Uzi wa vyakula tu

Kanda ya Kati
IMG_20210727_192531.jpg
 
Unaweza kujionea hapa kuwa chakula ambacho mwili wako unahitaji siyo chakula ambacho hisia zako au mdomo wako au utamaduni wako uliokulia unahitaji.

Wengi wenu hapa mkiona chakula hiki mtapatwa na kinyaa lakini ni chakula kilichojaa virutubisho na ambacho ndicho mwili wako unahitaji.

Tunasema kuwa umekua mkubwa kwenye masuala ya lishe na vyakula pale ambapo utaanza kula vyakula ambavyo mwili wako unahitaji na siyo vile ambavyo unavitamani wewe labda kwa utamu wake au kutokana na utamaduni uliokulia.

Kula vyakula ambavyo mwili wako unahitaji ni suala la kujifunza na kusoma juu ya vyakula bora na mapishi yake ili uweze kuvijua.View attachment 1870720
Nakubaliana na wewe. Ugumu upo kwa familia zetu hizi una mke mna watoto sita, ndugu zako na ndugu wa mkeo jumla mpo kumi na tatu ndani uwezekano wa kumudu kula hivi ni mdogo
 
Nakubaliana na wewe. Ugumu upo kwa familia zetu hizi una mke mna watoto sita, ndugu zako na ndugu wa mkeo jumla mpo kumi na tatu ndani uwezekano wa kumudu kula hivi ni mdogo
Upo sahihi kabisa mkuu.Tatizo kubwa ambalo linatusumbua waafrika ni umasikini wetu wa akili wa kuwekeza nguvu zetu,akili zetu,maarifa yetu pamoja na ujanja wetu katika kupata watoto wengi badala ya kuwekeza katika kupata utajiri.
 
Hapa Arusha kuna mboga wanaita mnafu ni tamu sana ikiandaliwa vizuri nimekuja kuijulia Arusha
Unaitwa Mnavu, hii ni mboga ya watu wenye asili ya tanga(wazigua) Mnavu mbali na utamu wake, lakini tena huongeza damu kwa watu wenye matatizo ya kupungukiwa na damu na hata maafisa wa afya huwashauri wananchi kutumia mboga ya mnavu ili kuinarisha MFUMO wa damu yao mwilini.
250px-Solanum_nigra_bgiu.jpg
 
Unaitwa Mnavu, hii ni mboga ya watu wenye asili ya tanga(wazigua) Mnavu mbali na utamu wake, lakini tena huongeza damu kwa watu wenye matatizo ya kupungukiwa na damu na hata maafisa wa afya huwashauri wananchi kutumia mboga ya mnavu ili kuinarisha MFUMO wa damu yao mwilini.View attachment 1871221
Uupate uliopikwa kwa tui la nazi... Mama! 👌😝 Kando yako bonge la ugali wa moto na glass yako ya juice ya ukwaju, baridiiiii! 🤣 🤣 🤣
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom