Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,862
- 5,680
Jamani hebu tukumbushane baadhi ya matukio ya kisanii ya awamu hii ya tano chini ya Magufuli toka iingie madarakani hapa wakituona sisi wananchi ni wajinga kumbe sisi tunawacheka tuu kuwaona ni waigizaji.
Mimi nitaonesha maigizo yao mawili kisha wewe utaongeza mengine kuonesha usanii wa hawa Matapeli wa siasa hapa nchini.
1. Tukio la kwanza la kisanii ni lile la kukamata Askari 9 Mwanza ikidaiwa walikuwa wanatorosha madini yenye thamani ya bilioni 27. Kiongozi wa Malaika alijitapa kuwa anazo taarifa za uhakika kuwa Askari wale walikuwa wakisindikiza Madini hayo na kuahidiwa kupewa bilioni moja na pia walishapewa milioni300. Cha kushangaza baadae Kiongizi wa Malaika akasikika anaagiza Askari wote warudishwe kazini na kesi yao ikawa imeishia angani.
2. Tukio la pili ni la kutekwa Mfanya biashara Mo Dewji. Kamanda Mambosasa alisema mfanya biashara huyo alitekwa na raia wa kigeni wazungu wawili.
Cha kushangaza zaidi raia hao wazungu eti wanazungumza lugha za kusini mwa Afrika. Na pia wakaja na gari lao mpaka Posta mjini wakaacha gari lao na silaha zao na kumuacha Mo Dewji hapo mjini kabisa wakatoweka.
Halafu yule Kiongozi Mkuu akaja na kibwagizo chake akimuuliza Kamanda Mambosasa kuwa eti msifikilie Watanzania ni wajinga.
Je, wewe una igizo gani la hawa jamaa? Lete hapa tuwaeleze hawa jamaa kuwa sisi Watanzania sio wajinga.