HS CODE
JF-Expert Member
- Jul 5, 2019
- 1,779
- 4,330
Wakuu mambo vipi? Naona ma PDF yameanza kumwagika, changamoto ya malalamiko ya kwanini Utumishi wako kimya, inakwenda kuisha huku changamoto nyingine zinazotokana na kuitwa zinaanza kuibuka kwa kasi ya ajabu. Hii ni kwa wote, wanaokwenda kwenye Saili mbalimbali na hata wanaowategemea.
Tafadhali, naomba tutumie uzi huu kwa kutaja, nyumba za wageni ambazo ni rahisi mtu kukaa na kufika eneo la Usaili kwa gharama ndogo, maeneo zilipo, gharama na hata mawasiliano kama yapo. Hii itasaidia wengi hasa wanaokwenda kwenye Saili Dodoma kwa mara ya kwanza, au hata waliowahi kwenda na wakaishia kuteseka.
NB: Japo sio kwa umuhimu, inasemekana wengine hulala nje, baa na maeneo mengine kwa kutokuwa na pesa kabisa. Kama hayo maeneo yapo na ni salama naomba tusaidiane kuyataja ili watakaojikuta hali haziruhusu wakimbilie huko.
Asante.