Uzi maalum wa malezi ya watoto;Maswali na majibu

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,372
Wakuu,

Sina uhakika kama kuna Uzi hapa JF unaohusu mambo mbalimbali kuhusu malezi ya watoto ambapo watu wanaweza kuuliza maswali kupeana uzoefu wa namna ya kulea watoto hadi wanapofikia umri wa kujitegemea (kama upo basi uunganishwe)

Kama mnavyojua tunapoanza kuwa na familia hakuna mahali au chuo utasomea namna ya kulea watoto hivyo hapa tutapeana uzoefu wa namna ya kukabiliana na changamoto za malezi na makuzi ya watoto tangu wanapozaliwa.

Kwa kuanza naomba nijue ni umri upi sahihi kwa mtoto kuanza kujitegemea katika kujitawaza mwenyewe baada ya kujisaidia?(iwe kwa maji au toilet paper)

Hapa lengo ni kujua kwamba iwapo ataanza kujitawaza mwenyewe aweze kujisafisha kwa uhakika kwani tofauti na hapo inaweza kupelekea kupata magonjwa ya Mara kwa Mara kama UTI(hasa watoto wa kike)na pia magonjwa ya tumbo kama hatanawa mikono vizuri.

Nasubiri uzoefu,

Ahsante.



images%20(2).jpg
 
Back
Top Bottom