Uzi wa kushuhudia mazuri ya kwenye ndoa, Tuyaweke pembeni yale mabaya yanayowatia hofu watu wasioe au kuolewa

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Hakika liko kusudi la Mungu katika mapenzi! Upendo ni tunda tam sana linalotafutwa na yule muovu!

Naomba kwa Uzi huu tuambizane Yale mazuri yaliyomo kwenye ndoa!

Ili wale tunao ogopa kuingia tupate hamasa!

Mliopo kwenye ndoa msishiriki kuyapa ushindi yale mabaya tu yasikike masikioni bali hata yale matam!

Naomba leo muyaweke hapa Yale mazuri ili wenye hofu wayapime na wingi wa Yale mabaya!

Kuna wakati huwa najiuliza! Hivi Busu la kila siku kwa mwaka mzima inamaana halina uzito kuliko teke la siku moja?

Hamuoni ya kwamba Wanandoa wanafurahia zaidi kuliko mda wa chuki?

Wanandoa jamii inawatazama nyinyi, je kwanini Hampendi kuonesha jamii Yale mazuri ili kuwaondolea hofu? Picha za mahaba mmezitia kufuli lakini za kuchinjana mnazileta bayana kwanini?

Naomba leo kwa yoyote humu anaejua tam yoyote ya ndoa atuambie hapa!

Story za kuchinjana na kuchomana visu na mkaa ebu leo tuziweke pembeni tuhesabu Faida za ndoa!

Wanandoa kama mtaamua kunyamaza hapa basi mtakuwa mmeshiriki dhambi ya kuyatangaza Yale mabaya yasikike zaidi kuliko mema!

Siyo kila siku tusikie negative tu!.. Naomba leo tuweke utam hadharani hapa ili ndoa iheshimiwe na watu wote! Nawangojea hapa huku nakula zangu karanga sitoki!

Siyo lazima uwe kwenye ndoa, hata kama haupo kwenye ndoa lakini unayajua matamu ya ndoa karibu ushuhudie hapa
 
Baadhi ya mambo mazuri ya wanandoa;

1. Mwanamke aliye kwenye Ndoa anaheshimika sana kuliko yule anayeishi peke yake bila mume
2. Mkiongozana wanandoa kisha mkapishana na Dada mwingine mwenye tako kubwa, Mume unajikuta unageuka kumuangali ila mke yeye huwa anakuangalia wewe mume wake - Hadi raha
3. Mkiishi vizuri kwenye ndoa, hali hii hupelekea hata watoto wenu wakiwa wakubwa nao hutamani maisha ya ndoa. Hivyo staili ya maisha ya wazazi huakisi pia kwenye maisha ya watoto wenu.
 
Kuna mambo mengine pekeyako unaona kama dunia inaelemea lakini ukimweleza mwenzi wako unapata unafuu na unaona maisha ni mepesi, wakati mwingine linatokea jambo la kifamilia umebanwa mwenzi anakuwakilisha na unaepuka lawama, kwa kifupi maisha ya kuishi wawili yana wepesi kwenye mambo mengi sana tofauti na ukiwa mwenyewe
 
Ukihitaji mtu wa kumweleza shida zako, hofu yako, huzuni yako, mawazo yako, furaha yako au hata mipango yako huna haja ya kumpigia shost, unamsubiri babe akirudi unaanza kumweleza, unadekezwa, unashauriwa, unatiwa moyo, na unnapata support ya kutosha
 
Ab

Absolutely full raha yani, ukiwa nae unavimba mbele ya mashostito, hubby hubby nyiiiiiigi si chako bhana akuuu
 
Hiyo 2 nimecheka, kumbe nayo ni faida ya ndoa
Baadhi ya mambo mazuri ya wanandoa;
1. Mwanamke aliye kwenye Ndoa anaheshimika sana kuliko yule anayeishi pekeyake bila mume

Back
Top Bottom