Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial atakuwa huru kuondoka Manchester United katika dirisha la usajili la Januari. Mchezaji huyo wa miaka 25 yuko huru kukaa katika Ligi ya Premia lakini anaweza kutafuta fursa barani, na Barcelona inaweza kuwa chaguo (Eurosport)
 
Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski anasema "sio lazima ajithibitishe katika ligi nyingine" baada ya kushinda tuzo la mfungaji wa mabao mengi Uropa kwa kufunga mabao 41 ya Bundesliga na Bayern Munich msimu wa 2020-21. (Mirror)
 
Walakini, rais wa Barcelona Joan Laporta hajakata tamaa kujaribu kumshawishi bosi wa Manchester City Pep Guardiola arejee Nou Camp. Guardiola, 50, aliongoza Barca kushinda mataji matatu ya ligi ya Uhispania na Ligi mbili za Mabingwa wakati wa kipindi chake cha miaka minne akiwa usukani kati ya 2008 na 2012(El Nacional - in Spanish)
 
Back
Top Bottom