Uzi maalum wa simulizi za fumanizi

Financial Analyst

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
1,605
2,743
First of all poleni kwa wote mlio pitia tabu hii ya kufamania wenzi wenu. Maisha itabidi yaendelee, natumani mnaendelea vizuri.

Mara nyingi haachwi mtu salama, Mwanaume/Mwanamke lazima afanye tukio kutokana na jazba atakayo kua nayo pale atakapo mfumaniwa mwenza wake na mtu mwingine.

Stori zipo nyingi kitaa, za binafsi, jamaa zetu au jamii inayoutuzunguka. Kwa mlio nazo tunaombeni share zenu ili tuweze kujisomea.


STORY IFUATAYO NI KUTOKA KWA MWANA JF MWENZETU.

Too Gentle Maoni yangu kama Mwanaume katika miezi 17 ndani ya ndoa


"Ni hivi, mm ni daktari, mwanamke niliyekua naishi nae ni mkulima. Kwahyo kuna msimu wa kiangazi anakua idle sana maana haendi shambani.. inaweza tokea hata miezi saba yupo nyumbani kama housewife.

Kutokana na hiyo hali na mazingira ya pale nyumbani nikawa naona anakua bored sana na kujichanganya mda mwingi na mashosti yani umbea umbea, nikaona isiwe kesi nikamfungulia biashara.

Nilitafta frame mitaa ya soko kuu. Nikamfungulia duka-genge (nadhani nimeeleweka) yani niliweka mahitaji ya dukani pamoja na gengeni ktk kiofisi kimoja. Ikawa asubuhi napoenda kazini namdrop pale gengeni, jioni nikitoka mapema narudi home kupumzika ikifika mda wa kufunga ananishtua naenda kumfata na kausafiri kangu. Hiyo ndio ikawa ratiba.

Sikatai, yule dada mcheshi sana na ana msambwanda wa kufa mtu. Kama biashara zilivyo akaanza kua na mazoea na masela wa pale sokoni, sikua na wasiwasi kwavile nilijua ni mambo ya business ukiwa kauzu sana wateja ni ngumu kukuzoea.

Kuna mwamba nilikua namkuta mara kadhaa mida ya jioni anasimama pale dukani kuhudumiwa analeta leta viutani vya kijinga jinga kwa wife, wife nae anajichekesha chekesha kifala fala tu. Msela ana ofisi yake ya kukopesha ela mtaa wa jirani ila aliweka sana mazoea na wife.

Ghafla mtaji ulivyokua nikaona wife dharau nyingi analeta, mara nikitaka kumpitia jioni analeta sababu nisimfate atafika chap na boda na visingizio vya kifala fala.

To make the topic short, pale kitaa wahuni wengi ni machizi wangu wakanitonya mchizi wa mikopo anamega wife wakanichorea ramani fresh na hivi juzi jmosi tukawanasa red-handed lodge, nikafukua mtaro wa jamaa na wife nikamuachia. Naskia mwanamke amerudi kwao na kwangu anaogopa kurudi kamtuma rafiki yake afate nguo...

Sorry kwa unandishi mbovu nilikua night jana usingizi mwingi sana sikulala kabisa"
 
From Nyendo




"Joyce Kilia amezungumza na familia ya Vicent (Mwanamme anaedaiwa kufumaniwa na mke wake)

Akizungumza Agnes Vicent Malya( Mfumaniaji) anasema yeye ni mke wa ndoa wa Vicent Malya na wamefanikiwa kupata watoto wawili na mme wake.

Anasema ilikuwa tarehe 18/5/2020 aliondoka asubuhi na mme wake, mme wake alikuwa anaenda mahakani kutoa ushahidi wa kaka kesi ya kaka yake. Anadai waliachana na mme wake vizuri eneo la magereza.

Anadai akiwa sokoni aliambiwa na mmewe kuwa alishafika na mme wake akamwahidi kumtumia 12000 kwa ajili ya mafuta ambayo mkewe alikuwa ameomba na wala haikutumwa hela hiyo wala hawakuwasiliana tena.

Anadai ilipofika saa 12 jioni ndipo alipompigia na kumuuliza kama bado yupo mahakamani na akamjibu kuwa yupo mjini, naye akamwambia mmewe kuwa yeye bado yupo msibani maana alikuwa kaenda msibani, mmewe alimjibu kuwa atakwenda amsubiri arudi ili waondoke wote.

Anadai alimsubiri mmewe bila mafanikio na ndipo alipoamua kuchukua bodaboda na kurudi nyumbani, na ilipofika saa tano usiku alimpigia simu mmewe lakini haikupokelewa mpaka yeye alipoamua kulala bila kumuona mmewe akirudi nyumbani.

Siku ya tarehe 19/05/2020 aliamka na kuendelea na majukumu ya kifamilia na alimpigia mmewe na akapokea kisha kumjibu kuwa ameamka salama.

Baadae alielekea shambani kuchukua mahindi na alifika nyumbani kwa mama mkwe wake na kwenda kuchukua funguo mahali wanapowekaga na hakukuta funguo bali sadolini ya maji ambayo kwa kawaida haikai hapo alipoikuta.

Alimtumia meseji mme wake kumuuliza funguo ipo wapi? Akajibu kuwa ipo kwa dada yake na mlio wa meseji ulisikika ndani ya chumba ambacho yeye mke kasimama dirishani.

Ndipo alipogundua kuwa mme wake yupo ndani ya nyumba hiyo ndipo alipomwambia kuwa kama yupo Boma apokee simu na ndipo alipiga na simu ikaitia humo ndani.

Na baadae alimuuliza wifi yake kama funguo ipo kwake ndipo wifi yake huyo alikwenda eneo la tukio na dada mtu alikana kuwa na funguo hiyo.

Na baada ya hapo waliamua yeye na wifi yake wakaanza kupiga ukunga na ndipo walipochungulia kwenye vitundu vidogo vya dirisha na kumuona aliwa kitandani na mme wake.

Anadai kuwa baada ya wao kupiga ukunga ndipo mmewe alipotoka ndani mbio na kumpush kisha akakimbia, baada ya hapo alimuona mwanamke yule ambae ndie mwizi wa mmewe na kuanza kumpiga.

Anasema kitendo kile sio kizuri alifanya hivyo kwa kuwa alishindwa kuvumilia maumivu ya kuchukuliwa mme na mwanamke ambae kashamuonya mara nyingi kwa swala la kutembea na mmewe.

Mwanaume nae azungumza

Amekiri kuwa mfumaniaji ni mke wake wa ndoa pia mfumaniaji ni mtu ambae walifahamiana sehemu ya kuuzia vinywaji na walikuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Anadai wana uhusiano uliodumu kwa miaka mitano na anadai kuwa alikuwa anatumia gharama kubwa kumhudumia dada yule hata anashindwa kukidhi mahitaji ya familia yake na mpaka biashara za mwanaume huyu ziliyumba kwa sababu ya mwanamke huyu.

Anadai kuwa mwanamke huyu alihamia Mwanza na hivyo Vero alikuwa kaenda kwa Boma muda huo kuoka Mwanza. Na anadai kuwa mwanamke huyo alimkataza kurudi nyumbani na kulazimisha walale wote, na akatoa ushauri wasiende gesti maana ni gharama na akadai hela ya gesti ampe na akashauri waende pale kwenye nyumba ya mama yake.

Anadai ni kweli walifumaniwa na tuhuma za kuwa Vero aliibiwa sh. laki tisa na elfu saba ni uongo kwa kuwa huwezi tembea na hela hiyo ikaibwa na usitoe taarifa polisi.

Anasema anashukuru kwa tukio hilo kutokea kwake ni fundisho ili alirudi kwa familia yake maana dada huyo amechangia kumfilisi na miradi yake yote imekufa na hata hela ya kupanga nyumba hana anaishi kwa shemeji yake.

Amesema anaomba wanaume wenzake wenye tabia kama yake waache Maana sio jambo zuri.

Pia soma
"
 
From Kanungila Karim




DUNIA ina mambo! Wakati wanawake wengi wakiitamani ndoa ili kujijengea heshima, mambo yamekuwa tofauti kwa mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jackline Chuwa ambaye amekwaa skendo ya kudaiwa kufumaniwa.

Imedaiwa kuwa, Chuwa alifumaniwa na mume wake Leonis Ngasa akiwa na mwanaume mwingine (jina halikupatikana mara moja) hivi karibuni wakati ndoa yao ikiwa ingali na miezi miwili tu na ushee.

NI TABATA DAR

Imedaiwa kuwa, tukio hilo limetokea maeneo ya Tabata Shule jijini Dar ambapo shuhuda wa tukio hilo, alilitonya Ijumaa Wikienda kwamba baada ya kufumania, mume wa Jack (Ngasa) alijikuta ametupwa nyuma ya nondo Kituo cha Polisi Tabata-Shule kwa tuhuma za kumpa ‘vitasa’ mkewe.

“Yani jamaa alipewa mchongo kwamba mkewe yupo na jamaa sehemu maeneo ya Tabata-Shule, akafika fasta sasa kwa kuwa jamaa alikuwa na hasira, akaibua varangati la kufa mtu. “Yule mwanaume aliyekuwa na Jack akatoweka hivyo jamaa akabaki na mkewe na kumtembezea kichapo kikali kwelikweli, alimjeruhi sana damu zikawa zinamtoka kichwani,” kilidai chanzo.

AMPELEKA HOSPITALI

Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya kumshikisha adabu mkewe na kuona amemuuza sana, alimchukua na kumpeleka katika Hospitali ya Madona kumtibia. “Walipofika pale Ngasa akajaribu kupindisha maelezo kuwa mkewe amepata ajali ili kuepuka msala na yeye aweze kuondoka akasema amuokota akiwa amepata ajali, mkewe aliposikia kauli hiyo akaja juu na kusema si kweli bali amempiga.

ADAIWA KUINGIA MITINI

“Aliposema hivyo, Ngasa alilazimika kutoweka eneo hilo ambapo Jackline naye alimuunganishia kwa kumuitia mwizi na ndipo alipofukuzwa na watu wa bodaboda kisha wakamtaiti alipokuwa karibu na Kituo cha Polisi Tabata-Shule. Polisi wakatokea, wakamtia ndani Ngasa, wakalichukua na gari alilokuwa nalo mkewe eneo la tukio kisha mwenyewe wakamkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.”

IJUMAA LAANZIA POLISI

Ili kujiridhisha, baada ya kupata taarifa hizo, Ijumaa Wikienda lilifunga safari mpaka kituoni hapo ili kupata ukweli wa jambo hilo ambapo askari mmoja wa kituo hicho alikiri uwepo wa tukio hilo lakini akaomba hifadhi ya jina kwa kuwa hana mamlaka ya kuzungumza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom