Uzi wa vyakula tu

IMG_20210503_150739_336.jpg
 
Ahaaa Usinichoke mie kupika sijui hata maharage siwezi....Labda chai tuu

Hayo macaroni unaunga tuu sio
Mafuta....vitunguu maji....nyanya basi ?
Iko hivi : Hayo macaroni ni kama tambi au spaghetti zinauzwa kwenye packet zipo plain hazina taste yoyote.

Bahati mbaya mie yameisha hapa ngekupigia picha.

Sasa kupika yake: unayachemsha yenyewe mpka yawive yawe laini kiasi. Then unachuja mana yakiiva huwa yanabaki na maji yale ulochemshia so uyachuje ili yabaki makavu.

Then unapika kama roast la nyama ya kusaga au kuku alonyambuliwa. Kwenye roast sasa ndio unakarangiza ivo vitunguu maji, nyanya, na nyanya ya kopo plus spices kiasi.

Roast likishakolea kadri upendavyo.....unamimina yale macaroni yako ulokwisha yachemsha then unachanganya vizuurrriiii. Chakula tayari kwa kuliwa
 

Similar Discussions

64 Reactions
Reply
Back
Top Bottom