Uzi maalumu tuliowahi kuibiwa na wasaidizi wa ndani(Housegirl)

kisokolokwinyo20

kisokolokwinyo20

Member
Joined
Apr 15, 2019
Messages
99
Points
125
kisokolokwinyo20

kisokolokwinyo20

Member
Joined Apr 15, 2019
99 125
Hivi majuzi tu nilikuwa na msaidizi wa ndani kwangu kutokea mikoa ya Kaskazini, alikuwa anatimiza wajibu wake vizuri kuanzia kuwahi kuamka, kufanya usafi, kupika na kumuangalia mtoto wangu mdogo.

Lakini hapa majuzi amenipiga tukio kwa kuniibia pesa zangu ninazotafuta kila siku kwa kuvuja jasho jingi.

Yani aliingia ndani kwangu kisha akapekua hadi akakuta wallet iliyokuwa imenona mshiko kisha akasepa nayo.

Hawa watu hata uwe mwema vipi hawaishi vituko.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kunde Ekeke

Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Messages
1,437
Points
2,000
Kunde Ekeke

Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2018
1,437 2,000
Nasikiaga wanasema mnawalipa kidogo hiyo aliyochukua ni bonus yake
 
Titans

Titans

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Messages
1,362
Points
2,000
Titans

Titans

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2010
1,362 2,000
Siri ya dada wa kazi ni kuwa wiki ya kwanza akianza kazi unaweza sema hapa nimeokota dodo kwa jinsi anavyojituma.Sisi tulipigwa 70k anyway hatukumhisi. Ila alipika wali boflo so wakati wa kula nikasema huu wali si mzuri. Kesho yake tumeenda church ile tumerudi tunakuta masufuria yote kayatoboa na msumari na kasepa zake.

Yeye ni mtu wa kuleeee "Mike T ningekuwa star, ningekuwa na mkwanja kachaa, ningekuwa mi mrefu na mkwanja kachaa Iringa town ingekuwa balaa"
 
NZURI PESA

NZURI PESA

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2011
Messages
5,834
Points
2,000
NZURI PESA

NZURI PESA

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2011
5,834 2,000
Nasikiaga wanasema mnawalipa kidogo hiyo aliyochukua ni bonus yake
Lina ukweli kwa wengine Ni malipo na mateso lakini kwangu Ni tofauti mkuu.
Naamini ule usemi usemao "mgogo MGOGORO" Miaka ya nyuma kidogo nililetewa house girl mshahara Laki na hamsini,kazi yake kubwa Ni kuangalia nyumba na kujipikia chakula chake Cha mchana KAZI ZOTE HUFANYWA NA WANAFAMILIA LAKINI ALINI IIBIA MTOTO KWA USHURIANO NA JIRANI WAKAMSAFIRISHA NJOMBE!
 
NZURI PESA

NZURI PESA

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2011
Messages
5,834
Points
2,000
NZURI PESA

NZURI PESA

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2011
5,834 2,000
Pole mkuu,ni bora kuweka mlinzi kazi za home fanyeni wenyewe madada wa kazi siyo wema kabisaaa
 
Sakasaka Mao

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2016
Messages
3,357
Points
2,000
Age
55
Sakasaka Mao

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2016
3,357 2,000
Lina ukweli kwa wengine Ni malipo na mateso lakini kwangu Ni tofauti mkuu.
Naamini ule usemi usemao "mgogo MGOGORO" Miaka ya nyuma kidogo nililetewa house girl mshahara Laki na hamsini,kazi yake kubwa Ni kuangalia nyumba na kujipikia chakula chake Cha mchana KAZI ZOTE HUFANYWA NA WANAFAMILIA LAKINI ALINI IIBIA MTOTO KWA USHURIANO NA JIRANI WAKAMSAFIRISHA NJOMBE!
Comments kama hizi zinaacha maswali mengi ya kiriwaya kichwani!

Mgelikuwa mnachanganua msala mzima ulikuwaje, maana msomaji unamwacha na 'ombwe' asijue kilichoendelea baada ya mtoto kuibwa!

Je alipatikana? Je huyo mwizi alitiwa mbaroni nk nk!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sheremaya

sheremaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Messages
1,827
Points
2,000
sheremaya

sheremaya

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2015
1,827 2,000
Comments kama hizi zinaacha maswali mengi ya kiriwaya kichwani!

Mgelikuwa mnachanganua msala mzima ulikuwaje, maana msomaji unamwacha na 'ombwe' asijue kilichoendelea baada ya mtoto kuibwa!

Je alipatikana? Je huyo mwizi alitiwa mbaroni nk nk!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanakera bora wakae kimya tu,,.
Eti waliniibia mtoto na kusafirisha njombe?
Kaishia hapo tu utazania huyo mtoto anathamani ya chupa ya chai au flat tv..
Kuibiwa mtoto ni issue nyeti mzee funguka mwisho wa siku alipatikanaje
 
kisokolokwinyo20

kisokolokwinyo20

Member
Joined
Apr 15, 2019
Messages
99
Points
125
kisokolokwinyo20

kisokolokwinyo20

Member
Joined Apr 15, 2019
99 125
Wanakera bora wakae kimya tu,,.
Eti waliniibia mtoto na kusafirisha njombe?
Kaishia hapo tu utazania huyo mtoto anathamani ya chupa ya chai au flat tv..
Kuibiwa mtoto ni issue nyeti mzee funguka mwisho wa siku alipatikanaje
Ka vumbi la Congo vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pancho boy

pancho boy

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Messages
1,552
Points
2,000
pancho boy

pancho boy

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2018
1,552 2,000
Wanaume wenzangu kama tulivyokubaliana kwenye kikao kilichopita..

Kitasa cha housegirl kiwe kibovu milele!
 
kisokolokwinyo20

kisokolokwinyo20

Member
Joined
Apr 15, 2019
Messages
99
Points
125
kisokolokwinyo20

kisokolokwinyo20

Member
Joined Apr 15, 2019
99 125
Wanaume wenzangu kama tulivyokubaliana kwenye kikao kilichopita..

Kitasa cha housegirl kiwe kibovu milele!
Hahah hawa huwa wako kwenye siku za hatari muda wotr yani ukiweka mali tuu inakuwa ulimbo ananasa...watch out hata kama kitasa kisiwe kibovu to that extent!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
chenjichenji

chenjichenji

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Messages
1,097
Points
2,000
chenjichenji

chenjichenji

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2013
1,097 2,000
Wanakera bora wakae kimya tu,,.
Eti waliniibia mtoto na kusafirisha njombe?
Kaishia hapo tu utazania huyo mtoto anathamani ya chupa ya chai au flat tv..
Kuibiwa mtoto ni issue nyeti mzee funguka mwisho wa siku alipatikanaje
Hahahahaaaaa...
Hapo anaweza endelea hivi..."Aliniibia mtoto na kumsafirisha Njombe ,mimi kesho nikaenda kwenye mishe nikaona mambo hayaendi kabisa nawaza mtoto tu nikaamua kurudi nyumbani kucheki cheki muvi baadae nikatazama tamthilia ya sultani halafu nikaamua nilale ili kupunguza mawazo...".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtena

mtena

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Messages
1,579
Points
2,000
mtena

mtena

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2014
1,579 2,000
Aisee kwa usawa huu kama ww na mkeo wote ni wafanyakazi na mnayegemea mkizaa mtoto mumtafute house girl kwa kimshahara chenu cha 80000 ni bora mkaacha kuzaa tu huyo mtoto atapata tabu sana

Pia istoshe kuwa hatapata malezi mazuri akiwa mtoto ni wakike ni hatari na akiwa wa kiume ndio kabisa
Na housemaid ukimnyanyasa anakosa pa kulipizia machungu yako hivyo jua basi atamlipizia mtoto wako mdogo ili kusuuza nafsi take

Nadhani mlipata kisa cha kule mabibo miaka ya nyuma 2010 house girl alimuweka mtoto kweny oven na yy akachapa sake raba!
Ndio mana nawapenda sana wanawake majobless( mama wa nyumbani) namzalisha weeeee analea watoto wangu vizur tukishafunga uzazi na mfungulia biadhara maisha yanaendlea

Love u sana mama .............

Sent using Jamii Forums mobile app
 
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
8,819
Points
2,000
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
8,819 2,000
Hivi majuzi tu nilikuwa na msaidizi wa ndani kwangu kutokea mikoa ya Kaskazini, alikuwa anatimiza wajibu wake vizuri kuanzia kuwahi kuamka, kufanya usafi, kupika na kumuangalia mtoto wangu mdogo.

Lakini hapa majuzi amenipiga tukio kwa kuniibia pesa zangu ninazotafuta kila siku kwa kuvuja jasho jingi.

Yani aliingia ndani kwangu kisha akapekua hadi akakuta wallet iliyokuwa imenona mshiko kisha akasepa nayo.

Hawa watu hata uwe mwema vipi hawaishi vituko.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wanaoitwa house girls siku hizi baadhi ni mawakala wa matapeli. Anakuwa anamilikiwa na mtandao wa matapeli halafu anatafuta kazi. Akipata anafanya vizuri sana siku za kwanza kumbe anawataimu tu na siku akipata mwanya anachukuwa chake na kusepa. Kundi la pili ni wale waliokuja mjini na kuasi... wamekuwa machangudoa. Na hivyo hivyo. Anatafuta kazi anafanya siku mbili tatu akapata nafasi anaiba na kusepa. House girl unayeweza kumuamini ni yule ambaye umeletea kutoka kijijini kwenu, na mnajua kwao.
 
Forum statistics

Threads 1,285,012
Members 494,369
Posts 30,847,295
Top