Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Itakua hivi bana
1594541600798.jpg
 
Hebu tupate maarifa kidogo
Kulikua na Mchina mmoja alikuja kijijini kwetu akasema anahitaji Paka, ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi wanakijiji wakahaha kusaka Paka, wakawaleta mchina akanunua wote akasepa nao.
Akarudi tena akasema vipi, naona wameadimika, sasa ntanunua kwa bei ya 35,000 kila paka mmoja, wanakijiji wakaenda mbali zaidi msituni, kamata Paka, leta kwa mchina, mchina anasepa nao.
Halafu wiki inayofuatia Mchina anasema bado anataka
Paka, saivi atanunua kwa Laki. Wanakijiji macho yamewatoka, hawana tena paka.

Mchina anasema basi ntaftieni kwa laki na
Nusu. Kesho yake inasikika kuwa kuna Mchagga
anauza Paka kijiji cha pili, anauza kwa 100,000/=, wanakijiji wanawahi fasta
wanaenda nunua Paka wote wa kijiji cha pili.
Wanarudi kijijini hawana pesa ila wana paka wakijua watamuuzia mchina fasta kwa laki na nusu, Mchina hatokei Ng'oooo!!!! Infact, yule mchina alikuwa anawakusanya tu na kuwahifadhi kule kijiji cha pili akijua ataja wauza kwa 100,000/= kwa hawa hawa wa kijiji hiki.

Huu pia ni uwekezaji
 
Back
Top Bottom