Uzi Maaluma wa Blockchain and Cryptocurrence au Altcoins

Mwana Ilala

JF-Expert Member
Jan 29, 2013
1,287
483
Hallo,
Kwa sasa dunia inakoelekea, huenda tusitembee tena na cash mfukoni,
Au hela aina ya fiati, ikaja kutoweka.

Kadri siku zinavyo kwenda, binadamu anazidi kuvumbua mambo mengi kupitia technolojia.

Kwa sasa kuna kitu kinachoitwa Sarafu ya Mtandao iliyovumbuliwa kwa mara ya kwanza na mtu mwenye Asili ya Japan kwa jina Maarufu kama Satoshi Nakamoto [Bitcoin 2008] Kwa kitaalamu inajulikana kama Cryptocurrence, hela ambayo iko kwenye uficho ikisaidiwa na technolojia ya Blockchain.

Technolojia hii bado ni ngeni kwa binadam hapa ulimwenguni. Na inakadiriwa ni asilimia tatu pointi 4, ya watu wote duniani wenye uelewa wa hii sarafu ya kimtandao. Kwa hapa Tanzania, Watu wenye hii elimu ya Blockchain na sarafu ya kimtandao, wanakadiriwa kuwa pungufu ya watu wasiozidi 9,800

Sarafu ya kwanza kutengenezwa na huyu bwana Satoshi Nakamoto, inaitwa Bitcoin 2008, Baada ya hapo zikafuata sarafu nyingine kama vile Ether, na nyingine nyingi zaidi sarafu elfu 2, hivi sasa zilizopo kwenye masoko tofauti ulimwenguni kote.

Fuatilia uzi huu,
Uweze kufaidika kwa technojia hii
Ambayo kwa muda mfupi, watu wametengeneza utajiri
Kwa kuwekeza kiasi kidogo tu cha fedha zao na kupata returns
Ambazo hadi wajukuu wao wataja faidi kwa hela walizotengeneza kupitia hii technology ya Blockchain na cryptocurrence.

Karibu uchangie, kile unachoelewa kuhusu hii technolojia ambayo
Inakadiriwa kufanya maajabu kwa muongo wa 2020’s



Sent from my iPad using JamiiForums
 
Back
Top Bottom