Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

20190516_074058.jpeg
 
Robin van Persie

Mai 12 mwaka huu, Van Persie alicheza mchezo wake wa mwisho ambao walipoteza akiichezea Feyenoord kwa mabao 2-0 dhidi ya ADO Den Haag, Mshindi huyo wa Ligi Kuu England msimu wa 2012/13 akiwa na United, aliagwa kwa heshima dakika ya 93 ambapo alitolewa na nafasi yake akaingia Dylan Vente.
 
Petr Cech

Cech, 36, mwenye rekodi ya kutoruhusu nyavu zake kuguswa kwenye mechi 202 kati ya michezo 443, aliyocheza Ligi Kuu England ‘EPL’, ataangwa rasmi kwenye mchezo wa fainali ya Europa Ligi dhidi ya timu yake ya zamani ya Chelsea, Mei 29.
 
Andrea Barzagli

Aprili 13, baada ya kupata nafasi ya kucheza, Barzagli, 38, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Italia ‘Serie A’ ambao Juventus ilipoteza kwa mabao 2-1 mbele ya SPAL, beki huyo aliyeshinda mataji nane akiwa na vibibi kizee hivyo vya Turin, alisema atastaafu mwishoni mwa msimu huu.
 
Yossi Benayoun

Mchezaji wa zamani wa West Ham, Liverpool, Chelsea, Arsenal na QPR, Yossi Benayoun, 39, kwenye mchezo wake wa mwisho akiwa na Beitar Jerusalem alionekana kuwa na watoto wake watano ambapo wote kwa pamoja walikwa wakiwapungia mkono wa kwakheri mashabiki wa timu hiyo.
 
Back
Top Bottom