Kwenye Ligi Kuu England kuna marefa kibao waliofichuliwa timu zao wanazoshabikia, lakini jambo zuri ni kwamba hakuna hata mmoja aliyekiri kushabikia moja ya timu zinazoshika nafasi sita za juu kwa maana ya Liverpool, Manchester City, Tottenham, Chelsea, Arsenal na Manchester United.
 
Martin Atkinson– Leeds United

Mwamuzi huyo aliyezaliwa Machi 31, 1971 huko katika mji wa Bradford ameripotiwa kuishabikia timu ya Leeds United. Kwenye Ligi Kuu England alianza kuchezesha mechi mwaka 2005, huku mechi zake kubwa alizowahi kuchezea ni pamoja na ile fainali ya Kombe la FA ya mwaka 2011 iliyozikutanisha Manchester City na Stoke City.
 
Mechi nyingine ni fainali ya Kombe la Ligi baina ya Manchester United na Sunderland mwaka 2014. Atkinson ni mwamuzi wa beji ya Fifa alianza kwa kuwa mwamuzi msaidizi mwaka 1998 kabla ya kuanza kupuliza kipyenga kwenye Ligi Kuu England Aprili 2005.
 
Michael Oliver– Newcastle United

Michael Oliver ni moja ya waamuzi maarufu kabisa kwenye Ligi Kuu England kwa sasa. Mzaliwa huyo wa mji wa Ashington, alijiunga kwenye Ligi Kuu England mwaka 2010 huku timu yake anayoshabikia ni Newcastle United inayonolewa na Mhispaniola, Rafa Benitez.
 
Mechi zake kubwa baadhi alizowahi kuchezea ni pamoja na fainali ya Kombe la FA mwaka 2018, ambapo Chelsea waliichapa Manchester United 1-0 na ile pia ya Kombe la Ligi 2016, wakati Man City iliposhinda kwa penalti dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa fainali.
 
915 Reactions
Reply
Back
Top Bottom