Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge na 11 ya mwaka 1995, na ilianza kufanya kazi tarehe 1 Julai 1996.

TRA ndio wahusika wa mambo yote yanayohusisha kodi mbalimbali za Serikali Kuu na Ushuru mbalimbali.

Uzi huu ni maalum kwa ajili ya matatizo mbalimbali yanayopaswa kutolewa ufafanuzi na TRA kwani kuna maafisa mbalimbali wa TRA hapa ambao wanaweza kutoa msaada au watu ambao wamewahi kupata issues kama hizo wakakupa mwanga.

Zingatia

Kutaja aina ya bidhaa inayotakiwa kulipiwa ushuru au aina ya huduma husika

Karibuni
 
Wadau habarini za mida hii,

Leo nilikuwa kwenye mchakato wa kulipia mapato ya biashara yangu TRA ila nilipofika kwenye ofisi zao nikaambiwa napaswa kuhamisha TIN yangu kutoka nilipoikatia (mkoa tofauti na nilipo) kuleta mkoa nilipo ndipo niweze kulipia mapato.

Naombeni uzoefu kwa yeyote ambaye alishafanya hii, utaratibu wa kuhamisha ukoje?

Asanteni
 
Ni rahisi. Muandikie email au barua meneja wa mkoa husika ukimueleza kua umehama mkoa. Ni jambo la dakika 2 tu wanahamisha fasta.

Hata ukimpigia simu meneja wa mkoa uliokua ni jambo la muda mfupi tu.
 
Sasa mkuu wewe ulikuwepo kabisa kwa wahusika muhimu wanaojua haukuwauliza alafu unauliza huku ? ila nadhani kwa kuwaandikia barua officially wanaweza wakawasiliana information zako zikawa transfered from point A to B

Pia ingawa TIN ni moja ila biashara hata kama ni branch au nyongeza ya biashara nyingine inakuwa na certificate yake.., kwahio kama una biashara nyingine mkoa mwingine na hii mkoa mwingine utapewa certificate mbili zenye namba moja ila location tofauti..,

Kama ulifunga ile biashara ya kule itabidi / ilibidi uwaandikie barua ya kuacha kufanya biashara ili waache kuhesabu madai.., unless otherwise mpaka kesho wataendelea kukudai
 
Wadau habarini za mida hii,
Leo nilikuwa kwenye mchakato wa kulipia mapato ya biashara yangu TRA ila nilipofika kwenye ofisi zao nikaambiwa napaswa kuhamisha TIN yangu kutoka nilipoikatia (mkoa tofauti na nilipo) kuleta mkoa nilipo ndipo niweze kulipia mapato...Naombeni uzoefu kwa yeyote ambaye alishafanya hii, utaratibu wa kuhamisha ukoje?....

Asanteni
Andika barua kwa meneja wa wilaya/mkoa uliopo kuomba kuhamisha hiyo TIN,uipeleke ziwe mbili watazigonga mihuri moja watakupa ubaki nayo,baadaya kama ya wiki mbili utaenda mkoa unaohamishia biashara utarikuta file lako huko hapo umemaliza.
 
Asante mtaalamu, foleni ya TRA jamaa hakutaka kunisikiliza
Sasa mkuu wewe ulikuwepo kabisa kwa wahusika muhimu wanaojua haukuwauliza alafu unauliza huku ? ila nadhani kwa kuwaandikia barua officially wanaweza wakawasiliana information zako zikawa transfered from point A to B

Pia ingawa TIN ni moja ila biashara hata kama ni branch au nyongeza ya biashara nyingine inakuwa na certificate yake.., kwahio kama una biashara nyingine mkoa mwingine na hii mkoa mwingine utapewa certificate mbili zenye namba moja ila location tofauti.., kama ulifunga ile biashara ya kule itabidi / ilibidi uwaandikie barua ya kuacha kufanya biashara ili waache kuhesabu madai.., unless otherwise mpaka kesho wataendelea kukudai
 
Ni rahisi. Muandikie email au barua meneja wa mkoa husika ukimueleza kua umehama mkoa. Ni jambo la dakika 2 tu wanahamisha fasta.

Hata ukimpigia simu meneja wa mkoa uliokua ni jambo la muda mfupi tu.

Sidhani kama ni rahisi hivyo, mie nililazimishwa kufungua TIN mkoa mwingine halafu mwaka uliofuata walinisaidia lakini nikaambiwa niandike barua kule nilikoanzia ili faili langu lihamishwe na kweli nilifanya hivyo hata hivyo mwaka uliofuata tena nilipoenda kulipia nikakuta faili halijaja na kufanya jumla ya miaka 2 na baada ya hapo nafikiri faili lilikuja kwani sikuulizwa tena habari ya kuhamisha faili
 
Wadau habarini za mida hii,
Leo nilikuwa kwenye mchakato wa kulipia mapato ya biashara yangu TRA ila nilipofika kwenye ofisi zao nikaambiwa napaswa kuhamisha TIN yangu kutoka nilipoikatia (mkoa tofauti na nilipo) kuleta mkoa nilipo ndipo niweze kulipia mapato...Naombeni uzoefu kwa yeyote ambaye alishafanya hii, utaratibu wa kuhamisha ukoje?....

Asanteni
1. Kuhamisha TIN
Kuna member hapo juu white wizard kaelezea vema. Nakushauri fuata ushauri huo. ie andika barua kwa incharge ktk Tax Sevice Centre yako, state clearly unahmishia TIN yako ktk Tax Service Centre ipi, then baada ya muda rudi kufuatilia kama suala lako lishafanyiwa kazi ukiwa na copy ya barua ile uliyoomba uhamisho wa TIN

2. Kulipia kodi
Ungeomba karatasi ya malipo ya kulipia kodi hy ya mapato hata hapo ulipo ungepewa pasina kujali na tawi lako au laah. Vlvl Tax Consultant aliesajili anaweza kukuprintia pia karatasi ya malipo ukalipia hata akiwa ofisini kwake
 
Dogo nina uhakika 100% na nilichokiandika.

TRA hawana shida kuhusu kuhamisha TIN.

Nenda ofisi ya TRA iliyo karibu na wewe upate huduma.
Ndio tatizo la kufananisha fb na jf!!! Mimi nimeshahamisha TIN sana, lakini sio kwa utaratibu huo uliousema eti hata kwa simu tu!!! Hahaaa hapa jf watu hutoa ushauri/msaada kwa uzoefu walionao sio kukurupuka kama uliyosema wewe, mambo ya ki ofisi ni documentation, kwangu nina..... Kama wewe, heshima mbele
 
Mimi mwaka Huu mwezi wa 4 nilihamisha kutoka Temeke kuja Kinondoni. Nilienda TMK ni Dakika 2 tu. Wanakuambia Tayari. Ila itabidi uende na Tin No na ID yotote me nilikua na Leseni ya Udereva.

Kuna mtu aliniambia unaweza ata piga simu au ukaagiza mtu. Ila kupiga cm naona itakua sio possibble maana wanauliza ID
 
Mimi nilihamisha wiki iliyopita. Kama ulivyosema, 2 minutes. Nilikuwa na TIN Certificate yangu na kitambulisho. Walinihamisha from Mkoa wa Pwani tu DSM ( Ubungo) in 2 minutes.
 
Ni possible. Kuhamisha TIN hakuna mlolongo wowote kabisa. Ukienda mwenyewe, ukipiga simu vyote vinawezekana. Ni jambo la dakika 2 unaambiwa tayari.

Lengo ni kukurahisishia wewe mlipa kodi usipate usumbufu wa kulipa kodi.
 
Sikiliza dada, mimi na wewe tuko tofauti, mimi hii kazi ndio kazi yangu, wewe kama unaenda ofisi za umma kuonyesha makalio lazima utachelewa kupata huduma maana lazima ushikwe shikwe makalio na upigwe miti ndio uhudumiwe.

Ukienda ofisi za umma nenda kikazi utahudumiwa haraka usiende kutangaza na kuonyesha watu mqundu, utacheleweshewa huduma.
Hakuna mfanyakazi wa TRA, anaweza akawa na ushauri kama ule!!! Tofautisha fb na jf!!

Sasa angalia ushauri wako na wangu mkulima nani amepata thanks, za kutosha!! Cha ajabu unakimbilia matusi!!! Na sio kila mtu ajulikane anafanya gani huo ni utoto wa fb, pole sana
 
Mimi nilihamisha wiki iliyopita. Kama ulivyosema, 2 minutes. Nilikuwa na TIN Certificate yangu na kitambulisho. Walinihamisha from Mkoa wa Pwani tu DSM ( Ubungo) in 2 minutes.
Huo ndio utaratibu, sasa huyo jamaa mmoja eti anaongopea watu eti hata kwa kupiga simu tu wanahamisha,!!! Nimembishia eti ni mfanyakazi wa TRA, badala ya kujibu hoja anakimbilia matusi,
 
Huo ndio utaratibu, sasa huyo jamaa mmoja eti anaongopea watu eti hata kwa kupiga simu tu wanahamisha,!!! Nimembishia eti ni mfanyakazi wa TRA, badala ya kujibu hoja anakimbilia matusi,
Mimi nilishakuwaga na tatizo kama ilo. Mpaka leo sijajua hatima yangu, mwaka 2012 nilifungua TIN ya bihashara pale Mwanza. Lakini mlolongo wa kupata Leseni ya bihashara ikawa ngumu nenda uku rudi uku mpaka nikashindwa kupata Leseni ya bihashara.

Sasa mwaka 2013 nimerudi zangu home DSM. Wakati zoezi la kubadilisha wote wenye Leseni za gari kuwa na izi za electronics wakasema uwe na TIN Number. Kwenda Samora pale Posta (DSM) wakaniambia tayari TIN Number unayo nikachukua Leseni ya Gari. Mwaka 2016 nikabadilisha leseni kama kawaida lakini mwisho wa mwaka 2016 likaja zoezi la kufanya update za TIN Number zote apa Tanzania.

Sasa naenda pale Kimara Baruti kufanya update ya Tin number, wakaniambia faili lako la Tin number lipo Mwanza wakanipa namba piga uku na uko sikufanikiwa kuamisha ilo faili la Tin number kutoka Mwanza kuja Mkoa wa Ubungo wa ktk TIN Number. Sasa apo uwa najiuliza TRA, uwa ufanyaji wao upoje kwa mikoa ya TRA.

Maana ilishindukana mpaka leo sijapata muda wa kurudi pale Mwanza Tanzania kwa ajili ya kuamishia pale Kimara DSM. Na wenyewe walikuwa wananiambia piga simu lakini hakukua na response yoyote kutoka TRA Mwanza mpaka wakawa wanasema nisafiri mpak Mwanza kwa ajili ya kubadilisha iyo Tin number kuileta apo Kimara DSM

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
1. Kuhamisha TIN
Kuna member hapo juu white wizard kaelezea vema. Nakushauri fuata ushauri huo. ie andika barua kwa incharge ktk Tax Sevice Centre yako, state clearly unahmishia TIN yako ktk Tax Service Centre ipi, then baada ya muda rudi kufuatilia kama suala lako lishafanyiwa kazi ukiwa na copy ya barua ile uliyoomba uhamisho wa TIN

2. Kulipia kodi
Ungeomba karatasi ya malipo ya kulipia kodi hy ya mapato hata hapo ulipo ungepewa pasina kujali na tawi lako au laah. Vlvl Tax Consultant aliesajili anaweza kukuprintia pia karatasi ya malipo ukalipia hata akiwa ofisini kwake

Nimeenda TRA tena leo asubuhi wataalamu kuufanyia kazi ushauri wenu na nikapewa barua ya kuhamisha TIN kutoka mkoa niliokuwepo, mimeijaza nikaambiwa by jumatatu utaratibu utakuwa umekamilika; Nimeandika namba yangu pale wamesema nitapewa ujumbe. Nitawapa mrejesho wiki ijayo....

Ila nimeambiwa siwezi kulipia mapato mpaka TIN itakapohamishwa... Hapo kwenye ushauri namba 2 mtaalamu nipe maelezo zaidi tafadhali nifahamu channel ya kupitia.
 
Nimeenda TRA tena leo asubuhi wataalamu kuufanyia kazi ushauri wenu na nikapewa barua ya kuhamisha TIN kutoka mkoa niliokuwepo, mimeijaza nikaambiwa by jumatatu utaratibu utakuwa umekamilika; Nimeandika namba yangu pale wamesema nitapewa ujumbe. Nitawapa mrejesho wiki ijayo....

Ila nimeambiwa siwezi kulipia mapato mpaka TIN itakapohamishwa... Hapo kwenye ushauri namba 2 mtaalamu nipe maelezo zaidi tafadhali nifahamu channel ya kupitia
 
Back
Top Bottom