Uzi wa vyakula tu

Cheatn month loading
IMG_20211122_221809.jpg
 
SOMA HAPA!!!!MAMBO MUHIMU KATIKA MAPISHI

nyama au samaki Ukitia viungo( vitunguu saum, tangawizi, masala) ongeza mafuta kidogo na mtindi vjk viwili inalainika na kunoga

Ukikosa vanila unaweza saga Ganda la limao bichi kuleta harufu nzuri kwenye keki au chapati maji

Ukitaka kupika mboga ya karanga, saga karanga kisha tumia maziwa kukorogea karanga badala ya maji inanoga sana
Chapat ukiógeza kdg nazi ya unga na ukakandia maziwa chapati inakuwa zaid ya nzuri

Ukitaka chips au ndiz ziwe nzuri, chemsha kdg dk 5 ipua zichuje maji then weka kwenye freezer. Ukitaka kukaanga toa pasha mafuta choma usisubiri zitoke barafu, utastaajab radha yake

Ukiona mafuta yamekuwa mengi kwenye supu au mchuzi tumia mkate wa siles kupitisha juu kufyonza

Ukitaka maharage yawe na rojo zuri,baada ya kubandika tia mafuta ya kupikia yaivie pamoja

Ukitengeneza juice ya rosela au ubuyu unaweza weka mchaichai pale unapochemsha juice inavutia sana

Chapati ikilala ukitaka kuipasha iwe lain ichove kwenye maji baridi na kuitoa then pasha kwenye frypan bila mafuta..itakuwa kama umepika leo

Ukipika matembele ukiweka tangawiz na pilipili manga yanakuwa matamu balaa

Juice ya parachichi weka ndimu au limao utaipenda

Ukitaka samaki wabichi wasivurugike au kung'ang'ania wkt wa kukaanga. Wapake unga wa ngano wakolee halafu kaanga ni watamu mno

Ukitaka kubadili pishi la wali weka kitungú maji, saumu na iliki kdg wkt wa kuchemsha maji then yachuje halafu pika wali wako unanukia balaa

Kama unatumia gesi kupikia wali, jaribu tumia maji ya baridi kupikia mchele unanoga hasa

Ukitaka utumbo uive haraka weka limao pekee bila chumvi kwa yatke maji ya kwanza.

1.Chumvi ikizidi kwenye mchuzi menya kiazi mbatata weka ganda acha uchemke chumvi itapungua sana

2. Ukiunguza wali kata kitunguu maji nusu weka kwenye wali Funika kwa dakika tano kinasaidia kutoa harufu ya moshi

3. Tui lisipokolea kwenye maharage weka unga wa sembe tikisa acha itokote hata kama nazi ni nusu itakua kama umeweka nazi tatu

4. Maharage ukitaka yaive upesi weka kijiko cha baking powder

5. Mchuzi wa maini ukitaka uwe rost nzito au mchuzi wowote na hauna nyanya za kutosha weka kijiko kimoja cha chakula unga wa ngano ukoroge na maji kidogo then weka kwa mchuzi wacha uchemke dk 5

6. Muhogo ukiwa hauivi weka making powder kijiko kimoja

7. Nyama ikiwa ngumu au ukitaka ilainike upesi kwangulia papai bichi

8. wali ukishika, ukiungua, kabla ya kufunikia, waweza pia tumia margarine au blue band, ukipakua harufu ya kuungua haitokuwepo tena

9.carrot iwe fresh kama imesinyaa kwa fridge weka kwenye maji ya barridi nusu saa itakua kama imetoka shamba……
Screenshot_20211123-092931.jpg
Screenshot_20211123-092916.jpg
Screenshot_20211123-092905.jpg
 
Tips: 1; Akandie butter au margarine yoyote, dough liwe laini lakini lisilonata mikononi wala sehemu ya kusukumia (tunasema dough limeiva)

2; Asikate chapati ndogo ndogo/ nyembamba, Chapati zake ziwe zina kauzito fulani, sio kama zile za kwa mama niwekee.

3; achomee butter au hata mafuta ya kawaida, ila pan inaweza mbadilishia matokeo, atafute pan moja nzito na non stick.

Vikorombwezo vingine kama kukandia maziwa au nazi havibadili muonekano bali zinaongeza ladha. Btw, Hizo chappo kwenye picha mwenye nazo hongera zake, mimi zangu ni nzuri lakini sio kama hizo za kwenye picha nadhani nimeshaweka picha humu za chappo moja au mbili.

Maji yawe ya moto ama vuguvugu
 

Similar Discussions

64 Reactions
Reply
Back
Top Bottom