crankshaft
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,410
- 3,376
Katika kijiji kimoja alitokea kijana mmoja aliyekuwa mahiri sana katika mchezo wa drafti.
Yoyote aliyejitokeza kucheza naye alimshinda,kutokana na hilo kijana alijawa na sifa majivuni na kiburi.
umaarufu wake ulikuwa mkubwa sana kijijini hapo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza mchezo huo na hakutokea mtu yeyote aliyeweza kumfunga kutoka kijijini pale.
siku moja alitokea mzee mmoja kutoka kijiji kingine. Alipofika katika kijiji kile kutokana na umaarufu wa yule kijana alipata kusikia habari zake.
basi mzee akaomba mechi na kijana lakini kijana kwa sababu alikuwa anajiona kuwa mkubwa akasema yeye hachezi na mtu bure ukitaka mechi na yeye lazima umlipe.
kwa bahati mbaya yule mzee hakuwa na pesa yoyote kwa wakati ule lakini alikuwa na punda ambaye alikuwa akimtumia kama usafiri wake.
ikabidi amuweke rehani yule punda ili kama akifungwa kijana atamchukua mpaka atakapompatia pesa zake. Kijana akakubali mchezo ukaanza. Mchezo ukapigwa paleee mwisho wa mchezo kijana akashindaaa.
(inaendelea)