Jon Moss– Sunderland

Mwamuzi, Jon Moss ni mmoja kati ya wale wenye heshima kubwa wanaochezesha Ligi Kuu England. Mwamuzi huyo ameripotiwa kuwa shabiki wa Sunderland. Alizaliwa Oktoba 18, 1970 katika mji wa Sunderland na ndio maana haishangazi kuona akiwa shabiki wa timu hiyo. Kwenye Ligi Kuu England alijiunga mwaka 2011 na moja ya mechi zake kubwa alizowahi kuchezesha ni ile fainali ya Kombe la FA mwaka 2015, wakati Arsenal walipoichapa Aston Villa 4-0.
 
Anthony Taylor– Altrincham

Mwamuzi, Anthony Taylor amekuwa na bahati sana ya kuchaguliwa kucheza mechi kubwa kwenye Ligi Kuu England. Refa huyo alizaliwa Oktoba 20, 1978 huko jijini Manchester na ameanza kujiunga na Ligi Kuu England tangu mwaka 2010. Timu inayotajwa kushabikiwa na refa huyo ni Altrincham.
 
IMG_1768.JPG

Huyu Binti Mgumu kweli aisee
 
Mike Dean– Tranmere Rovers

Moja ya waamuzi wenye umri mkubwa kwenye Ligi Kuu England akizaliwa Juni 2, 1968 huko kwenye mji wa Wirral na amejiunga kwenye ligi hiyo mwaka 2000. Mwamuzi huyo, ambaye moja ya mechi zake kubwa zilizoacha kumbukumbu alizowahi kuchezesha ni ile ya fainali ya Kombe la Ligi 2011,
 
ambapo Arsenal waliduwazwa na Birmingham kwa kuchapwa 2-1. Timu anayoshabikia Mike Dean ni Tranmere Rovers. Ndani ya mwezi huu, Mike Dean aliweka rekodi kwenye Ligi Kuu England kwa kuonyesha kadi nyekundu 100, wakati alipomntoa beki wa Manchester United, Ashley Young kwenye mechi ya kichapo dhidi ya Wolves.
 
Craig Pawson– Sheffield United

Craig Pawson alianza kuchezesha mechi za Ligi Kuu England mwaka 2013 na tangu wakati huo amekuwa mmoja wa waamuzi mahiri kabisa kwenye ligi hiyo, huku moja ya mechi zake kubwa kuchezesha ilikuwa nusu fainali ya Kombe la FA mwaka 2017, wakati Arsenal walipoichapa Manchester City 2-1.
 
915 Reactions
Reply
Back
Top Bottom