Uzi Maalum wa Marafiki zako wakubwa wa utoto na Nyakati zenu bora ambazo huwezi sahau.

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
MODS NAOMBA MSIJE MKAUNGANISHA UZI HUU.

Better days, Nice friends, Beatifull Mommonts..

Maisha yanaenda kwa kasi sanaa, kuna nyakati kipindi hicho kabla dunia haijakubadilisha na kukukalibisha kwa maovu na kila aina ya changamoto ukizikumbuka unatamani kutoa machozi kwa furaha na hata kutamani maisha yale yajirudie hata kwa masaa, lakini sasa haiwezekani sasa ni wewe dhidi ya Dunia.


Maisha ya kusubiri kitwa kula,
Maisha ya kwenda kugalagala Kwenye Matope unarudi Unavuliwa nguo zinafuliwa, unaogeshwa, unapakwa mafuta, unavalishwa nguo safi unaambiwa nenda kalale...
Maisha unaamka/unaamshwa ule..
Maisha unachagua chakula na unasikilizwa..
Maisha unaumwa na njaa wewe lakini unabembelezwa kula..

Hujui utavaa nini lakini mwishowe utavaa na utapendeza.

Hukujua, hukupanga wala kuwaza lolote kuhusu maisha yako lakini Mzazi/Mlezi ashamaliza yote na kwako Mambo ni manyoofu..

TUMIA SEKUNDE HIZI KUMUOMBEA MZAZI/MLEZI WAKO MEMA POPOTE ALIPO NA KATIKA HALI YOYOTE.

Hizo ndio zilikua zama zako, na hautokuja kuziishi tena...

Ni kipindi hiki ambacho ndio unaanza ku pata marafiki na taratibu kujifunza kupenda hasa ule upendo wa Agape.

Hakuna kikubwa katika kipindi hicho zaidi ya Marafiki wa michezo, na hawa ndio nataka tujikumbushe na matukio yetu, Achana na Marafiki wa faida wa leo hii..


Wengi wetu pengine marafiki wale hatupo nao tena karibu na wengine tumepotezana nao kabisa,
Pengine Kuhama kwa familia zetu,
Vifo, Elimu, kazi, na kila aina ya harakati za maisha yenu mapya.
lakini kumbukumbu yako kwao na nyakati zenu huzisahau.

Nani unamkumbuka(kama utakua huru kumtaja)?
Nini baina yenu unakikumbuka?
Wapi(kama utakua huru kutaja)

Binafsi kuhama hama kwa familia yangu sababu za kikazi za wazazi zimenifanya niishi na marafiki wengi lakini pia Wengi nimepotezana nao..

Kipindi tunaingia kwenye ma tairi ya magari na kubilingishana pale Mabibo external opposite na kituo cha polisi kwenye kile kijimteremko..

Kipindi tunatengeneza baiskeri za miti na kushuka nazo milimani kule kijijini,

Kipindi tunacheza mpira karibu na ofisi za kambini tunapasua vioo tunafichiana siri tunachapwa wote,

Kipindi tunapanda kwenye magari mabovu na mabehewa ya treni kucheza kule ifakara..

Kipindi Tunaenda baharini kucheza kwenye maboti ya zamani, mitumbwi, makontena yaliyochakaa na kando kando ya bahari na kuvua vijisamaki

Kipindi tunaenda porini kuwinda ndege kule kijijini Mbeya.

Zote hizi zilikua nyakati za furaha sana, michezo hii ilijaa hatari bila sisi kujijua mpaka wakubwa watuonye..

Kati ya michezo ya hatari ninayoikumbuka kuicheza ni..
Huo wa kujikunja kwenye Tairi na kubiringishwa kwenye mteremko huko utajua mwenyewe..

Kwenda kwenye pori kubwa lenye wanyama hatari kuwinda ndege na sungura tena tukiwa vifua wazi..

Kutengeneza bembea za kamba za miti ya porini na kurushana mbali chini pakiwa ni parefu na mbele ikiwa na maporomoko(hapa rafiki yetu kamba ilikatika akatuliza matako kwenye kisiki akapata jeraha kubwa)

kwenda kuogea baharini kwenye kina kirefu tukiwa wadogo kabisa..

Kulala kwenye njia ya treni na ukiisikia inakuja kusikiliza ule mtikisiko ikikaribia unakimbia(hapa nilipigwa kibao ambacho sijawahi kukishuhudia maishani mwangu)

Kucheza mpira kwenye barabara kubwa ya Mabasi.

Nina matukio mengi sana sanaa lakini naomba niwachie na ninyi.

Yote hayo Nishukuru Mungu nimekua salama, japo nina alama za kumbu kumbu za matukio ya Ajali.


Sasa sisi ni watu wazima, maisha yameturudia sisi,
Ni nyakati za watoto wetu..

Hembu share,
Kwa wale ambao nimewakumbusha mambo ya huzuni Naomba mnisamehe sana, hata mimi kuna mambo nikikumbuka naumia..
Ila hakuna jinsi maisha lazima yaendelee...

Mpe Heshima, upendo na salamu rafiki yako mkubwa wa utoto ambaye ukimkumbuka unatamani mgeishi karibu maisha yenu wote au hata mbapokutana hua unafurahi sana na kukumbushiana enzi zenu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_20200508_124418.jpg
 
Back
Top Bottom