Uzi maalumu kwa ajili ya VIFUNGASHIO (Packages): kutana na wauzaji au wanunuzi wa vifungashio hapa

Superfly

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
965
1,966
Habari za wakati huu wapendwa? Natumai mko poa.

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Tanzania ya leo wajasiliamali tumekua wengi na tunajihusisha na shughuli za utengenezaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali, au utoaji wa huduma fulani. Katika shughuli hizi Vifungashio (packages) vimekua vikihitajika na kutumika kwa kiasi kikubwa..

Hivyo basi lengo la uzi huu ni KUKUTANISHA watu wote wenye uhitaji wa vifungashio vya namna yoyote ile au wauzaji (dealers) ili shughuli zetu kama wajasiliamali zisikwame.

Kama unauza kifungashio cha aina yoyote ile weka picha zake na contacts ili mwenye uhitaji ufanye mawasiliano na wewe.

Binafsi natafta "Glass jars" yaan zile container ndogo kama za kuwekea Jam n.k, natafta pia sealer (sealing machine), natafuta pia dealer wa vizibo kama vile vya soda. Nitafurahi sana nikipata msaada kutoka kwenu wadau.

KARIBUNI.
 
Du! Kujiajili kugumu sana hivi maombi ya kua makamu wa raisi wanatuma wapi?
Nasikia sirikali washatangazia watu waanze kutuma maombi
 
Mimi ninahitaji vikontena vya kuwekea matunda ya kukata ila nishapata vinapopatikana.

Hivyo vikontena vya siagi vipo kariakoo sokoni.
 
Mimi ni muuzaji wa vifungashio ,nipo gongo la mboto moshi bar ,kwa vifungashio aina zote nicheki 078864382
 
Habari za wakati huu wapendwa? Natumai mko poa.

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Tanzania ya leo wajasiliamali tumekua wengi na tunajihusisha na shughuli za utengenezaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali, au utoaji wa huduma fulani. Katika shughuli hizi Vifungashio (packages) vimekua vikihitajika na kutumika kwa kiasi kikubwa..

Hivyo basi lengo la uzi huu ni KUKUTANISHA watu wote wenye uhitaji wa vifungashio vya namna yoyote ile au wauzaji (dealers) ili shughuli zetu kama wajasiliamali zisikwame.

Kama unauza kifungashio cha aina yoyote ile weka picha zake na contacts ili mwenye uhitaji ufanye mawasiliano na wewe.

Binafsi natafta "Glass jars" yaan zile container ndogo kama za kuwekea Jam n.k, natafta pia sealer (sealing machine), natafuta pia dealer wa vizibo kama vile vya soda. Nitafurahi sana nikipata msaada kutoka kwenu wadau.

KARIBUNI.
Mkuu salama.?
Glass jars za ujazo gani??
 
Back
Top Bottom