Uzi wa vyakula tu

IMG_0877.jpg

IMG_0657.jpg

Nyama kavu na samaki wa kuchoma mpishi mimi mwenyewe
 
Namna ambavyo mimi hupika kama nahitaji kupika vichache tu
Mahitaji

1.blueband 150gm

2.sukari robo

3.baking powder

4.ngano robo

5. Flavour

6 .yai

Namna ya kuandaa

1.unachukua blueband unaweka kwenye chombo ulichoandaa,unachukua sukari unaimiminia ulimoweka blueband then unachanganya,ukiwa na mixer inakuwa ni rahisi zaidi kama huna unaweza kutumia hata mwiko,unakoroga hadi uhakikishe sukari na blueband vimelainika kabisa ukiishika usisikie ule ugumu ugumu wa sukari,hapa ukitaka vilainike haraka unaweza kuisaga sukari kwenye blenda kabla ya kuchanganya na blueband.then unaweka yai

2.unachukua ngano unachanganya na baking powder(baking powder mi huwa nakadilia tu) then unachukua unga wako unakuwa unaweka kidogo kidongo kwenye mchanganyiko wa blueband na sukari unachanganya unaweka kidogo unachanganya.unachanganya hadi uone havinatii tena mkononi.ukimaliza kukanda mchanganyiko wako hakikisha ukivuta havivutiki,yaani ukivuta vinakatika

3.unaweka flavour uipendayo

4.unachukua kibao unasukuma kama unavyosukuma chapati,usisukume vinene sana au vyembamba sana unaweka vya kati tu,then unaanza kukata,kama una vile vidude vya kukatia unatumia kama huna hata kifuniko cha kopo unatumia

5.una oka kwa moto mdogo sana ni vyepesi kuungua ukizidisha moto.

6.epua subiri vipoe tayari kwa kutafunwa.

Nb.unaweza kutengeneza ukachanganya na maziwa,nazi e.t.c

Nb.ni rahisi kuelewa kwa video kuliko maandishi.
Ni rahisi sana kuvitengeneza hivi vidude
Upo vizuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom