Uzi wa Series/Movie ngumu kueleweka

Lost,
Game of Thrones (wabishi watabisha)
Tenet,
Faith (ya kikorea)

Sent using Jamii Forums mobile app
Game of thrones kwa mara ya kwanza naitazama niliona hahieleweki.

Ila kadri nilivyokuwa naitazama nilijikuta naelewa kupita kiasi na kufanya kuwa ndio series yangu bora ya muda wote.

Nimeweza kuitazama pia mara nyingi zaidi kuzidi series/movie yeyote.
 
Filamu zote hazieleweki. Pia, filamu zote zinaeleweka. Inategemeana na mtizamaji wa filamu husika.

Filamu zingine usipoelewa lugha tu iliyotumika humo ni kikwazo kuielewa filamu nzima.
 
Filamu zote hazieleweki. Pia, filamu zote zinaeleweka. Inategemeana na mtizamaji wa filamu husika.

Filamu zingine usipoelewa lugha tu iliyotumika humo ni kikwazo kuielewa filamu nzima.
Sio kweli mkuu kuna filamu ni rahisi kuelewa na zingine ni ngumu kuzielewa haijarishi mtu Una uelewa gani, hapa tunaongelea ni Kwa asilimia ngapi watu Fulani hawakuelewa movie Fulani kwahiyo ambayo itatajwa sana obviously ni ngumu kuelewa

Mfano hivi kuna mtu hajawahi kuelewa movie ya The Bodyguard ya jet Lee? Hii movie ata ispokuwa na subtitles na ata aangalie mtoto mdogo ataelewa Tu kwakuwa story yake inaeleweka

Haya tuje ni Wangapi hawajaelewa LOST? TENET? kwamba hawa wote uelewa wao ni mdogo? Jibu hapana story ya movie ndio ngumu na inahitaji uwe na background ya mada husika kama sio kitabu cha hiyo story basi uwe una elimu nayo, mfano TENET kama huna msingi mzuri wa physics ni ngumu kuelewa maana wanaongelea relativity theory kwahiyo Kwa movie za Aina hii ata uwe unaelewa vipi lugha bado itakuwa ngumu Tu kwako
 
THE WITCHER

Kila nikiiangalia nasinzia
Hahahaha. Episode ya 6 or 7 ndio wameeleza matukio yote.

Unaweza kusema ndio ilitakiwa kuwa episode ya kwanza.

Napenda sana movie/series za namna hii.

Jitahidi ufike episode ya 6/7 kama sijasahau.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom