Uzi Maalumu wa kutaja Vijiwe maarufu vya kuuzia gahawa maeneo mbalimbali nchini

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,206
4,696
Yapo maeneo mbalimbali ( Vijiwe) yanayohusika na uuzaji wa kahawa chungu almaarufu gahawa.

Zipo huduma nyingine zinazopatikana kama alkasusu, tangawizi na kashata

Nimeona itapendeza kutaja vijiwe husika ili kurahisisha wateja kufikia maeneo hayo kwa urahisi na kupata huduma.

Karibuni:
1. Soko kuu - Arusha.
2. Kinondoni kwa manyanya mkabala na kituo cha mabasi ya kwenda posta - Dar es Salaam.
3. Buyuni Chanika mkabala na kituo cha mabasi ya kwenda mjini.
4. Kawe ndani ya kituo cha mabasi ya kwenda posta, kariakoo, mbagala, tegeta n.k.
 
mm ni mgonjwa sana wa kahawa roasted.. hapo chanika nishapata huduma hapo kwa hapo stand. iko safi.. pia kwa lushoto pale asante coffee ni kitu na nusu mzee..manzari pia imekaa poa mixer na novel zipo pale mziki mlaini kwa mbali huku ukiwa na kichupa chako cha coffee matata sana. i enjoy coffee more than beer aisee
 
Vipi kijiwe kile kilikuwepo mahakama ya kinondoni upande wa shule kipo?

Kuna kijiwe kingine kipo mwananyamala kama unaelekea sokoni.

Ila kijiwe kilicho nguli na hadi viongozi serikalini walikuwa wanakujaga ni cha magomeni shibam.

Bado vya kko sasa ....pale livingstone

Ova
 
Hivi vijiwe vya kahawa na vile vya draft 90% ya wanaopiga soga humo ni wazee wa makoti marefu na kofia za pama.

Jichangane kujifanya waijua sana nchi hii ukione cha mtema kuni
 
Hivi vijiwe vya kahawa na vile vya draft 90% ya wanaopiga soga humo ni wazee wa makoti marefu na kofia za pama.

Jichangane kujifanya waijua sana nchi hii ukione cha mtema kuni
Vipepeo weusi, hata pale feli kabla ya mzee hajaenda chattle.. wachuuzi wengi wa samaki walikua chenga sana ukijimix unajikuta Ununio.
 
Chato sokon pale kuna kijiwe kikubwa kimezindulowa na wajanja wa chatoh majuzi hapo gahawa bure ila sound ujue kupiga haswaaa maana jamaa hawajui kiswahil bali wanapiga mchanganyo wa kiswa na kichatoh
 
Dodoma nzima hakuna kahawa kama kahawa ya kwa Major! Kijiwe chake kiko maeneo ya Majengo. Kama ni mgeni basi ukifika maeneo ya soko la Majengo ulizia tu kwa Major
 
Kariakoo pale ukiwa unaingia stend ya mabasi ya mwendo kasi ule mlango wa mabasi tu ukitembea pembeni kidogo tu kipo kijiwe hapo cha wajuaji balaa
 
Back
Top Bottom