Uzi maalumu wa kupeana maujanja ya tiba/huduma ya kwanza ya mitishamba isiyo ya kishirikina

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
3,863
8,353
Heshima kwenu waheshimiwa.

Nauleta huu uzi kwa kujua na kuheshimu ukubwa wa jamii forums kuwa ina kila aina ya watu wenye vipaji, maarifa na karama na vipawa mbali mbali.

Huu uzi Ni ombi kwenu wakubwa, naomba kwa uzi huu tu-share tiba au huduma za Kwanza za mitishamba zisizo za kishirikina.

Binafsi nitaanza kwa kutoa chache Sana ninazozijua na ninategemea kupata maarifa zaidi kutoka kwenu kuhusu mitishamba.

N.B, swala la tiba hasa za mimea tusizifanyie masiara maana unaweza kuongea hapa jukwaani kwa masiara mwingine akaenda akafanya kweli kumbe umemuelekeza SUMU akapata madhara au hata kufa.

1 MAJANI YA VIAZI VITAMU

TIBA YA KIDONDA NDUGU
Kidonda huoshwa kwa maji ya vuguvugu yenye chumvi kiasi, AU oshea kidonda kwa maji na utomvu wa papai lilisoiva Wala kukomaa ambao bado limening'inia kwenye mti, kisha ponda ponda majani ya viazi vitamu (matembele) hadi yalainike sana kupata bonge la majani hayo, kisha tandaza/siriba kidonda kwa kutumia bonge la hayo matembele.

Siku za mwanzo wa tiba, usafishaji na uwekaji wa dawa hiyo ufanyike kila siku, kidonda kikianza kupata nafuu ya kuridhisha tiba ifanyike kila siku ya 2 (ipite siku 1 katikati)

2 MAKAMATA NGUO (Black Jack) AU EBIHURURA kwa kiha

a) TIBA YA MAUMIVU YA KUUMWA NA MDUDU KAMA NGE, NYIGU, NYUKI, SUNGU SUNGU n.k
Fikicha majani mabichi ya makata nguo/black jack kwenye viganja vya mkono au twanga/ponda ponda hadi yalainike halafu paka kwa kuchua sehem iliyoumwa na mwathirika atapata nafuu.

b) TIBA YA UGONJWA WA TRAKOMA/UGONJWA WA MACHO
fikicha majani mabichi ya makamata nguo/black jack kwenye viganja vya mikono hadi yalainike, kisha Yale maji maji yadondoshee kwenye macho ya mgonjwa. Yanasaidia sana na HAYAWASHI MACHONI (from my own experience)

3 SUKARI

TIBA YA JERAHA LOLOTE BICHI

ukipata jeraha lolote la wazi lisilo chimbika na lisilo hitaji kushonwa, basi haraka Sana futa damu halafu weka sukari, iache hapo hadi sukari iyeyuke kabisa. Kama unaenda hospitali Basi nenda kuchoma sindano ya kuzuia tetenasi tu maana ukishaweka sukari KIDONDA HAIKWEZI KUOZA, KITAKAUKA HADI KIPONE na HAIWASHI KWENYE KIDONDA.

ZINGATIA: Sukari itumike kwenye kidonda au jeraha kipya.

4 MNYAA

Sumu ya kuua MCHWA

changanya matone 10 ya mnyaa kwenye maji lita 1, changanya halafu nyinyiza / pulizia kwenye mchwa

Wakuu, kwa heshima na taadhima, naomba kuwasilisha uzi huu kwenu. Kwa yeyote mwenye maarifa na mitishamba naomba a-share na sisi hapa, au Kama ataona taabu kuweka hadharani elimu/ maarifa yake adimu naomba anitumie PM maana mm Ni mwanafunzi na mpenzi mkubwa na na hii elimu ya mitishamba na huwa nina daftari maalum kabisa la ku-note.

Kwa heshima kubwa kabisa naomba kuwasilisha.

KARIBUNI

Picha hii hapa chini ni dawa ya mtu aliegongwa na nyoka nimebahatika kuipata leo, Kuna babu amenipatia kwa mapenzi yake kwa kuona ninavyopenda elimu hii, na Kuna mautundu amenielekeza, nita-share nanyi hapa hapa namna ya kusimamisha sumu ya nyoka isisambae mwilini ili umuwahishe/umfikishe mgonjwa kwenye tiba.

N:B
MIMI SIFANYI BIASHARA WALA SITANGAZI BIASHARA HAPA, USINIFATE PM KUULIZIA DAWA, Mimi sio mganga.

Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
Dawa ya aliegongwa na nyoka, hii inarudisha sumu nyuma badala ya kusambaa na inaua sumu pia
IMG_20200331_131232_014.jpeg


Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
Hiyo picha ya hiyo dawa sijaipost hapa kutangaza biashara, hyo Ni kwa ajili yangu na haiuzwi.

Kuna watu watasema natangaza biashara, narudia sifanyi biashara hapa okay?

Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
1. Me nataka ya kutoa sumu mwilini....madawa ya Hosp meshakunywa mengi mno

2. Ya kunenepesha na kuongeza uzito NB. Me sio mwembamba ila nna uzito chini ya 60

3. Ya mafua & kikohozi

4. Kuongeza nguvu za kike... Kuna watu hawana hapa au wanazo chache ila wataona aibu kusema, nimewasaidia 😂😂😂

5. Ya Joints...baridi ikizidi unaweza shangaa tu kiwiko kinauma.

6. Kuongeza damu... Rosela, kuna watu humu mboga mboga mpaka washauriwe na dk

Nimechoka kuandika.
 
Depal, Namba 6

1 chemsha majani ya makamata nguo na kunywa maji hayo, au uwe unachanyanya majan ya makamata nguo kwenye mboga ule (hayana sumu)

2
Screenshot_20200331-163158.jpeg


Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
Natafuta dawa ya mtu mzima (above 70yrs) aliyevimba miguu. Hana tatizo la figo, ini wala sukari. Mguu unavimba kutokea kwenye unyayo kuelekea kwenye goti.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom