Uzi maalumu kwa wapenzi na tunaomiliki Toyota Corolla Rumion

Itatoweka sokoni Kama Verosa na Oppa!
Nimeiona huku mkoa haishawish kwa barabara zetu huku!
Na barabara za mchina huku zilivyo na mawimbi sijui itakuwaje!
Ziishie hukohuko kwenye barabara za makumbusho!
Kilicho towesha verosa na opa ni ulaji wa mafuta.
 
Hii gar ninzu kwa nje ukiindoa bampa la mbele, ndan wameboa sana kuweka dashboard katikati kama ist, vitz, raum, ractic n.k. kila mtu abiria anaina kila kitu.
Inakera balaa. Mtu anaingia kwenye gari anakuuliza mbona taa ya mafuta inawaka....
 
Kwa miaka zaidi ya mitatu (3) imetokea trend kubwa ya wabongo wengi kuipenda hii gari ndiyo maana Leo nimeona na Mimi nikiwa kama shabiki na mmiliki wa hii ndinga niisifie Kwa mambo machache...
Kwanza ukishikia neno corolla ujue kabisa kuwa ni gari Ngoma ngumu hasa Kwa upande wa engine pia gari hizi zimekuja Kwa Aina mbili za engine kuna Toyota rumion 1.8 CC 1790/engine code 2ZR na Toyota rumion 1.5 CC 1490/engine code 1NZ.

Sasa Kwa Leo nitazungumzia Sana hii yenye CC 1490 ambayo ndiyo wabongo wengi tumenunua,Kwa kifupi ni bonge moja la ndinga kuanzia ndani(interior design) na (exterior design) ina space ya kutosha kama uwanja wa taifa pia ina bonge moja la mziki WA kufa mtu kwasabb spika zimeanzia nyuma Kwa juu pamoja na twita zake huku spika zingine zikifungwa milangoni mwake.

Tukirudi Kwenye upande wa engine ni kuwa hizi gari zinaingiliana Sana engine zake kwasabb 1NZ imetumika Kwenye raum, sienta,pro box ,IST ,spacio, Porte na nyinginezo.. ndiyo maana tukianzia Kwa Magari yote hapa bongo ambayo ni mini van hasa Kwa Toyota nadhani rumion ndiyo Mpira (gari) wamaana huwezi kuifananisha na spacio, Porte,OPA,ractic,raum,IST, Sienta na pro box kuanzia muonekano wake wa nje na ndani ndiyo usiseme.
seat zake ni tamu Sana zenye kufanana na Toyota vanguard (Kwa mtu ambaye anazijua au ameshawahi kuzikalia) huku zikija na kitambaa cha moquette hiki ni mahususi kabisa Kwa Magari yenye akili pia taa zake headlight zinaudjustment ambayo unaweza kupunguza zikawaka mbele ya gari yako au zikawaka mbele zaidi kuanzia Mita 50 na kuendelea.

Pia Kwa upande wa gear box transmission inatumia mfumo wa CVT yaani kila kitu ni smooth Sana,hata Usalama juu brake ni WA kisasa ikitumia ANT -LOCK BRAKE PADS SYSTEM (mbele na nyuma kuna disc brake badala ya ule wa kizamani wa kutumia drum).
Mwisho nawatoa hofu Kwa wale wote ambayo waliokuwa wanataka kununua hii ndinga kuwa wasicheleqe kufanya maamuzi juu ya mashine
View attachment 1601824View attachment 1601825View attachment 1601826View attachment 1601827
Gari mbaya, muonekano kama Buti la jeje.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom