Uzi wa upatanisho, utani na urafiki kati ya wana JamiiForums walio na mirengo tofauti ya kisiasa

superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
4,905
2,000
Uzi huu ni maalum kwa cc members wa jf ambao hatupendani kabisa na tunapingana na kukinzana kweli kweli katika siasa.

Lengo lake ni ku absorb machungu yetu na TOFAUTI zetu.

Ule mkinzano tulionao kwenye majukwaa ya KISIASA tuupunguze humu kwa kutaniana na kutakiana heri katika maisha.

Natambua kwa uwazi ccm pamoja na kwamba kwasasa haitendi haki kwakweli mnaonea Sana wapinzani na mnazorotesha democrasia ya taifa letu ila bado naamini ndani ya CCM Kuna watu wazuri marafiki wazuri ambao ni friendly in nature despite hostile political situation.

Huu ni uzi ambao Sky Eclat aolewe na jinga lao na Erythrocyte aolewe na Kawe Alumni na mimi nimuoe kibibibi FaizaFoxy jamani.

Karibuni kwa couple na marafiki wenye mawazo tofauti ya KISIASA tuwe marafiki humu.

Ila usikubali kukutana na yeyote 'fesitufesi' utakutana na wasiojulikana.

Sheria za JamiiForums ndiyo ultimatum.

Superbug.
 
Top Bottom