Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SAMAKI AINA YA SALMON.

Huyu ni samaki aliye maarufu sana duniani. Ukiachana mbali na kuwa na minofu pia mafuta ya samaki huyu ni mujarabu katika kulinda afya ya mwili dhidi ya maradhi pamoja na kusaidia ukuaji mzuri wa mwili na akili hususan kwa watoto wadogo.
 
Samaki huyu anapatikana sana kwenye mito iliyopo Amerca ya Kaskazini (North Amerca) samaki hawa maarufu wanapatikana kwa wingi sana. Miongoni mwa maajabu ya samaki hawa ni safari yao ndefu ya kutembea kutoka mto ni kwenye baharini na kurejea tena walipo toka baada ya kukaa muda mrefu wakiwa baharini.
 
Samaki hawa wanaweza kuruka maporomoko yenye urefu unaokadiriwa kufikia mita 3. Pia Salmon anaweza kukutana na sehemu ya mto ambayo ina maji kidogo au pamekauka, samaki huyu anaamua kuruka ili ayapate maji ama atasubiria mpaka maji yaingie aendelee na safari yake.
 
Wataalamu wanatueleza kuwa mnyama huyu anaweza kupajua mtoni alipo zaliwa kwa kutumia harufu ya maji. Inaelezwa kuwa samaki hawa wanaweza kutofautisha harufu za maji hata kwa kiwango kidogo sana. Samaki huyu pindi anapozaliwa kule mtoni harufu na maji ya eneo alipozaliwa anakuwa na kumbukumbu nayo bila ya kujali amekaa baharini kwa muda gani.
 
Back
Top Bottom