Uzi Maalum wa kupeana updates za hali ya barabara jijini Dar es Salaam

Carnivora

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
3,651
5,983
Wakuu nawasalimu.

Niende kwenye mada.

Lengo la uzi huu ni kupashana habari kila siku na saa tofauti tofauti juu ya hali za barabara jijini kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri. Kikubwa hasa ninachokilenga ni kupashana habari juu ya foleni au uhuru wa barabara kwa kila muda. Mtu anaweza kuuliza hali ya barabara na member mwingine akachangia kuelezea hali halisi anaweza kutuma na picha kuonesha namna hali ilivyo. Ili yule ambaye anapanga kuitumia barabara fulani afanye maamuzi sahihi ili kuokoa muda na mambo mengine pia.

Kila mmoja hapa nadhani ameshawahi kujikuta amestuck kwenye foleni halafu anawaza kwanini asingepita njia fulani. Lakini hakuna wa kumlaumu, hukulijua hilo. Pengine ungeahirisha safari yenyewe kabisa kama haikuwa na uharaka/umuhimu mkubwa, ukafanya jambo jengine.

Nini kimenisukuma kufanya hilo?
Leo asubuhi nilikua natumia barabara ya JK Nyerere nikielekea Kinondoni majira ya saa 3 hivi asubuhi. Njiani niliona askari polisi wengi wamesimama mmoja mmoja kila kwenye mwingiliano wa barabara. Maana yake wamejiandaa kusimamisha chombo chochote kitakachoingia njia hiyo kuelekea uwanja wa ndege. Nilipofika mataa ya Chang'ombe, JK Nyerere/Kawawa na Chang'ombe Rd zinapokutana hali ilishaanza kuwa mbaya. Gari zote zinazotoka Keko zilipigwa stop hakuna kuvuka, gari zote pamoja na bodaboda zinazotoka Karume zimepigwa stop hakuna kuvuka...hakukuwa na gari zinatoka mjini pia. Mimi kwa kuwa nilikua naenda Kinondoni niliruhusiwa kuendelea na safari yangu. Sikufahamu kulikua na msafara wa kiongozi gani.

Hapa ndio likaja wazo ningeweza kuapdate wadau kuwa huku hali ya njia si shwari kwa sasa. Hivyo mtu anaweza kufanya maamuzi yake. Lakini pia kuna kipindi cha mvua barabara huwa hazifai kupita tunaweza kupeana updates, kuna kutokea kwa ajali, labda lori limenguka na kuziba njia n.k

Natumani nimewaza vyema.

Tattoo.
 
Back
Top Bottom