Uzi maalum wa kupata connection za ajira na machimbo mengine

ndugu zangu, kutokana na changamoto ya ajira inayotukumba, watu tumesoma lakini ajira zinakuwa ngumu kupatikana, kikubwa tujifunze kutokuchagua kazi, waswahili wenyewe wanasema ni bora kidogo cha halali kuliko kukosa kabisa ama ukapata kikubwa cha halamu ambacho kinaweza kukutia mashakani. vile vile "ukitaka kupata kitu ambacho hujawahi kukimiliki ni lazima uthubutu kufanya kitu ambacho hujawahi kufanya"

niliangahika sana kutafuta ajira, japo ni holder wa diploma ya uandishi wa habari, lakini nilijikuta ndoto zangu za kufanya kazi kwenye vyombo vya habari zinafifia kwani kila nilipo bahatika kupata kazi kwenye kampuni za habari, mishahala ilikuwa haikidhi vigezo haswa ukizingatia kupanda kwa gharama za maisha.

niliamua rasmi kuachana na taaluma niliyosomea baada ya kuona malengo yangu yanazidi kufifia. naomba niwape moyo ndugu zangu mnaotafuta ajira, msikate tamaa. weka mipango kichwani huku ukitafuta mbinu mbadala za kujikwamua.

safari yangu ya maisha ilivyoanza

View attachment 1742667
baada ya kuhangaika sana bila mafanikio kutafuta ajira inayoendana na elimu siku moja nikiwa huko Arusha, nilienda kuomba kazi kwenye godauni moja la bia, lililopo pale ngusero...kalibu na FFU. kwenye hilo godauni kulikuwa na mlinzi wa kampuni ya KK. ambayo hivi sasa inatwa garda yule mlinzi aliniambia "pale hakuna kazi" ila kama nitapendezwa na kazi ya ulinzi basi nipeleke vyeti vyangu vikafanyiwe uhakiki kwenye kampuni yao ya ulinzi ya garda, iliyopo huko kijenge karibu na Impala hotel ARUSHA.

kweli nilibahatika kwenda na walipo kagua vyeti vyangu viliwarizisha hivyo safari yangu ya ulinzi, ilianzia hapo, nilifanya mafunzo yao ya takribani siku 14, wakatutunuku vyeti kwenye mafunzo hayo tulikuwa walinzi zaidi ya 60 wenye elimu kubwa zaidi ya yangu. lakini wote tuliweka elimu zetu kando, tukaamua kuwa wafungua mageti ama wabeba virungu.
View attachment 1742669

kipindi naanza kazi hii ya ulinzi nilikuwa nalipwa 250k kwa mwezi lakini kuna miezi mingine ilikuwa inafikia hadi 280k...kiujumla kamshahala hako kalikuwa hakaitoshi kabisa, lakini nilivumilia nikajipanga na bahati ilikuwa yangu kwani kwenye hii kampuni huwa kuna promosheni ya kwenda kusoma kozi zinazoendana na mahitaji ya ofisi, kila ukienda kozi na kimshahala nacho kidogo kinatuna. kidogo hivi sasa kimshahala kimetuna na mimi natembea na pochi kubwa mfukoni.

View attachment 1742670

hivyo ndugu zangu, tusiogope kufanya kazi kwakuwa ndugu zetu watatucheka, kuna walinzi wana mishahala mikubwa kama watu wa serikali na pengine mikubwa zaidi ya watu wa serikalini. hivyo karibuni kwenye sekta ya ulinzi, japo bado napambana kuhakikisha ndoto zangu za kuendeleza taaluma niliyosomea lakini napambana huku nikiwa kwenye kazi ambayo kwa kiasi fulani inaniletea heshima mtaani ata pakitokea tatizo ninaweza nikatoa mchango japo kidogo.
View attachment 1742671

hivyo nimeona niwaletee hii fursa kwa watanzania ambao hamchagui kazi karibuni sana Gardaworld.

jinsi ya kujiunga na GARDAWORLD

1. uwe Mtanzania ambae utanzania wako hauna shaka kabisa
2. uwe na vyeti halisi vya shule {tumia cheti cha elimu ndogo kabisa isiwe juu ya kidato cha nne.... utakuja kunishukuru hapo baadae kwa mbinu hii}
3. uwe na cheti cha kuzaliwa
4. uwe mrefu haswa.
5. uwe na namba ya nida ama kitambulisho cha nida pia ukiongeza kitambulisho cha mpiga kura itakuwa poua
6.uwe na wadhamini wawili ambao watakuwa teyari kufika ofisini kwaajili ya kujaza fomu maalum za kukudhaminiView attachment 1742673

kama unavyo vigezo tajwa hapo juu, na upo Dar es salaam panda dala dala zinazoelekea Kawe haswa zinazopitia ubarozi wa marekani {moroco} kisha utashuka kituo cha KWA MWINYI {ukiwa mitaa hiyo unatakiwa kuwa makini muda wote ujiepushe na kushangaa shangaa haswa nyumba za karibu na ofisi ya Garda kwani ofisi hiyo ipo karibu na nyumbani kwa Rais mstaafu AL-HASSANI MWINYI na maeneo hayo yana ulinzi mkali}

View attachment 1742674
baada ya kufika kwenye ofisi za garda wakakufanyia vipimo na usaili wa awali utapewa maelekezo ya hatua inayofuata. hakuna rushwa katika kupata kazi hii, wala mimi mtoa post sina uwezo wa kukusaidia kuruka kigezo chochote ili uweze kupata kazi hii, kitakachokubeba kwenye kazi hii ni vigezo tu. ukiwa na vigezo stahiki utapata kazi. ukiwa huna kigezo mwenyezi Mungu akupe hitaji la moyo wako katika makampuni mengine yanayoendana na vigezo ulivyo navyo.

hivyo nafungua rasmi mianya kwa watanzania wenye mapenzi ya dhati kwa wenzao kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa kutuandikia hapo chini juu ya ajira iliyo karibu na wewe lengo ni kukwamuana, nina uhakika hii itakuwa sadaka kubwa kuliko kusaidiana fedha. na wale ambao tutabahatika kupata kazi kupitia uzi huu turudi kutoa ushuhuda ili wengine wapate pakuanzia.​

View attachment 1742676

MUNGU IBARIKI JAMIIFORUMS,

MUNGU WABARIKI WANA JAMIIFORUMS

MUNGU IBARIKI TANZANIA

MUNGU IBARIKI AFRIKA​
Ni kweli kabisa. Nami nilienda hapo mwezi uliopita, nilikuwa na vigezo karibia vyote isipokuwa urefu tu nd'o uliniangusha.
 
Nimekuja dar kujaribu bahati yangu maana najua ajira ni changamoto. Nimefika dar kwakuwa sina mtaji ikabidi nitegemee nguvu zangu. Nikaanza kutafuta kazi ya kufyatua tofali(za block) kama siku tatu hivi, sijafanikiwa maana kila chimbo nikienda watu wapo wa kutosha. SASA kama kuna mtu yyt yupo na connection ya vibarua, tenda mbalimbali anistue nipo tayari kufanya kazi.
 
Ingependeza kwa yule anayesema anatafuta aeleza na taaluma yake na ngazi ya taaluma hiyo pamoja na uzoefu wako, itasaidia kwa anayetaka kusaidia, kuliko kusema tu "Mi natafuta"
 
Bsc in Agricultural engineering and Mechanization
Nina experience katika
-Computer Aided design
-Machine maintainance
-Irrigation systems design
-Infustrial automation
-Agronomy
-Industrial safety and risks management
--Value chain analysis
 
Kama kichwa cha habari kinavyo someka
ningependa uzi huu uwe maalum kwa kupeana connection mbalimbali za kazi .

Katika kuzunguka kwangu kote kutafuta kibarua/kazi nimebaini kuwa bila kujuana na mtu ni vigumu kupata kibarua/kazi .

bila connection ni ngumu kupata kazi hivyo basi ni vizuri tupeane connection mbalimbali za kazi

Uzi huu utumike kuwakutanisha watu mbalimbal mwisho wa siku kupeana connection za kazi kutokana na ombi la muhusika.

Tupo watu mbalimbali jamii forum tukitafuta kazi/kibarua lakini kutokana na kutokuwa na connection tunakosa Hivyo basi uzi huu uwe msaada kwetu.

Elezea unahitaji connection ipi katika kazi kisha subiri kupewa connection na wadau mbali mbali katika kai/ajra Na tenda

Lengo ni kusaidiana na si vinginevyo. Tuweke roho mbaya pembeni kisha tuungane pamoja katika gurudumu la maendeleo Kwa taifa.
 
Back
Top Bottom