao wasomaji hawazipiti lazima watazisoma.

Waandishi hawa makala zao zinauza na kujenga gazeti na mwisho wa siku gazeti linapata heshima kuwa ni gazeti lenye kuelimisha umma. Zaidi zinaweka hoja stahiki inayoongoza na msimamo wa jamii.

Lakini uandishi wa namna hii una bei yake. Mwandishi lazima awe tayari kulipa. Leo nilikuwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Jengo la Maalim Seif Makao Makuu ya ACT Wazalendo ndipo nikapata fursa ya kuviona vichwa hivi viwili vikiwa pamoja.

Moyo ukaanza kuongeza kasi. Uwanja una pilika nyingi. Nimeingiwa na hofu kichelewa hawa watu wataagana na picha nitaikosa. Kwangu mimi jua litakuwa limezama na Maghrib imeingia. Kiza tayari. Mpiga picha yeyote hili atakuambia.

Kuna picha huwezi kupiga hata kama utawinda kwa miaka 100. Hii picha ya hawa nguli wawili ni mojawapo. Wapi utampata Alberto na Jabir wako pamoja kama hivi na ukawapiga picha? Na si picha tu. Picha wameuramba. Wamependeza.

Hawa kwa sasa nchini petu ndiyo walimu wa vijana waandishi wanaonyanyukia katika uandishi unaohangaisha akili ya msomaji. Kila neno kwenye karatasi limepimwa kupata uzito wake.

Wahariri wanawajua watu hawa. Wakipokea makala zao naamini hujiambia wakasema, "Kumekucha." Wahariri wanajua katika uzoefu wao na watu hawa kuwa kalamu zao zinakata kama upanga wa Sayyidna Ali.

Si kalamu za kuchezea.
Utajikata vidole.

1667162044680.png
 
namkumbuka Ally Salehe Albeto uchaguzi mkuu wa vyama vingi 1995. ccm wabaya sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom