Kuhusu pesa, timu hizo za Ligi Kuu England halijawahi kuwa tatizo kwao kwenye kufanya matumizi ya mastaa wake wapya kwa ajili ya kuboresha vikosi vyao.
Katika suala la usajili, usishangae kuona mastaa hawa watano wakinaswa na wababe hao wa Big Six kwenye Ligi Kuu England dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.
Katika suala la usajili, usishangae kuona mastaa hawa watano wakinaswa na wababe hao wa Big Six kwenye Ligi Kuu England dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.
Manchester United imeripotiwa kuwa kwenye mbio kali za kumfukuzia kinda huyo wa Kiingereza ikitaka akacheze beki ya kulia baada ya Antonio Valencia kuondoka klabuni hapo kutokana na mkataba wake kufikia mwishoni.
Beki huyo wa kulia, anayekipiga huko Crystal Palace ameripotiwa kuwa na kipaji kikubwa sana hasa baada ya kuonyesha ubora kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita. Huduma yake inaweza kugharimu Euro 70 milioni.
Lakini, sasa anataka kurudi Ulaya, huku Arsenal ikitajwa kuisaka huduma yake usiku na mchana. Taarifa zinadai Arsenal inaweza kunasa huduma yake kwa Euro 25 milioni.
Timu kibao zinaisaka huduma ya mchezaji huyo, lakini huko kwenye Ligi Kuu England, Tottenham Hotspur inaripotiwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuinasa saini ya mchezaji huyo. Spurs inamtaka Ndombele baada ya Mousa Dembele kuondoka na Harry Winks kuwa majeruhi.
Vipimo vya afya viliripotiwa kuwa tatizo, lakini kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi Liverpool inarudi tena kwa kiungo huyo mshambuliaji ikitaka atue kwenye kikosi chake kuongeza nguvu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.