Uzinduzi wa CHADEMA Arumeru: Haijawahi kutokea - WAMERU wasema kesho watatoa UTABIRI WA NANI MSHINDI

Majivuno haya hata Igunga ilikuwa hivi hivi.Tusubiri tuone usihesabu vifaranga kabla ya kutotolewa Mkuu!!
Mambo yanazidi kubadilika mlichobakiza nyie ni kujivunia kumbukumbu.....maana hata KANU huwa wanasema hivyo hivyo mwaka 2002 tulishindaga uchaguzi.
 
- Mkutano kurushwa LIVE na STAR TV na pia kurushwa LIVE kupitia Internet CHADEMA TV (Online)
- Maandamano ya kufa mtu - Kutoka njia mbili: USA river na KIKATITI.
- HELCOPTER (CHOPPER) mwanzo mwisho
- WASHILI na WAZEE wote kuhudhuria na kumtamka rasmi mgombea wa CHADEMA Joshua Nassari kuwa ndio chaguo lao
- Hivi sasa Watu kutoka pande zote za jimbo la meru wanaanza kufika USA kwa ajili ya uzinduzi
- Wapiganaji kutoka Karatu, Longido, Moshi, dodoma, Zanzibar, DSM na maeneo mengine wameshafika na wengine kufika kesho kujiunga na kambi

Mkuu, kwa hiyo mtasomba watu kutoka kila mkoa kwenda kufanya huo uzinduzi ambao haujawahi kutokea Arumeru..

Katika huo uzinduzi wenu robo tatu watakaokuwepo ni wageni kutoka nje ya Arumeru.

Robo ndio wapiga kura wa Arumeru, mwisho wa siku matokeo yakitoka mtasema kura zimeibiwa haiwezekani mikutanoni tulikuwa na watu wengi tupate kura chache.

Jipangeni vizuri sio kupeana matumaini humu JF kura zinapigiwa Arumeru sio JF.
 
Igunga na uzini ilikuwa hivi hivi .

Kama kuna kosa wewe na wenzako mnalifanya ni kujaribu kufananisha Arumeru na Igunga& uzini na sisi hilo linakuwa faida kubwa kwa CDM (Arumeru ni tofauti mno watu wanajua kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe si sawa na igunga au Uzini) watu huku ni waelewa mi nimetoka arumeru vijijini maeneo ya ngurdoto kata ya maji ya chai nimeongea na wazee baadhi wa ccm wanahamasishana wampigie nassari kura na siyo sumari wengi wanasema wao hawaami chama ila hawamchagui mtu ameletwa

Kwa hiyo kipimo walichotumia kulinganisha meru na igunga au uzini ni kizuri mno kwa CDM

ukitaka kuthibitisha angalia star tv kesho au sunrise radio or mj radio
 
Ni yule ambae picha yake ipo kwenye chupa ya konyagi. Sijawahi ona ameshusha mikono chini toka nizaliwe.
.
 
- Mkutano kurushwa LIVE na STAR TV na pia kurushwa LIVE kupitia Internet CHADEMA TV (Online)
- Maandamano ya kufa mtu - Kutoka njia mbili: USA river na KIKATITI.
- HELCOPTER (CHOPPER) mwanzo mwisho
- WASHILI na WAZEE wote kuhudhuria na kumtamka rasmi mgombea wa CHADEMA Joshua Nassari kuwa ndio chaguo lao
- Hivi sasa Watu kutoka pande zote za jimbo la meru wanaanza kufika USA kwa ajili ya uzinduzi
- Wapiganaji kutoka Karatu, Longido, Moshi, dodoma, Zanzibar, DSM na maeneo mengine wameshafika na wengine kufika kesho kujiunga na kambi
Mfa maji
 
jamani nipo so anxious kuona ufunguzi wa kampeni kama tulivyoambiwa na star tv..lakini wameweka series zao tena..kama kuna mtu ana taarifa yoyote atujuze kama wanarusha au tukaendelee na kazi wengine..
 
Chadema mmeanza tambo zenu. Hatutaki kusikia mambo ya kuchakachuliwa mbele ya safari. Badala ya kujipanga kusimamia na kulinda kura zenu nyie mnakazana kushabikia umati wa watu.

Hapo juu,,,,,Unataka kuolewa,au unahitaji mume wa kukuoa? amua moja.
 
Mkuu, kwa hiyo mtasomba watu kutoka kila mkoa kwenda kufanya huo uzinduzi ambao haujawahi kutokea Arumeru..

Katika huo uzinduzi wenu robo tatu watakaokuwepo ni wageni kutoka nje ya Arumeru.

Robo ndio wapiga kura wa Arumeru, mwisho wa siku matokeo yakitoka mtasema kura zimeibiwa haiwezekani mikutanoni tulikuwa na watu wengi tupate kura chache.

Jipangeni vizuri sio kupeana matumaini humu JF kura zinapigiwa Arumeru sio JF.

Nahisi ulichokiandika hapo juu hakina mawasiliano na ubongo wako.
 
jamani uwanja umetapika kweli kweli. Mh Mbowe kaongea mambo ya msingi sana. Kweli wabunge wa CHADEMA vichwa
 
Back
Top Bottom