Uzi maalumu kwa ajili ya nyimbo za kiafrika "afro-pop"

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
Siku hizi naweza kukaa siku nzima nasikiliza muziki kutoka Afrika bila kuchanganya na ile kutoka Ulaya na Marekani. Viwango vimeanza kuwa vizuri sana huku kwetu Afrika kiasi kwamba Muziki wetu unaanza kusikilizwa sana huko duniania kote. Sasa napenda kufahamu zaidi kuhusu muziki wa Afrika hasa wa kizazi kipya, na natumai kwamba kuna wasanii na nyimbo nyingi nzuri ambazo sizifahamu. Kama wewe ni mdau wa nyimbo nzuri za Afrika basi naomba utupie hapa halafu wadau tutaenda kuzitafuta.

Binafsi wiki hii nimetumiwa nyimbo mpya za ADEKUNLE GOLD, FIREBOY DML, WANDE COAL na wengine ambazo sikuwahi kuzisikiliza na nimetumia hili wiki lote kuzisikiliza. Ntaziweka hapa, na naomba kama wewe una nyimbo nzuri za kizazi kipya kutoka Afrika basi tafadhali weka hapa.

Cc: Surya
 
Back
Top Bottom