Uzinduzi wa daraja la Kigamboni na kisa cha dharau za wanafunzi wa Afrika Kusini

Malaika Mkuu

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
902
909
Jaana baada ya Jpm kuzindua daraja hili mimi na rafiki zangu tulipanga kwenda usiku saaana ili tukalishangae kwa uhuru.

Yapata saa sita usiku tukaanza safari mimi nikiongoza msafara huo...

Ukimya ulitawala katika safari yetu kila mtu alikuwa akiwaza lake mimi hamu yangu kubwa ilikua kuona rangi rangi ambazo huziona kwenye picha za Ulaya tuu

Hatimaye tukawasili eneo lilikua tulivu saaana hakuna magari wala wapita njia tulikuwa pekee yetu....

Nilipoanza kushuka sikuelewa sasa napita kwenye fly over kisha nikitokea chini ya daraja la treni

Nilipoanza kulifikia daraja nilikumbuka kisa cha wanafunzi wa Africa Kusini waliokuja kwenye mafunzo ya vitendo mwaka 2005 hadithi hiyo nilisimuliwa na profesa wa chuo kikuu UDSM profesa Mutahaba nikiwa chuo..

Profesa Mutahaba alitusimulia hivi...

Aliwapokea wanafunzi kutoka Africa Kusini, walikuja kutembelea kambi za wapigania uhuru wa Africa Kusini walioishi Tanzania

Wanafunzi hao waliposhuka uwanja wa ndege walianza kuukosoa kuanzia uwanja wa ndege katika safari hiyo walibeza miundo mbinu yetu na kuumuliza maswali mengi mengi yaliomuumiza kichwa profesa. Walibeza hawajaona hata barabara za juu na chini wakati Tanzania imepata uhuru kabla ya taifa lao.. Walipongia mikoani walichoka kabisa.

Mwisho wakauliza

Nyinyi tangu uhuru fedha zenu mmefanyia nini umri wa taifa lenu na miundo mbinu hii haviendani

Profesa Mutahaba aliwajibu

Fedha nyingi za taifa letu mmekula nyie na nchi za Kusini mwa Africa baada ya sisi kupata uhuru fedha zetu nyingi zilitumika kuwakomboa muwe huru kutoka kwenye makucha ya ukoloni, hii ilikuwa sadaka yetu kubwa kwa waafrika wenzetu muda si mrefu mkija tena baada ya miaka 20 hamtatukuta hivi.

Vident havikuuliza tena.....

TUMETHUBUTU TUMEWEZA TUNASONGA MBELE..

Wasalaaamu......

1461186539821.jpg
1461186571450.jpg
 
vibaka wa ccm na story zao za kusutana.pf angesema ukweli tu kwamba ccm wanatia ndani pesa zote za Umma full stop.

swissme
 
pf hakutaka hadithi ndefu na kujishusha ndio maana akaona ni vema awatie code waliposhindwa kufungua wakawa wapole ha ha ha ha
 
Back
Top Bottom