TUBONGE KIUME: Uzi maalumu wa Kijiwe cha Wanaume

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,985
69,371
Habarini za muda huu wakuu,

Leo nimeona tuzungumze jambo moja hasa kwa sisi WANAUME.

Nimeanzisha thread hii kwa ajili ya sisi kujadili "mambo yetu" kwa lengo la kufundishana, kuhabarishana, kuonyana na kuelekezana kadiri ya "miiko ya jinsi ya kiumeni"

Najua kuna watu wataniona mtu wa ajabu na kusema mambo gani haya lakini si kwa ubaya.. Nafahamu pia kuwa kuna wachache watanielewa na wengine hawataelewa au itachukua muda kuelewa lengo la huu uzi.

Leo acha nije kitofauti..wanaume tuna hulka ya kukaa na vitu sana moyoni na mwisho wa siku tunapata majanga, stress,sonona, kupelekea kufa mapema na kuonekana dhaifu, kwa hiyo ni vizuri kufunguka na kusema ya moyoni (Japo sijalazimisha mtu kufunguka mambo yake ya ndaaani sana/too personal) ili waliopitia changamoto kama zako wajifunze pia. Ukitoa mzigo ulio nao moyoni itasaidia kutibu tatizo ulilonalo kwa maana wanaume wenzako tuko hapa tutakushauri na kukupa a,b,c.... kuliko ufie na tai shingoni ni bora uje hapa kurefresh.

Vilevile katika ulimwengu wa leo, baadhi ya "miiko na asili ya uanaume" naweza kusema imeanza na inaendelea kupotea siku hadi siku kiasi kwamba inahatarisha ustawi wa kizazi imara cha wanaume kijacho huko mbeleni katika "malezi na makuzi". Kwa mfano, Wote ni mashahidi kuwa siku hizi kuna wanaume wanapenda kuwa kama wanawake, wana tabia za kike.. "Unakuta mwanaume amelegea, hawezi kukaza" kakaa kizembekizembe tu... inafikia stage 'mwana' anafanya mambo mpaka unashindwa kumtofautisha yeye na wa kike.

Kiukweli huwa naumia sana kuona "watani zetu" wakitusema sana kuwa Hatusimamii nafasi na wajibu wetu, mara tunapenda vitonga, ooh wewe dume suruali, wakiitwa wanaume na wewe utatoka? hatujiamini mara sijui hatujui kuhudumia na shombo zingine ambazo haziandikiki hapa zenye lengo la kutudhalilisha.

Tuelezee changamoto mbalimbali tunazopitia iwe ni kazini, kwenye ndoa/familia, mahusiano,mtaani, sehemu za ibada,sokoni n.k.. Tusemezane na tuinuane kama sio kusaidiana katika kuiweka jamii kwenye mstari na kuiweka nafasi ya kiumeni kama ilivokuwa zamani . Kama ni ishu binafsi kama ana ushauri anaweza kukufuata private DM au hata hapahapa kadiri kama unaona itafaa..

Wanaume tusonge mbele, tusikate tamaa na kusimama kidete/imara, TUSITETEREKE. Tukosoane na tuambizaneni ukweli kuhusu mambo kadhaa yanayohatarisha kupoteza 'hulka ya uanaume' ili kupunguza malalamiko kwenye jamii kwa namna moja au nyingine

Naamini kupitia uzi huu wanaume kadhaa watajifunza, watahabarika na wengine kutatua changamoto mbalimbali katika jamii yetu hii yenye changamoto lukuki. Mungu pia atulindie watoto wetu maana kizazi cha sasa hivi kinateketea kwa kivuli cha ''utandawazi'' tofauti na zamani.

Kuongezea machapisho au "maoni fundishi" kutoka vyanzo mbalimbali inaruhusiwa ilimradi tu iendane na maudhui ya uzi.

NB: -Naomba tutumie lugha zenye "staha" na nzuri kuepusha uzi huu kufutwa au kufungiwa comments, kwa kuwa lengo la huu uzi ni kuelimisha {mizaha, porojo na majungu si mahala pake hapa}

- Uzi huu ni kwa ajili ya kuelekezana, mnaosema ''umekuwa kungwi wa kiume'' shauri zenu chukua linalokufaa, halikufai pita tu pembeni.

Asanteni, lets discuss!

"Real masculinity is not dominating the weak, Real masculinity is empowering the weak"

"A man who is truly masculine embraces responsibility and loves, honours, protects and provides for his family and loved ones. He lives with integrity, motivated by conviction, not comfort or convenience. True masculinity is not determined by how much physical strength a man has but rather the strength of his character''

MEN ARE MADE
 
TUONGEE KIUME: Tutaogopa kuwatambulisha watoto wetu kwa jamii

Hatuwezi kuishi nyuma ya muda, labda tukiamua. Na kama mmoja wetu akiamua hivyo basi kuna mawili, kwanza huenda maisha yakawa mazuri kwake binafsi lakini yenye kuwakera watu wake wa karibu.

Pili huenda maisha yakawa yanamkera yeye binafsi na kumkera zaidi kila anayemzunguka.

Nyuma ya muda huu tulionao sasa sehemu pekee ya kuhifadhi kumbukumbu za picha ilikuwa ni kwenye albamu. Kila familia ilikuwa na ya kwake. Ukitembelea, ukipewa, ukaitazama utakutana na sura zote humo zilizonaswa katika nyakati tofauti — Baba, mama, watoto na zaidi.

Lakini katika muda huu tulionao mambo yamebadilika. Picha hatuziweki tena kwenye albamu, badala yake kwenye mitandao ya kijamii. Hii imetoa fursa kwa watu wapya hata tusiowafahamu wajue maisha yetu — japo sio kwa uhakika,

Japokuwa kwa kupitia picha mbili tatu tunazoziweka kwenye akaunti zetu za mitandao ya kijamii wanapata taswira fulani hivi.

Ukiweka picha ya ‘kagari kako’, watu watajua ushaacha kutembea umesimama siku hizi. Ukiweka ya mkeo wataelewa kwamba kumbe jamaa sio bachela tena. Ukiwaweka watoto watu watafahamu kuwa kumbe fulani ni baba.

Sasa hivi, wengi wanaotumia mitandao hii hawana woga wa kuchapisha picha za familia. Yaani mtu aliyeoa na ana watoto haoni shida kuchapisha picha ya familia yake kwenye mitandao yake ya kijamii —lakini tunapolekea hili litakatika na badala yake kama kuchapisha tutakuwa hatuweki kabisa picha za watoto wetu.

Hili litafika ukomo kwa sababu kwa kweli wanawake wanatuchanganya. Wanatukosesha amani na watoto wetu kwa kiasi kwamba usipokuwa na moyo mkubwa na mgumu, moyo wa kiume wenye kustahimili kweli kweli unaweza ukafa kwa ‘stress’ tena mapema kabla ya ahadi.

Tunakosa amani kwa sababu kiwango cha kumilikishwa watoto ambao si wetu kimekuwa kikubwa mno. Mwanamke anakwambaia ujauzito ni wako, unahudumia miezi tisa, anazaliwa mtoto, unalea miaka 6 halafu linaibuka jitu tu kutoka lisipojulikana linakwambia mtoto ni damu yake.

Inatisha, na hii itatufanya tuwe na wasiwasi na tuache kujivunia watoto wetu. Unaweza ‘ukapost’ picha yako uko na unayeamini kuwa ni mwanao kwenye mitandao ya kijamii halafu jitu likaja kuandikwa kwa chini. “Asante kwa kunilelea mwanangu.”

Wanaume tuna mioyo ya uvumilivu sana lakini kwenye matukio magumu ya namna hii mioyo yetu inashindwa. Inashindwa kwa sababu kwanza ni fedheha.

Ulishajinadi na mtoto miaka nenda rudi ukiamini ni mwanao na hata Jamhuri inafahamu hilo — yaani kila sehemu jina lako linatumika kama la baba wa moto, shule, hospitali na kila linapohitajika, lakini kumbe muda wote huu unamilikishwa mzigo wa mwenzio.

Kwa hali hii tutashindwa kuwatambulisha watoto wetu popote pale.
 
KWA WANAUME

Hatari: Aina 10 za Wanawake Ambao Mwanaume Hafai Kuwa na Uhusiano Nao Zaidi ya Kujitakia Matatizo.

Japo kila mtu anakasoro zake ila kuna tabia ndogo ndogo ambazo huleta maharibiko kwenye mahusiano na kuufanya uhusiano kubadilika kutoka kwenye amani na utamu unaopaswa kuwa nao na kuwa mchungu iwapo mwanaume asipokuwa makini wakati wa uchaguzi wa mwenzi anaetaka kuwa naye na nimejaribu kufanya utafiti na kuongea na wanaume walioachana na wenzi wao pamoja na wale waliopigwa chini japo wanang'ang'ania wao ndo waliowatema wapenzi wao na kuongea nao kwa mapana juu ya nini kiliwafanya wafikia uwamuzi huo mzito wa kuachana na wenzi wao, ndipo tukapata maelezo mengi na kukuandalia wewe mpenzi msomaji wa kiumeni.com aina ya wanawake kumi ambao inakubidi kufikilia mara mbili kwa marefu na mapana kabla ya uwamuzi wa kuamua kumpa sehemu ya maisha yako.

1. Mwanamke Mchungu: Unamjua yule mwanamke ambaye huwa na hasira na jinsia ya kiume muda wote? Huwa haishi kulalamika wanaume huwa ni wapumbavu, mwanaume haaminiki ni kama mbwa, yeye hasira yake huwa ipo juu ya wanaume muda wote na anaona mwanaume hawafai na hawana umuhimu wowote, hii inawezeka inatokea labda sababu ya katendwa na kuvunjwa moyo mara nyingi, mwanamke wa aina hii iwapo akiwekwa ndani huwa ni vurugu, kukosea inatokea ila kwake itakuwa ni matusi na kosa moja dogo atalichukulia kwa uzito wa ajabu ambao hata haupo, akiwa na hasira ni kutukana na kutoa maneno ya chuki na kashifa kutokana na kutendwa kwake nyuma na wanaume na mrundikano wa hisia ambazo hajazitatua moyoni mwake na hasira zake huwa ni za karibu maana anakuwa hamuamini mwanaume wake hivyo yupo tayari tayari kuangalia kosa ili apate sababu.

2. Mwanamke Mchoyo: Ukiwa unahitaji nyumba iwe na furaha na mwenza ambaye anahitaji furaha yako na ya kwake pia, unahitajika sana kukaa mbali na mwanamke mchoyo, mwanamke wa namna hii yeye huwa anakuwa anajiweka mbele tu kuangalia masilahi yake bila kuangalia hisia zako na tofauti na hapo hata ndugu zako wakija sababu ya ile choyo anasababisha mvurugano wa familia na siku zote huwezi kujikuta na furaha zaidi ya kuwaza kutatua tatizo hili kabla hujalimaliza limeingia jingine.

3. Mwanamke Mpenda vitu: mwanamke huyu la kwake pesa, hajakiona hiki anakitaka, kile nacho anataka bila kuangalia hali ya kiuchumi imekaaje, kamuona jirani Mama Naniii kavaa vile na yeye anataka ashindane nae, anakuwa anajari zaidi vitu vya kidunia bila kuangalia familia yake ipo katika hali gani, yupo radhi kuvunja familia, kuvunja uaminifu wake kwako na hata ule wa kidini ili tu hali ya kile anachokuwa anakihitaji moyoni kitimie. Na siku zote huwa hawezi kuwa mwenza mzuri zaidi ya kukuumiza kichwa na kupasua nyongo yako kwa mawazo ya kumridhisha pale ambapo hauna uwezo napo.

4. Mwanamke Mtongozwaji: Umevutika na yule mwanamke ambae yeye huwa na ukaribu na wanaume mmoja au mwingine kupitiliza? Anacheka cheka na mwanaume huyu na yule kama lile limjusi la kwenye mawe linahama kutoka jiwe moja kwenda jingine likitikisa kichwa kwa kujikubali bila kujishitukia na kufanya wanaume wengi wajihisi labda wanapendwa na msichana wako. Inakubidi uwe mwangalifu maana mwanamke wa hivi huwezi kumfanya mwenza wako maana iwapo hata ukimuoa tabia za namna hii huwa ni ngumu kuziondoa na atakuhisi labda unawivu unamfatilia sana sababu ameisha kaa sana nje ya msitari mpaka hajui mwisho wa mipaka ni wapi. Ukimuoa mwanamke huyu usije shangaa kusikia mkeo anasifa ya kujichekelesha kwa wanaume wa mtaa wako.

5. Mama Shughuli: Huyu ni shida, kila aina ya sherehe yeye kaalikwa na zote anaziudhuria, Diamond anaimba kwenye klabu ya karibu saa nane usiku yeye yupo, siku zote yeye anavaa nguo ya fasheni ya kisasa zaidi na ndo mkufunzi wa sherehe zijitokezazo, maisha yake yalishazoea hivyo na furaha yake na maongezi yake yanategemea hafla kubwa ijayo. Mwanamke wa sampuli hii huwa huwezi kumfanya mwenza na kuhisi utajenga nae familia, labda wewe ndo uwe mtunzaji watoto na mchunga nyumba wakati yeye yupo bize usiku na masherehe.

6. Mpenda kupewa kipaumbele: Japo ni jambo la kike kutaka kupewa kipaumbele na jamii, ila ukiwa ni ugonjwa hapa lazima jasho liwe linakutoka kila siku, mwanaume mzuri ni yule anaemjali mkewe, ila kama mke yeye ndo anataka umjali yeye tu, kila ukitaka utoke anataka akuone, hujaenda kibanda cha kuangalia mpira jirani ameshapiga simu urudi anashida na wewe, yeye anataka ya kwake tu bila kuangalia hata wewe unahitaji muda wako binafsi wa mambo mengine, ukiwa na mwenza wa namna hii unakuwa mtuma kwake badala ya kufurahia nawe maisha yako jinsi unavyozeeka polepole, kuishi kwako inakuwa ili umtimizie shida zake yeye.

7. Mwanamke Mbea: Je Saa zote yeye hana ya kwake, anataka kujua flani anaishije na anafanya nini?, mwanamke wa namna hii haumuhitaji. Manaume huitaji mwanamke ambae anauwezo wa kujenga familia na hii inaitaji akili ambayo inauezo a kutatua matatizo yanayoizunguka familia yake, kama mwanamke akili yake ipo bize kuaza Mama Majuto nyumba ya pili leo wamekula nini haezi kua na akili ya kujenga zaidi ya kuongeza umasikini ka kutumia muda wake kusema na kuongelea juu ya wengine badala ya kufanya kazi za kimaendeleo, na utakuwa na wakati mgumu pia wa kumfanya akufikilie kuhusu wewe, unafika nyumbani yeye yuko mtaa wa pili kaendea umbea.

8. Mwanamke Mwenye Deko: Kuna wanawake wengine wameshazoea kudekezwa kwao, na hana tabia ya kufanya kazi ili aweze kujitimizia mahitaji maana hajakuzwa hivyo na hii siku zote haipo kwenye sifa ya mwanamke mzuri na mke mzuri, hata kama ukijitoa na kujitahidi kumpa maisha aliyokwisha zoea, jua kabisa ukimuoa watoto lazima watatokea kwenye familia, na mama mwenye deko hawezi kukuza watoto maana watoto wanahitaji kazi kubwa ya kuwaangalia na kuwakuza. Hivyo mwanamke wa namna hii hatoweza kuwa mwenza mzuri.

9. Mwanamke Ambaye Hana Msimamo: Mwanamke ambae huwa na hali ngumu kufanya maamuzi ya chochote, (kikazi, kijamii, kirafiki, kimahusiano au kwa vyovyote vile..) na hivyo hivyo hatokuwa na uwezo kwenye maamuzi hasa kwenye ndoa, maana atakuwa bendela kifata upepo, mtu akimwambia hiki yeye atakiamini, kile vile vile atafuata huko huko, na itakuwa ngumu pia kuwa mke mzuri maana dunia imejaa maneno mengi na vishawishi vingi.

10. Mwanamke Mwenye Mdomo Mchafu: Je ukigombana naye kidogo maneno yake yanakuwaje? maneno ya kebehi hayamuhishi, akikasirika hata heshima baina yenu inakuwa haipo tena?, vipi kuhusu watu wengine anaowaona wapo chini ya hadhi yake?, Kama majibu unayojijibu yanaelekea hana heshima kwa binadamu wenzake basi hapo umekanyaga bomu, litalipuka muda wowote na iwapo likilipuka lazima litakuumiza kihisia, na iwapo ukimfanya akawa mkeo basi kaka lazima kila jioni baada ya kazi utapitia baa ilio kalibu nawe inaendelea kukupa pole kwa kuyapa shida maisha yako ambayo yangekuwa matamu zaidi iwapo ungegunduwa mapema.

TAFAKARI KISHA CHUKUA HATUA!!
 
Men,

Whenever you want to build a house,

GO BUILD.

Whenever you want to buy land,

GO BUY.

Don't ask for permission or validation.

IT IS YOUR HOUSE. IT IS YOUR LAND.

I feel sorry for men who are living in houses built by their women.



Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 

Wanawake washindane na ufanisi binafsi, si wanaume​

Juzi kati tulikuwa tunasherehekea kimataifa siku ya wanawake — Yaani dunia kwa pamoja tulikuwa tunawakumbusha mama zetu, dada zetu, shangazi, bibi na binti zetu kuwa nafasi yao katika maisha inafahamika, inathaminiwa na umuhimu wao unaonekana kuanzia ngazi za familia, kitaifa hadi kimataifa.

Kwamba labda bado mwanamke au wanawake hawajafikia wanapolenga lakini hilo linawezekana kama wataendelea kung’amua changamoto kubwa zinazowakabili na kuzifanyia kazi.

Hapa kwenye changamoto kuna tatizo — binafsi nakubaliana karibu na dunia nzima kwamba mwanamke ni muhimu duniani. Na ukifuatilia utagundua utofauti mkubwa uliopo kati ya mwanamke na mwanaume ni jinsia tu.

Isipokuwa wanawake wanafeli sehemu moja — kutaka kuithibitishia dunia kwamba wao wanaweza kuwa kama mwanaume au zaidi ya mwanaume. Hii ni propaganda inayowamaliza kila siku pengine bila wenyewe kufahamu.

Milele daima mwanamke hawezi kuwa kama mwanaume na haitakuja kutokea — Ndiyo, kama ambavyo milele daima mwanaume hawezi kuwa kama mwanamke na haitakuja kutokea kwa sababu utofauti wetu na wao upo kwenye upande wa kijinsia tu, jambo ambalo kama utaamua kuchunguza si ambalo limetufanya wanaume kuonekana ni wenye daraja la juu zaidi ya wanawake — bali ni utendaji ndiyo umetuweka hapa.

Sisemi kwamba wanawake si watendaji, hapana. Ninachomaanisha ni kwamba, tangu mwanzo wa maisha ya dunia, wanawake hawakuwa wakipata fursa sawa ya kuonyesha uwezo wao wa utendaji, karibu asilimia 75 ya kila kilichogundulika ulimwenguni sasa kimefanyika na mwanaume kwa sababu wanaume walikuwa wanapewa nafasi ya kufanya na kuonyesha. Hii imetengeneza daraja, wanaume tukaonekana ni wafanisi zaidi.



Sasa kunakowarudisha nyuma wanawake ni kutaka kuthibitisha kwamba wao wanaweza kuwa kama mwanaume. Nadhani, kwa sasa hawatakiwi kushughulikia hilo, wanatakiwa wageuzie jicho kwenye utendaji. Wanapopata nafasi, wafanye kitu kwa ufanisi kuzidi kawaida, yaani washindane na ubora binafsi kuliko kushindana na mtu aliye nje.

Nadhani hii ni kanuni inayowasaidia hata watu wengi waliofanikiwa. Kama unataka kufanikisha jambo pambana na wewe mwenyewe. Tuwaambie mama zetu, binti zetu, wake zetu, shangazi zetu, bibi zetu na kila mwanamke anayetuzunguka kuwa; Wanawake wanatakiwa kupambana na ufanisi wao wenyewe , si kujilinganisha na kushindana na wanaume.

Kwa lugha rahisi ya mfano ni kwamba, kama mwanamke atapewa nafasi ya uongozi leo hii, shabaha yake inatakiwa kuwa kiongozi bora — sio kuongoza kwa ubora zaidi ya wanaume waliowahi kuongoza.

Tunafahamu bado kuna changamoto kubwa ya kupata hizi nafasi, kwa sababu bado si wenye roho wote wanataka kutoa fursa zilizopo mikononi mwao kuwapa wanawake. Lakini hakuna kisichokuwa na changamoto chini ya jua. Mahubiri zaidi kuhusu nafasi kutolewa bila kujali jinsia yafanyike, na wanaopata nafasi wazitumie vizuri.
 

Jinsi mkeo, familia na baamedi watakavyokukumbuka ukizimika​



Ungependa ukiondoka duniani watoto wako wakukumbuke namna gani? Kwamba ni mwanaume mmoja, aliyebahatika kuwa na uhusiano na mama, kisha wakaoana, tukapatikana sisi.

Au mwanaume aliyewahi kumpenda mama yetu, akashindwa kuvumilia kuwa mbali na anachokipenda, akamuoa, kisha tukapatikana sisi, wakatuleta duniani na kutukuza kwa upendo licha ya kwamba kuna wakati maisha yalikuwa yanalazimisha isiwe hivyo.

Akatupambania sisi kama wanae kuhakikisha tunapata kila kitu kinachostahili kutoka kwa baba, kisha Mungu alipoona inatosha hapa duniani, akamchukua, kumtanguliza mbinguni, ili nasi, na mama yetu, siku tukienda huko, tukute anatuandalia sehemu nzuri kama alivyotufanyia hapa duniani. Unapenda wakukumbuke vipi?

Na mkeo akukumbaje? Kwamba ni mwanaume niliyekutana naye nikidhani ananipenda, nampenda, tunapendana, tukafunga pingu za maisha na tangu hapo maisha yangu yote yakawa ni kifungo cha ukweli – sina uhuru, furaha, amani kiasi kwamba sijui kwa nini Mungu alibariki ndoa yetu?

Au ungependa akukumbuke kwamba ni mwanaume ambaye nilipokutana naye, niligundua hakutokea tu, Mungu alimleta kwenye maisha yangu ili awe kiongozi wangu, ili kesho na kesho kutwa na siku baada ya kesho kutwa niishi nikifurahia pumzi niliyopewa.

Nikashindwa kuvumilia maumivu ya kumpoteza, tukafunga pingu za maisha, kwa maana ya kwamba, tulivifungia vitu vyote vinavyopoteza utamu na maana halisi ya uhai; amani, furaha, raha, upendo na uhuru ndiyo ilikuwa sehemu kuu ya maisha yetu.



Nikampa zawadi ya watoto, akanipa zawadi ya kuwalea na kuwapenda, na sasa Mungu akasema, nauchukua mwili wake, naurudisha ulipotokea, mavumbuni, lakini roho na nafasi naicha kwenu, ataishi moyoni mwako milele daima. Ungependa mkeo akukumbukeje?

Familia yako nayo ikukumbuke vipi? Kwamba ni yule mtoto wa mjomba, anayeishi Nyegezi, yule mwaka juzi kwenye msiba wa marehemu shangazi alikuja amelewa, akaamka usiku na kuanza kutapikia watu wakiwa wamelala.

Au ungependa iwe? Yule ndugu yetu anayeishi Kasulu, mtoto wa mjomba. Yule mwaka juzi wakati tupo kwenye msiba wa marehemu bibi, alitoa wazo kwamba tuanzishe kikundi cha kusaidiana kwenye shida na raha kwa ajili ya watu wote tuliowahi kukulia kijijini kwetu, ili matatizo yakitokea, tusipate tabu kama ilivyokuwa kwenye msiba wa bibi. Ungependa wakukumbukeje?

Na mhudumu wa baa unayopenda kunywa unataka amwambie vipi mwenzake kwamba wewe umekwenda? Amwambie, hulijui lile baba Jeusi Jeusi hivi, lile likilewaga linapenda ugomvi. Si lile lilimshika makalio Suzi siku ile, meneja akamuitia mabaunsa wamtimue.

Au aseme, ‘Jamani! humjui yule baba anakujaga na wenzake watatu, akilewa anakuwa na stori za kuchekesha. Anapenda sana kukaa viti vya hapa kaunta? Ungependaje?

Sasa hapa kupenda ni jambo moja tu, la pili na ndilo ambalo la msingi zaidi ni kwamba unatakiwa uishi katika matendo ambayo ndiyo yataamua ukiondoka watu wakukumbuke kwa namna gani. Kumbuka hakuna atakayedumu duniani.
 
Men,

Listen,

Protect your parents and siblings with all your might. Even if they are skunks, protect them. They are your blood.

Never allow strangers to talk trash about them.

If your parents and siblings have an issue with your wife, chances are they are 100% right. They can't be wrong and she is right. LISTEN TO THEM.

If you allow your woman to talk bulshit about your parents chances are you are an idiot.

Just lie down and die and we forget about you.

Simp!

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 

Mwanaume kutunza watoto wa kimada nalo ni tatizo​



Labda haikuwa tabia yako ya ndani ulivyokuwa mtoto, lakini kwa sababu uliwahi kuwa mdogo kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna kipindi ulijikuta una hamasa sana kufanya majukumu ya familia za watu kuliko familia yako.

Mfano nyumbani kwenu wanakutuma kwenda sehemu, mathalani gengeni, lakini unakataa. Kisha unazunguka mitaa miwili mitatu, unatokea nyumba ya jirani— huko mama mmoja anakutuma cha kufanana na ulichokataa nyumbani — unakubali haraka haraka utadhani mchuzi utakaokuja kuungwa kwa ndimu ulizotumwa na wewe unakuhusu.

Tabia hiyo ya kujitoa kwenye visivyokuhusu, wengine tulipokuwa tuliachana nazo lakini kuna wenzetu bado wanaendelea nazo.

Mtu ana familia yake, mke na watoto wawili watatu. Wanawe wanasoma kwenye shule alizotuahidi Magufuli kabla hajawa Rais; za elimu bure, hilo sio tatizo.

Wanapolala watoto haparidhishi sana, kuna kitanda kidogodogo na godoro lililonunuliwa miaka kama 10 hivi iliyopita, limekuwa jembamba, limelegea kama ulimi wa mbwa — pia sio shida sana kwa sababu watoto wenyewe kila siku wanaamka na furaha.

Wakiugua, wanatibiwa kwenye hospitali za kawaida. Pia sio tatizo sana, ndiyo maisha yetu. Kwenye msosi nako ndio vile vile. Watoto hata wakila wali na maharage mwezi mzima ‘hawanaga’ shida.

Nguo ndiyo majanga matupu, zina matundu kama chandarua. Ila ni sawa tu kwa sababu watoto wenyewe hata hawajali, kwanza wakiwa kwenye michezo hata mashati hawataki kuvaa. Maisha yanakwenda.

Lakini sasa baba wa watoto hawa hawa, kakamatwa na mwanamke huko nje. Mwanamke ambaye unakuta kwa bahati nzuri kama sio mbaya naye ana mtoto wake mmoja — kimombo wanaitwa ‘Singo Maza’.

Mwanamke anajua Baba ana mke na familia huko lakini yeye hajali. Kinachotokea. Baba huyu huyu mwenye watoto wanaolala watatu kwenye kitanda kimoja cha futi tatu kwa tatu, anamuhudumia huyu mtoto wa mchepuko kama ndiyo mwanae wa kumzaa — mtoto wa kimada anaishi kifalme.

Anasomeshwa shule za Santi nani kwa pesa za baba huyu huyu ambae wanae wanasoma shule ya msingi Darajani Tandale kwa Mtogole.

Mtoto wa kimada anavaa nguo za bei mbaya, nguo za maduka ya vioo anazonunuliwa na baba huyu huyu mwenye watoto wanaovaa nguo zimechanika kama wako Sudan Kusini.

Mtoto Jumapili anatolewa ‘out’ mabaharini huko akachezee maji kama samaki. Na ni kwa pesa za baba huyu ambaye wanawe kuogelea ni hadi mvua zinyeshe, dimbwi la nyuma ya nyumba ya mzee Matola lijae, wajirushe humo kwenye maji yaliyochanganyika na maji taka yaliyotapishwa kwenye vyoo.

Hatusemi tusisaidie watoto wengine huko nje. Ila habari za kuchipulisha mbegu za wenzako wakati zako zinaharibika kama haijakaa sawa sawa hivi. Tujichunguze wazee wenzangu.

 
Neno nakupenda na mke wako

Kuna hii hadithi! Kiongozi mmoja wa nyumba ya ibada alifanya mazungumzo maalum na wanaume wanaosali hapo. Walikuwa takribani wanaume 30, na wote walikuwa wanaishi ndani ya ndoa.

Kabla hajazungumza akawaomba wote wenye simu wazishike mikononi, wakafanya hivyo bila kuelewa ni kwa nini. Kisha kiongozi akawaambia, ‘naomba mwende kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi. Na muandike hivi, Nakupenda.’

Wanaume wote wakafanya hivyo. Kiongozi akawaambia tena, ‘tumeni huo ujumbe kwenda kwa wake zenu’ bila woga wala wasiwasi, wanaume wote wakatuma.

Baada ya kuhakikisha kila mwanaume ametuma, kiongozi akaomba wasubiri kwa dakika moja ili huo ujumbe mfupi ujibiwe, kisha atampa fursa mmoja baada ya mwingine asome jibu alilopata kutoka kwa mkewe.

Jibu la kwanza liliposomwa lilikuwa limeandikwa. “Baba Sara. Huu ujumbe ulikuwa unamtumia nani?”

Nyingine ikasomwa; “Utakufa kwa umalaya mwanaume wewe.”

Nyingine. “Mungu ameanza kukuumbua. Ulidhani utanificha siku zote. Kwamba milele daima sitojua uasherati unaoufanya?” Nyingine ikafanana na hiyo, na nyingine na nyingine na nyingine. Yaani majibu karibu yote yalikuwa yale yale.

Kwa nini? Kwa sababu wake wa wanaume wote waliokuwa pale hawakuzoea kupokea ujumbe mfupi wa namna ile kutoka kwa wenzi wao. Kimsingi neno nakupenda kutoka kwa mume kwenda kwa mke halistahili kuwa ‘breaking news’. Linatakiwa kuwa jambo la kawaida kwa sababu ndoa inaumbwa na upendo, na upendo unadhihirika kwa namna mbili tu, vitendo na maneno.

Vitendo ni uwanja mpana lakini maneno ni uwanja mpana zaidi na wenye nguvu kwa sababu kwenye kuzungumza kila kitu kinawezekana, kwenye kuzungumza unaweza kujiua kama ukiachwa na mpenzi wako, lakini ukiachwa na mpenzi wako kwa vitendo, kujiua sio jambo rahisi. Kwenye kuzungumza unaweza kumpeleka mkeo ‘shopping’ Dubai kila wikiendi, lakini kwenda shopping Dubai kila wikiendi kwa vitendo ni mtihani mgumu.

Maneno ni silaha kubwa lakini ni kwa wanaume wengi wa Afrika au tuseme tu Tanzania si desturi yetu hivi. Wengi tuna tabia kama wavuvi wanaotumia ndoano. Mvuvi wa ndoano hutumia chambo kwa jambo moja tu, kumvutia samaki. Samaki akishawishika, akanasa, basi kazi ya chambo imeisha. Wanakwambia, samaki kashavuliwa, chambo ya nini?

Kabla ya kumpata mwanamke wanaume tunatumia kila kitu kinachoitwa kizuri. Maneno mazuri, matendo mazuri, nakupenda nyingi na ahadi kibao, lakini ukishakamata mzigo na kuweka ndani hayo mambo hayapo tena.

Mtazamo wetu ni kama vile ukioa mwanamke ni kwa ajili ya kukupikia, kulea watoto na kukufulia, lakini mambo mazuri mazuri hayamfai, hayo ni kwa ajili ya vimada wetu, nje.

Ndo maana tukichukua simu kuwasiliana na wake zetu, ujue tunauliza kama luku imekwisha, fundi alikuja kutengeneza milango au kutoa taarifa kuwa leo nitachelewa kurudi nyumbani.

Hapana. Hawa wanawake wapo nyuma ya mafanikio yetu kwa kiasi kikubwa, wanastahili vitu viwili vikubwa, upendo na kuoneshwa wanapendwa.
 
The danger of feminizing men is that they stay off their higher purpose which is to pursue their masculine intentions.

They become sissies. They begin making poor choices in life then get stuck in the consequences of their choices.

The truth is that nobody cares for you as a man.

Your only hope is to save yourself.

Bounce back from rejection,

Bounce back from disappointments,

Bounce back from losses,

Bounce back from failure,

Bounce back so hard that people will think twice before disappointing you again.

Seeking sympathy is not a man's purpose.

A man's purpose is to seek a solution.

It doesn't matter how complicated your current situation is, but you MUST get a solution.

You are a man and the world is watching you and waiting for a solution from you.

Don't get stuck. Start moving.

"We must all either wear out or rust out, every one of us. My choice is to wear out.” — Theodore Roosevelt

#MasculinityFriday

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 
Men,

Keep off another man's marital or relationship tribulations,

Do not rejoice when your fellow man is being persecuted by his woman,

Do not sit in cahoots with women to gossip about other men's failures,

Do not be a woman.

Be a MAN!

#MasculinityFriday

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 

Watoto wetu hawajui…​



Kama mwanaume kuna wakati unagundua ulitua kwenye mti usiokufaa; yule uliyemuamini mwanzo kwamba akiwa mmiliki msaidizi maskani kwako nyumba itakuwa ni edeni ndogo anakwenda ndivyo sivyo, tofauti na matarajio.

Huenda yeye ndiye aliyekuwa chanzo cha mambo kuharibika au pengine wewe ndiye unayestahili kubeba huo msalaba, kwenu haijalishi, kwa sasa wote mko ‘bize’ kuangalia namna ya kuutua huu mzigo ambao labda mwanzo, kila mmoja aliamini anaweza kuubeba na kupita nao katika kila hali.

Tunapofikia hapa wengi huona njia pekee ya kurejesha amani iliyopotea kwenye maisha yetu ni kutengana, kugawana ustaarabu kila mmoja achukue hamsini zake na bila kufahamu hapa ndipo tunapokosea.

Kuachana ikiwa ndiyo suluhisho la kwanza kwenye matatizo makubwa ya familia huko ni kupotoka, ni kupotoka kwa sababu tunawapoteza watoto wetu kwa namna fulani na kuzipoteza roho za upendo walizozijenga juu yetu tangu watufahamu.

Watoto hawajui kama kuna kipindi hufikia uhusiano wa baba na mama unashindwa kufanya kazi, hivyo kinachotakiwa kufuata hapo ni kuachana tu.

Watoto wetu si watu wanaoamini kwamba kuna uwezekano wa kupata furaha kwa mama mwingine, furaha pekee na ya kweli wanayoijua ni ile inayotokana na baba mzazi, mama mzazi na wao kuishi nyumba moja, kula pamoja, kutazama TV pamoja, kwenda kumtembelea shangazi kila mwisho wa wiki na kila kitu si vinginevyo.

Kuachana hakujawahi kuwafurahisha watoto wetu kwa namna yoyote ile hata kama wanaona waziwazi kwamba mmoja wa wazazi hayuko sawa labda baba analewa sana kiasi cha kuwadhalilisha hata wao huko kwa majirani.

Au mama kuwa na tabia za ajabu zenye kuwafedhehesha. Wenyewe wanaweza kuchukia, hata wakafikia hatua ya kuropoka kwamba kwa nini baba na mama msiachane tu, lakini kuwa makini hii huwa haitoki moyoni kwa maana sawa na kile unachokisikia.

Unaposikia mtoto anasema maneno ya hivyo basi elewa anachomaanisha ni kwamba, kwa nini baba na mama msiweke pembeni, mwenye tatizo ajirekebishe ili maisha yarudi kama zamani... Hiki ndicho wanamaanisha.

Hatusemi kutengana ni ‘dhambi kubwa kuliko’, hapana, kuna hatua inafikia huoni kama kuna uwezekano wa ndoa au familia kuendelea kuwa kitu kimoja na chenye amani ni lazima utengano uwepo.

Lakini ni vyema kabla watu hawajafikia uamuzi wa kutengana wakaangalia maisha ya watoto wao yatakavyokuwa na kuangalia maisha si kwa maana ya kwamba watakavyolipia ada ya shule na mahitaji mengine muhimu hapana, kuwaangalia watoto maana yake ni kutazama watakuwa na maisha ya furaha na amani kiasi gani pindi agano la ndoa yenu likivunjika.

Watoto wetu hawajui kama kuna sababu ya kumfanya baba na mama watengane, tuangalie mara mbilimbili uamuzi huu kabla hatujaukaribisha katika maisha yetu.
 

‘Ushushushu’ kabla ya kuoa ulikuwa na faida zake enzi hizo​

Waliobahatika kuishi enzi za analogia wanafahamu jinsi kuoa katika kipindi hicho ilivyokuwa shughuli nzito. Ilikuwa unaweza kuwa umepata mtu unayempenda kabisa lakini hadi apitishwe na wakuu wa familia ni lazima awe amekubalika kweli kweli.

Kipindi hicho ilikuwa ni lazima kigori afanyiwe udadisi wa maana, ule wa kuzama ndani kabisa. Achunguzwe baba yake, wamjue, wajue tabia zake nje ndani, afuatie mama na usishangae mwendo huo ukafanyika hadi kwa shangazi na wajomba.

Yaani kuoa kwenye enzi za analogia hakukuwa na tofauti na usalama wa taifa duniani wanavyotafuta maofisa wake.

Ila yote ile ilikuwa ni upande wa mwanaume kuhakikisha mtoto wao hapotei, anapata mke ambaye atakwenda kuwa kiranja mzuri wa nyumba—ukiwa na mke safi nyumba mbona itapendeza tu.

Sasa siku hizi, enzi za dijitali, kuoa kwa maana ya kupata mke imekuwa rahisi sana. Mke na mume wanakutana kwenye daladala, wanabadilishana namba za simu, wanawasiliana whatsapp siku mbili tatu, ya nne anakuja nyumbani, ya tano mnaita ndugu kadhaa mnaunda kamati, ya tano mnasambaza kadi za michango ya harusi, mnamalizia na kuoana, mnakuwa wanandoa.

Ndoa za hivi zinatunyima fursa ya kufahamiana kiukweli, kufahamiana kiundani, kwa sababu kuna wakati, unabahatika kupata mke safi lakini kuna baadhi ya mambo yanamchafua.



Kwa mfano, kuna jamaa yetu ameoa mke safi tu, lakini kwa sababu hawakuwa wakifahamiana kindakindaki, mume amekuja kugundua kasoro fulani nje ya mke wake ambazo huenda alitakiwa kuzifahamu mapema.
Walitembelewa na mkwe, mama wa mkewe, lakini ajabu, mkwe alikuja na sheria zake na kuibadilisha nyumba kuwa kama shule ya bweni hivi. Jamaa anakwambia, siku ya kwanza alichelewa kurudi, akamkuta mkwe yuko sebuleni anamsubiri, alipoingia tu, anaulizwa eti: “Mbona umechelewa kurudi? Kama ratiba zako ziko hivi huku si kumtesa mwanangu?” jamaa akawa mpole akidhani ni masihara tu ya wakwe wa kisasa.

Lakini kesho na kesho kutwa mambo yakaendelea vile vile. Ndiyo jamaa akagundua kumbe kuna vitu alikuwa havifahamu kuhusu familia ya mke wake, kwa sababu mambo ya namna ile angeyafahamu, huenda angekuwa sehemu nzuri, angejiandaa kuyakabili.

Sema uzuri jamaa mwenyewe alikuwa na akili za kushikiwa, aliapa kwamba atatumia njia za kihuni ili moja kati ya mambo haya mawili yatokee—mama mkwe abadilike au arudi nyumbani kabisa aiache nyumba na amani kama alivyoikuta.

Alichokifanya ni kununua pensi moja kubwa sana, isiyomtosha kabisa. Halafu akaanza kuwa na ratiba za kuwahi kurudi nyumbani, kisha wakikaa sebuleni na familia, anahakikisha anaketi mbele ya alipoketi mama mkwe tena kwa kuitanua miguu—sasa kujichanua, jumlisha pensi kubwa, jibu analo mama mkwe kwa sababu baada ya siku mbili aliomba nauli.
 

Wanaume tusio na hela, tunaongoza kulalamika wanawake wanapenda hela​


Kama una uzoefu wa kuishi kwenye nyumba za kupanga utakuwa unanielewa zaidi nikitaka kuongelea tofauti kati ya mwenye nyumba anayemiliki nyumba nyingi na yule ambaye Mungu kamjalia kuwa na kanyumba kake kamoja na ndo hako hako ambacho dalali alikupeleka, ukapanga.

Kwanza mara nyingi mwenye nyumba anayemiliki nyumba moja huwa mnaishi naye humo humo. Yaani yeye na familia yake hutumia sehemu ya nyumba na vyumba vilivyobaki ndiyo hupangisha.

Bado haijathibitishwa kibaiolojia lakini kuna uwezekano wenye nyumba wa aina hii, neva za miili yao zimeunganishwa na nyumba zao. Yaani ni kama nyumba ni yeye, yeye ni nyumba.

Ukigongelea msumari kwenye ukuta wa nyumba yake ni kama umemgongelea yeye. Akikusikia, hata ikiwa usiku wa manane atakuja kukugongea kujua kulikoni? Mbona unatoboatoboa nyumba yake. Na akiwa mwanamke ndiyo utagundua kwa nini muuza kahawa anatembea na chombo cha moto lakini hana leseni.

Utaambiwa; “Wakati najenga hii nyumba hukunisaidia hata kubeba tofali. Kwa hiyo nakuomba usinitobolee-tobolee nyumba yangu.

Au…

Kama umeajiriwa na bosi ambaye ana biashara moja tu na ndiyo hiyo hiyo anayoitegemea hapa mjini. Mathalani kakupa pikipiki yake uwe bodaboda au upo kwenye saluni yake kama kinyozi ni mtihani. Hesabu hataki ipungue hata Sh 500, na hatakai maelezo mengi. Kwa sababu ndiyo biashara anayotegemea, ukimpunguzia unamlazimisha na nyumbani pia apunguze vitu.

Lakini wenye nyumba wanaomiliki nyumba mbili tatu au mabosi wenye vyanzo vingine vya kutosha vya mapato wala hawana hizo mambo. Wana utulivu kwa kila jambo kwa sababu wanatembea na roho zao, hawaziachi kwenye biashara walizokuachia au nyumba waliyokupangisha.

Naanza kuhisi ni kama kuwa na vitu vinavyokutosha kunakufanya kuwa mtu msafi kwa sababu hata wanaume ambao tunalalamika wanawake wanapenda hela ni sisi ambao tuna pochi za kuungaunga, tunahonga visenti senti vishilingi mbili tatu.

Mwanamke akinyanyua mdomo kukuelezea shida yake na kuomba umsaidie pesa kidogo atatue tatizo unaona ni kama kakuomba figo kakukosea sana. Utaanzisha mijadala kwa kuandika maujumbe marefu marefu kama makala za uchumi kwenye mitandao ya kijamii kutudadavulia jinsi wanawake wanavyopenda pesa na blaa blaa za kutosha.

Wakati wenzetu ambao mifuko yao iko vizuri, ina kiwango cha SGR wala hawana hizo. Kwanza hawangoji mpaka waombwe, wakiona mwanamke amepoapoa tu wanajua kuna tatizo, na kwa sababu mifuko yao iko vizuri, wanaamini matatizo yote yanamalizwa na pesa. Kufumba na kufumbua wanafanya muamala na hiyo kwao sio kuhonga wala kuchunwa, wanapenda kusaidia watu wanaowapenda basi.

Lakini yote kwa yote asilimia kubwa ya wanawake wa mjini, wanapenda kuomba hela.

Tutafute pesa

 

Mapenzi na ‘siasa chafu’ ni Kurwa na Dotto​



Kama hazifanani hivi lakini zinafanana karibu kila kitu. Ukiwa huna msongo wa mawazo wa madeni mengi uliyonayo, ukatulia na kuliwaza hili unaweza ukagundua ni kweli ndoa na siasa chafu zinafanana mno.
Hapa sisi tuna sababu tatu za msingi.

Hongo

Karibu ndoa zote zinaanza na hongo. Mmoja ambaye ataanza kuonyesha kumuhitaji mwenzie lazima kuna chambo atumie kumnasa (hasa muhitaji akiwa ni mwanaume). Lazima ataanza kwa kuhonga pesa mbili tatu, kumtoa mrembo out, kumnunulia vizawadi vya hapa na pale ilimradi tu binti aone kuna mtu anamjali. Binti akishanasa kinachofuatia ni kuisoma namba.

Au kama mchakato hautaanzia kwa binti mwenyewe, labda utaanzia kwa wazee wa familia. Lazima wazee wanunuliwe sana pombe ili kuhakikishiwa kwamba anayetaka kumchukua binti yao sio mtu wa kawaida.

Viongozi wote wanaofanya siasa chafu kwenye mataifa ya Afrika wameingia madarakani kwa mtindo huu. Wa kugawa vikanga na makofia kama mabanda ya juisi ya miwa kwa wapiga kura. Na wazee wa kijiji wakamwagiwa kilo za unga na mchele kama hawana akili nzuri.


Uongo
Kama hivi tunavyozungumza wewe ni mwanandoa, na uliingia kwenye ndoa bila kutumia hata chembe ya uongo, kuwa wa kwanza kuokota mawe kuwapiga waongo.

Ndoa ni uongo; mwanzo utamdanganya binti wa watu, “Mimi niko hivi, mimi niko vile, nitakufanyia hivi, nitakufanyia vile” halafu mwisho wa siku hatoona ‘vile’ wala ‘hivi’ yoyote. Kadanganywa. Na uongo haushii mwanzo tu, unaendelea hadi ndani ya ndoa.

Huku kwenye siasa tushadanganywa sana, tushaambiwa sana ‘mkinichagua mimi hii Shule ya Msingi Mtakoma itakuwa na madawati hadi vyooni’; lakini leo tuna miaka sijui 50 sijui 40 ya uhuru na bado kuna watoto wetu wanalijua dawati kama msamiati tu, hajawahi kuliona.

Ndimi Mbili

Mwanamke mnaoana leo, mnakaa miaka 10 kwenye ndoa, mnabarikiwa watoto watatu wenye afya. Miaka yote hiyo 10 mnaambiana nakupenda, namshukuru Mungu kupata mwenza kama wewe, wewe ni mwenza wa tofauti sana, bila wewe mimi siwezi kuishi na mapochopocho yote ya mapenzi humo ndani.

Lakini kwa bahati mbaya likatokea jambo likapelekea mkatengana hapo ndipo utaelewa maana ya neno ‘ndimi mbili’. Utaambiwa mwanaume gani wewe, nimekuvumilia tu miaka 10 yote hiyo, huna lolote, unadhani bila wewe siwezi kuishi na makorokoro yote ambayo ni kinyume cha yale mliyokuwa mnaambiana kipindi cha ile miaka 10 yenu.

Sasa hii huijui kwenye siasa? Leo fulani ataitwa fisadi na chama pinzani, akihamia chama pinzani watamsafisha na kusema hakuna malaika kama huyo. Mwanasiasa mwingine naye atakaa miaka 10 chama fulani akikipigania kichukue madaraka, lakini akihama atakwambia kile chama ni cha mafisadi, wabinafsi na wabaguzi — na aliiishi humo kwa miaka 10 akituomba wananchi tukiingize madarakani. Ni kazi nzito.
 
Mkuu niulize maana ya kuwa akili za kushikiwa kama huyo jamaa nimecheka sana😅😅eti anaichanua miguu ukijumlisha na pensi kubwa
akili za kuambiwa akachanganya na zake yaani akampiga mama mkwe tukio/zengwe ili ampe uhuru na mkewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom