Uzi maalumu wa vifaa vya ujenzi

asiyetabirika

Member
Oct 14, 2019
46
55
Jamani naomba tupeane elimu juu ya vifaa mbalimbali vya ujenzi kama vile, bati ,vigae vya kuezekea, floor tiles,rangi,umeme, n.k, hii ni kutokana na utitiri wa matangazo ya vifaa vya ujenzi hadi kupelekea mkanganyiko kwa wenye uhitaji na wasijue ubora wa bidhaa husika unatakiwa kuwaje....

Lengo ni kuongeza ufahamu kwenye bidhaa husika, Unaweza uliza swali lako halafu wajuvi na wataalamu kwenye kifaa husika watakupatia jibu sahihi.

Karibuni...

FB_IMG_1565992675406.jpeg
IMG_20191015_193455_601.jpeg
 
ALAF ni baba lao aisee ila mwenzenu nimesimamisha ujenzi huku CEMENT IMEPANDA MFUKO NI 22,000 TSH

Kaka, ALAF na wengine tofauti yao ni Coating tu, ila ubora wa gauge ni ule ule sema ALAF kwenye coatingi ndipo anawapigia wapinzani wake
 
Nami nauliza tiles nzuri za kuweka kwenye nyumba ni zipi? Na je kwa nyumba ya urefu wa mita 8 na upana mita 6 (mstatili) haina kona kona nyingi inaweza nigharimu kiasi gani kwa gharama za tiles tu? Msaada wajuvi wa mambo ili nifanye finishing kwenye kibanda changu, niko mwanza ilemela.
 
Mafundi fungukeni hizi ndio kazi zenyewe
 
Sisi huku mtaani tumenunua sawa na kuezeka kipindi kimoja wenzangu wakafuata bei pungufu DRAGON leo langu linang'aa tofauti na wenzangu.
Bei rahisi inaumiza asee bora mtu ujipange taratibu uchukue kitu cha uhakika
 
Bei rahisi inaumiza asee bora mtu ujipange taratibu uchukue kitu cha uhakika
Eti unakuta bati ya migongo mipana ya rangi inauzwa 21,000 na MTU anafurahia bei huku akiona wewe uliyenunua Bati LA 35,000 umeibiwa...uzuri matokeo huwa hayachelewi
 
We unajua kwa nini tenda ya mabati ya miradi ya majengo ya serikali kapewa ALAF.Ni kwa sababu ya ubora wao
Mkuu bati za alaf kwa kanda ya kaskazini wanauzaje kwa mita kwa geji 28 na 30? Je kuna madhara gani endapo nitaezekea geji 30?
 
Back
Top Bottom