Uzinduzi rasmi M4C: Live toka Gold Crest - Mwanza (Kwa Kanda ya Ziwa)

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
384
0
Ndiyo wakuu ,heshima kwenu ! Hayawi hayawi yamekuwa , kesho kuanzia saa 2 usiku ,harakati za M4C homa na kiboko ya ccm pamoja na vibaraka wake itazinduliwa rasmi jijini mwanza kwa kanda ya ziwa katika hoteli ya Gold Crest live kupitia star television. Ni mara nyingine tena kesho umma wa watanzania utashuhudia kama kweli bado kanda ya ziwa ni ngome ya ccm au la.

Leo kutwa nzima nimekuwa na mizunguko yangu hapa city center ambapo gumuzo kubwa ni harakati za mabadiliko i .e M4C ambayo itazinduliwa kesho na uongozi wa Kitaifa.

Pia katika mizunguko hiyo nimekutana na magari kadhaa yenye alama/ nembo M4C . Baba wa taifa la India , Mahatma Gandhi alipata kusema " Be part of the change you wish to see in this world." Kwa tafsiri isiyo rasmi, alisema "Kuwa sehemu ya mabadiliko uyatakayo kwenye ulimwengu huu."

Vilevile naomba ninukuu maneno ya lango la kuingia makaburi ya waislamu pale mtaa wa Langolango-mwanza yanayosema "Swali kabla ya kuswaliwa." Tuungane kwa unyonge na umaskini ili kuitafta Tanzania tuitakayo kwa ajili yetu ,watoto wetu na vizazi vijavyo . Naomba kuwasilisha.
 

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,928
2,000
Wajipange vizuri, wajitahidi kuzuia watu wanaotaka kutumia harambee kutangaza nia ya kugombea ubunge kama ilivyokuwa kwenye harambee ya Dar. Ni muhimu pia waendeshaji wakajifunza kuzingatia taratibu na itifaki hasa linapokuja swala la MC. Siku ile Rose Mwakitwange alionekana kama picha tu mbele ya kina Godbless Lema na Joshua Nassari. Kama hawajajipanga wataishia kwenye malumbano ya kina Wenje na Henry Matata pamoja na kina Chagulani

Otherwise tunawatakia kila la heri na tupo pamoja....M4C
 

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,047
2,000
Nasikia kuna uwezekano wa Nyamagana na Ilemela kuchukuliwa na CCM 2015. Je ni kweli?
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,088
2,000
At night? what safety assurance will be given to members after they have left the scene????
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,088
2,000
Umesahau kuwa hata kule Arusha na Dar uzinduzi wa M4C ulifanyika usiku? Au una wasiwasi na wale polisi jamii waliomfanyizia Barlow unyama?

Mkuu
Katika vita adui hachagui pa kupiga, anachoangalia ni fulsa na hasa hapa kwetu bongo kuchafuana imebaki silaha pekee ya kuharibiana.

Ok, all the best.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
M4C kesho itakuwa ndani ya jiji la mwanza katika ukumbi wa Gold Crest.
kipindi kitarushwa hewani live na Star TV.
Kwenye harambee watakuwepo viongozi wa chadema taifa wakiongozwa na mwenyekiti wa chama kamanda wa anga Freeman Mbowe.
harambee itaanza kurushwa hewani kuanzia saa tatu usiku.

nawasilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom