.ALIYEKUWA kocha msaidizi wa Sir Alex Ferguson kwenye kikosi cha Manchester United, Rene Meulensteen amefichua kuwa kocha huyo kwa sasa ana furaha kubwa kutokana na Ole Gunnar Solskjaer kuirudisha timu kwenye ubora wake.
Meulensteen hivi karibuni alitembelewa na Ferguson na kuzungumzia maendeleo ya Man United tangu Solskjaer alipochaguliwa kuwa kocha wa muda kwenye kikosi hicho.
Kwa sasa anaona kama vile ni yeye yuko kwenye usukani kwa kile kinachoendelea kwenye klabu. Sir Alex, ni kama mashabiki wengine wa timu hiyo, walikuwa kwenye hali mbaya kwa kipindi cha miaka mitano na nusu.
Sir Alex anafurahishwa na Ole. Furaha kwa asilimia 100. Anafurahia mambo ya Ole. Anafurahi kwa jinsi United inavyocheza. Siku zote alikuwa akiwaambia wachezaji: ‘Nipeni kitu cha kushangilia. Kama mtaniburudisha, basi hapo mtakuwa mmewaburudisha mashabiki’. Ole amechukua hiyo na anaifanya Man United kwa sasa.”
Straika huyo Mwingereza, Kane anatarajia kurudi uwanjani baadaye mwezi huu baada ya kupata majeraha katika mechi dhidi ya Manchester United mwezi uliopita.
Lineker alisema: “Nimekuwa na wasiwasi kuhusu haya majeraha ya mara kwa mara ya enka. Inaonekana kuna tatizo mahali. Hakuna mchezaji anayetaka kuumia, lakini hapa inaonekana kuna udhaifu mahali.”
Kane alitarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili, lakini sasa anatazamiwa kurudi uwanjani hivi karibuni kwa mujibu wa taarifa zilizofichuliwa na klabu yake ya Tottenham.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.