IMG-20190111-WA0047.jpeg


Polisi wa Las Vegas nchini Marekani wametoa wito rasmi wa kutaka sampuli ya vinasaba (DNA) vya mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa tuhuma za ubakaji. Mchezaji huyo Mreno mwenye umri wa miaka 33, anatuhumiwa kumbaka Kathryn Mayorga katika hoteli moja ya kifahari iliyoko Las Vegas mwaka 2009.

Jarida la The Wall Street limeeleza kuwa wito huo wa polisi umetumwa kwenye mfumo wa Mahakama nchini Italia ili Ronaldo aelekezwe kuwasilisha sampuli hizo.

Mwanasheria wa Ronaldo, Peter S. Christiansen ameviambia vyombo vya habari kuwa wito huo ulikuwa wa kiuweledi na kwamba sio kitu kinachowashangaza kutokana na tuhuma zilizokuwepo
 
Beki wa kushoto wa Liverpool na Uhispania Alberto Moreno, 26, amesema kuwa hana mpango wa kuongeza muda mkataba wake katika klabu hiyo itakapomalizika. (Estadio Deportivo - in Spanish)
 
Mlinzi wa West Ham Reece Oxford, 20, anatarajiwa kushauriana na ajenti wake kuhusiana na hatima yake katika uga wa London Stadium. (Mail)
 
Chelsea inakaribia kuafikiana na Zenit kuhusiana na mpango wake wa kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Leandro Paredes, 24. (Sportitalia, via Metro)
 
Chelsea inapania kumsaini Gonzalo Higuain kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu - japo Juventus ina mpango kumuuza nyota huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 31. (Telegraph)
 
Winga wa England Jadon Sancho, 18, ana mpango wa kusalia Borussia Dortmund licha ya tetesi kuwa huenda akarejea katika ligi ya Premia. (Mail)
 
Everton ni miongoni mwa vilabu vinavyo ng'ang'ania kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Belgium, Michy Batshuayi baada ya mkataba wake wa kuchezea Valencia kwa mkopo kukatizwa. (Telegraph)
 
REAL Madrid inatafuta pa kuegamia. Vichapo sita kwenye mechi 18 ilizocheza kwenye La Liga si habari nyepesi.

Haiwezi kuwa ile Real Madrid inayofahamika na wengi. Luka Modric amejaribu kuwa mkweli.
 
915 Reactions
Reply
Back
Top Bottom