Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Njia 10 za kufanya Nywele zako ziwe za kuvutia na zenye afya.
kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa tunayoweka kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika na kukosa afya na mvuto. leo nimekuletea vidokezo vichache vya jinsi ya kutunza nywele zako.
 
1.kata ncha za nywele zako


kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. seli zinapokufa huzui nywele zinazozaliwa kushindwa kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi. lakini ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.
 
3.tumia shampoo inayoendana na nywele zako


tumia shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu na nzito. zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo . hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.
 
4.Zipe nywele nafasi


nywele nazo huitaji nafasi,kuchana nywele kila siku, kuzipaka nywele jelly kila siku, kuzichana mitindo tofauti, kuziwekea gundi na mafuta tofauti tofauti huzifanya nywele zako zichoke na kukosa afya. hivyo unatakiwa mara moja moja unazipa nywele zako nafasi ya kumupumzika. zipumzishe nywele zako kwa kusuka mtindo ya kawaida au rasta za mabutu.
 
5.usichane nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.


jaribu kuzichana nywele kwa kichanuo kikubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibub ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.
 
Njia 8 za kufanya ngozi yako iwe nzuri na ya kuvutia!
watu wengi husumbuliwa na tatizo la ngozi zao kuzeeka haraka, kukosa mvuto na kupoteza mvuto wake wa asili, wengi husumbuliwa na mapele, chunusi, ngozi kukauka, madoa na mashimo kwenye ngozi, na hii husababisha wengine kutumia gharama kubwa kununua vipodozi kwa ajili ya kutibu ngozi zao. leo nitawaletea dondoo chache tu za kufanya na kutunza ngozi yako ili iendelee kuwa na mvuto.
 
1.Tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako
watu wengi huharibu ngozi yao wenyewe bila kujua kutokana na kutumia vipodozi visivyoendana na ngozi zao, utakuta mtu ana ngozi yenye mafuta lakini anatumia vipodozi vya watu wenye ngozi kavu, au mtu mwenye ngozi kavu anatumia vipodozi vya mtu mwenye ngozi ya mafuta, hapo lazima ngozi yake itaharibika.
 
2.usilale na makeup usoni
unapokuwa umetoka nyumbani na kurudi usiku usilale na makeup usoni, hata mchana unapoamua kulala usilale na makeup, unapolala mwili huitaji kupumzika na ngozi huitaji kupumua, makeup huziba matundu ya ngozi hivyo kuzui ngozi kupumua vizuri na matokeo yake husababisha ngozi kuchoka, kuzeeka haraka na wakati mwingine kupata mapele au machunusi, hivyo kabla hujalala hakikisha umeondoa makeup zote kwa kutumia makeup remover.
 
3. safisha uso kabla ya kulala
kama hautaoga usiku au kabla ya kulala basi hakikisha umesafisha uso wako kwa maji safi na sabuni kabla ya kulala hata kama haukupaka vipodozi usoni, ngozi ya uso ni ngozi ambayo hukumbana na changamoto nyingi, hivyo ni vema ukahakikisha umesafisha ngozi ya uso kabla ya kulala ili kuipa ngozi nafasi ya kupumua vizuri
 
Back
Top Bottom