bachelor sugu
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 2,689
- 3,641
Amani ya mola daima iwe juu yenu wakuu.
Nikienda moja kwa moja kwenye mada ningewaomba tuelimishane na kupeana ushuhuda juu ya mimea mbalimbali(Ya asili ama ya kupandwa) na magonjwa mbalimbali inayoyatibu.
Itapendeza zaidi kama mtu ataleta mimea ambayo ameshaitumia na kutupa ushuhuda namna ilivyomtibu na hii itatusaidia kutufahamisha kiwango sahihi cha dozi tunachopaswa kutumia na muda sahihi wa kutumia ili kuweza kutuponyesha maradhi tunayohitaji kujitibu.Tukumbuke tu kuwa magonjwa yanaongezeka kila kukicha na yamekuwa changamoto kubwa sana katika maisha yetu na bahati mbaya zaidi hakuna tunachoweza kufanya ktk maisha haya pindi tunapokuwa wagonjwa hivyo tunahitaji kuwa serious katika Uzi huu kwa manufaa yetu na familia zetu.Binafsi nitaelezea tiba nilizozitumia na kuniponya katika maradhi haya yafuatayo;
Mmea wa 1; ALLOE VERA.
Magonjwa ;Malaria,Homa ya matumbo(Typhoid),Mzunguko wa damu(Blood circulation),UTI
MAANDALIZI
Majani 2 au 3 ya Alloe vera yenye maji ya kutosha,hata ukizidisha majani hayo hakuna madhara,
Yaoshe vizuri na Yakate vipande vidogo vidogo kisha yatumbukize kwenye chupa yenye maji safi na salama kwa kunywa yenye ujazo wa Lita 1 kisha funga chupa na uyaache kwa masaa 12 ili juice ya alloe vera iweze kujichuja na kuchanganyika na maji.
Baada ya muda huo chuja kikombe kidogo cha chai kimoja na unywe nusu saa kabla ya kula mara3 kwa siku kwa muda wa Siku 3.Hivyo ukiona inakaribia kuisha ile lita1 basi tengeneza nyingine kwa kutumia majani mapya ya alloe vera ili uweze kukamilisha dozi ya siku 3
Angalizo:Lazima uharishe katikati ya dozi au ukiwa unamaliza na hiyo kwangu ndio dalili kuwa dawa imefanya kazi hivyo usiogope.
Hakika ukikamilisha hiyo dozi magonjwa niliyotaja hapo nilienda HINDU MANDAL hospital na kupimwa FULL BLOOD PICTURE sikuonekana nina chochote katika hayo.
Mmea wa 2: MPARACHICHI(Majani yake yale malaini)
Unatibu;Jino linalouma hasa yale yaliyotoboka.
MAANDALIZI; Chuma majani yale mateke(malaini) ya mti wa mparachichi kisha yaoshe vizuri.
MATUMIZI; Tafuna majani hayo walau yawe ya kutosha kuanzia kumi(10)na kuendelea kisha mate yenye maji hayo uwe kama unasukutua kwa kumpeleka zaidi upande wenye jino linalouma kwa muda wa dk 5-10 kisha tema na usukutue.RUDIA zoezi hilo japo mara 3 kwa awamu moja.Fanya hivyo kwa walau siku 3 mfululizo na endelea kadri utakavyoona inakusaidia.
Hakika kuna siku niliumwa na jino na kukesha bila kufumba macho hata dakika moja na nadhani Salio wengi tuna jua jino linaumaje ila yangu nimtumie dawa hii leo hii ni karibu mwaka sijawahi kusikia hata kwa mbali jino likiniuma tena.
Huu ni ushuhuda wa mimea hiyo jinsi ilivyonitibu kwa viwango hivyo vya dozi.
Maumivu yakizidi muone daktari.
Naomba KUWASILISHA
Sincerely,Bachelor Sugu.
Sent using Jamii Forums mobile app